Sikubaliani na swala la kubakisha watoto shule kwa lengo la kutafuta ufaulu, wa Afrika embu tujue kuzingatia ratiba. Maisha ya mtaani ni muhimu mtoto ayafahamu na ajichanganye japo kwa mda mfupi wa likizo maana hao watu wa mtaani ndio atakao ishi nao mara baada ya kumaliza masomo.
Tusifikiri ya kuwa maisha ni kukariri makaratasi tu hawa wanafunzi kuna wengine watakuwa wafanyabiashara sasa atajifunza biashara wapi kama mda wa likizo mmewashikilia? Kuna wengine watakuwa wakulima atajifunza ukulima wapi kama mda wote mmemshikila? Je masoko na wateja atawatoa wapi kama hamtaki ajichanganye mtaani hata kwa mwezi mmoja?
Mimi ninachofahamu ni kuwa akili ikifanya jambo moja mda mrefu inachoka, na hata hao watototo ukiwabakisha shule kipindi cha likizo huku wakifahamu kuwa nilikizo wengi hawatasoma na kuelewa kitu kile watachofundishwa watahudhuria darasani kwa vile tu wanaogopa kuchapwa.
Kipindi cha likizo watoto hukitumia kutembelea ndugu zao kama shangazi, mjomba, baba wakubwa nk. Na hii huongeza mshikamano katika familia. Na waalimu pia mtumie muda huo kufanya kazi zenu za ziada na kutembelea ndugu na jamaa.
USHAURI WANGU KWA WALIMU.
1. Hakikishine mnamaliza syllabus kwa wakati.
2.Wakati wa likizo kila mwalimu wa somo hamkabidhi mwanafunzi mazoezi na maswali ya kutosha ambayo yatamlazimu mwanafunzi ayatafutie majibu na ayalete pindi shule ifunguliwapo tena ikiwezekana mzazi ajulishwe hilo, hii itamfanya mwanafunzi akatafute majibu kutoka kwa wenzake wa shule zingine hivyo atajifunza kitu kipya.
USHAURI WANGU KWA WAZAZI
1 Kipindi cha likizo tuwape watoto kazi nyingivsana za kufanya nyumbani, ikiwemo kupika, kufua, kuosha vyombo, kulima, kufagia mabanda ya ya mifugo, kuchunga na kukamua maziwa, kulima na kupalilia, kuuza maduka yasiyo ya vilevi nk. Hapo mtoto atajikuta hana muda wa kucheza cheza atajikuta anarefresh ya shuleni kwa kufanya jambo jipya wakati huo anawaza kuna mazoezi kapewa shuleni. Wala usimzuie mtoto kuangalia tamthilia wewe hakikisha majukumu uliyempa kayamaliza. Wala usimuingilie mambo yake ya shule maana kule atapewa mkong'oto asipofanya, wewe mpe kazi utamsikia anasema nina mazoezi nilipewa shuleni nifanye mwambie apangilie muda wake vizuri. Mtoto wa namna hii lazima awe active shuleni na nyumbani. Tusitengeneze vizazi vya makaratasi halafu akikosa ajira anazurura mtaani na hajui pakuanzia. Biashara hajui, ujasiriamali hajui, kilimo hajui, kupika hajui, kufua hajui, kufagia mabanda ya mifugo anaogopa kuchafuka, anaishia kukumbilia mjini na kujiunga na biashara haramu za kike au za kiume.