Hivi Mungu alikosa njia nyingine ya kufikisha ujumbe tofauti na Vitabu?

Njia bora unayoifikiria wewe ni ipi??--- ubora wa kitu unalinganishwa na kitu kingine la sivyo kitu kikiwa kimoja bila mbadala hicho kitabaki incomparable milele.
Hii umetoa wapi?
Ingekuwa hivi watu mpaka leo tungekuwa tunaishi misituni uchi tukiwinda wanyama na kuokota matunda maana kulikuwa hamna kitu bora kulinganisha na yale maisha..
Lakini Watu walikuwa porini ila wakafikiria kuwa hii haitoshi wakatengeneza vitu bora zaidi na kuendelea kuviboresha mpaka leo wewe upo Namtumbo unaongea namimi nipo Nanjilinji kupitia kakifaa ulikoshikilia mkononi.
 
Tatizo sio Mungu bali ni maandiko au hivyo vitabu.

Tuchukue kwa mfano wa biblia kitabu cha mwanzo ambacho inasemekana Musa ndie mwandishi wake.

Yeye alisimuliwa na Mungu, au mjumbe wa Mungu jinsi mwanzo wa dunia ya Adam mpaka pale walipo kuwa.

Huyo Musa nae alikuja kuwasimulia wengine, na hao wengine wakawa simulia wengine , mpaka pale utaalamu wa kuandika ukatokea, na ulipotokea huo utaaamu bado walikua hawaandiki kwenye karatasi kama sasa .

Kwa hiyo hiki kitabu jinsi kilivyo sasa kimepita kwingi sana na huko kwingi hakujatoka salama.

Kama alivyo sema mleta mada ilipaswa Mungu atumie njia nyingine kufikisha ujumbe wake kwa binadamu kuliko huu wa sasa.

Au aje upya kwa nyakati zetu hizi zenye teknolojia ya kisasa isio na shaka.
 
Kila kiumbe ni spesho, Tembo uspesho wake nk ukubwa wake kuliko wanyama wengine, Chui uspesho wake ni spidi kuliko wanyama wengine wa ardhini, Miti uspesho wake ni uwezo wa kubadilisha hewa na mwanga kuwa chakula, Sisimizi uspesho wake ni nguvu anaweza kubeba mara 10 ya uzito wake, Popo uspesho wake ni kuzaa na kupaa kama ndege nk. Nk.
Kwahyo hakuna eti huyu ni spesho kuliko wote, Kila kiumbe ni unique ukumbuke.

Akili, akili, akili ya binadamu ndio inayomfanya aweze kutawala wanyama wote na mazingira yote.

Tembo na ukubwa wake wote na speciality yake inaweza kuzidi Speciality ya akili ya binadamu??, all animals around us are subjected for subjugation by humans. Binadamu intelligence yake ndio power yake muhimu kuliko viumbe wote.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mkuu kuna watu wana jitihada sana na wanasoma sana mpaka wanabobea kwenye usabato, upadri, uislam, ulokole nk. Nk.

Wote hawa wanasoma kwa nia njema kabisa ya kumjua Mungu na tena kwa juhudi sana lakini wanajikuta wanafikia conclusions tofauti tofauti kabisa kuhusu Mungu.

So kama binadamu wanajitoa kuelewa maandiko lakini wanafikia conclusions tofauti mpaka Wanaanza kuuana.
Hapo tatizo sio kwa binadamu bali ni mwandishi, hakufikisha ujumbe vizuri.
Alitumia njia mbovu kufikisha ujumbe wake.
Mkuu unashauri angeleta ujumbe ili binadamu wote tuwe kitu kimoja kams malaika wake huko mbinguni??
 
Mimi kukosa ufumbuzi inamaanisha nayeye alikosa? Mbona kama unamshusha sana ase

Wewe unakosea sana kumshutumu Mungu bila sababu, Kwa maoni yako yasiyokuwa na mashiko unafikiri njia aliyoileta ni failure, kama ni failure angefanyaje??-- hapo huna jibu!!
 
Akili, akili, akili ya binadamu ndio inayomfanya aweze kutawala wanyama wote na mazingira yote.

Tembo na ukubwa wake wote na speciality yake inaweza kuzidi Speciality ya akili ya binadamu??, all animals around us are subjected for subjugation by humans. Binadamu intelligence yake ndio power yake muhimu kuliko viumbe wote.
Wewe mwenye hiyo akili ndio unaiona kuwa spesho, ila tembo yeye anakuona wewe ni spesho?
Simba anakuona wewe ni spesho?

Kutawala wanyama una maana ipi? Unaweza kumuambia Mamba njoo akakutii akaja?

Kila kiumbe by the way kinatawala mazingira yake, simba anatawala pori swala wanamkimbia, Mamba anatawala mito, Bacteria na vimelea wengine wanautawala mwili wako mpaka wanaweza kukuua...Na ukifa bado kuna viumbe watakula mpaka utaoza.
 
Hii umetoa wapi?
Ingekuwa hivi watu mpaka leo tungekuwa tunaishi misituni uchi tukiwinda wanyama na kuokota matunda maana kulikuwa hamna kitu bora kulinganisha na yale maisha..
Lakini Watu walikuwa porini ila wakafikiria kuwa hii haitoshi wakatengeneza vitu bora zaidi na kuendelea kuviboresha mpaka leo wewe upo Namtumbo unaongea namimi nipo Nanjilinji kupitia kakifaa ulikoshikilia mkononi.

Hapo mbona umeshajijibu mwenyewe!!--- zamani watu walivaa magome leo tunavaa nguo za pamba, hariri nk, sasa hapo unaweza sema pamba ni bora kuliko magome, hebu niambie ni njia gani bora ambayo Mungu angeitumia kutufikishia ujumbe wake kuliko njia hiyo ya vitabu (manabii)??!
 
Wewe unakosea sana kumshutumu Mungu bila sababu, Kwa maoni yako yasiyokuwa na mashiko unafikiri njia aliyoileta ni failure, kama ni failure angefanyaje??-- hapo huna jibu!!
Mkuu hebu fungua kidogo uelewa wako..
Mimi majibu naweza kuwa nayo au nisiwe nayo lakini hii haibatilishi hoja yangu kuwa hii njia aliyotumia amefeli.

Sasa kama amefeli ina maana ametumia njia mbovu, kwahyo ili kufaulu angetumia njia bora.

Mimi niwe naijua au siijui hiyo njia haimati kwasababu yeye ni mungu muweza wa kila kitu...Hawezi kushindwa si ndio?
 
Wewe mwenye hiyo akili ndio unaiona kuwa spesho, ila tembo yeye anakuona wewe ni spesho?
Simba anakuona wewe ni spesho?

Kutawala wanyama una maana ipi? Unaweza kumuambia Mamba njoo akakutii akaja?

Kila kiumbe by the way kinatawala mazingira yake, simba anatawala pori swala wanamkimbia, Mamba anatawala mito, Bacteria na vimelea wengine wanautawala mwili wako mpaka wanaweza kukuua...Na ukifa bado kuna viumbe watakula mpaka utaoza.

Tembo hana "conscious mind" speciality ya kitu chochote, wanyama wote wapo chini ya himaya ya binadamu na ndio maana tunaweza kuwachinja na kuwala bila wao kujitambua kwakuwa intelligencce yao ni ndogo na hivyo wanakuwa na low consciousness , wao wanakuwa driven by instincts, hapo ndipo superiority yetu inapokuja.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Sio vibaya ukimsaidia, anatusoma hapa anaweza akaleta solution
1. Malaika wawe visible...si huwa wanasema kila mtu ana malaika wake?
Sasa kila malaika anakuwa visible anakuwa anakufundisha Mambo ya Mungu kila saa ukiuliza.
Inakuwa haina haja ya kwenda kanisa hili au lile kupotoshwa na mwanadamu mwenzako maana utakuwa unapata directly from the source.

2.Aongeze uelewa wa binadamu ili wawe wanaelewa maandiko yake kama alivyokusudia ili kuepusha madhehebu kibao na mitafaruku.

3. Awabandike binadamu mafundisho yake akilini mwao, yani unazaliwa ukipata ufahamu tu automatically unakuwa unajua kila kitu kuhusu Mungu anataka nini, ila inakuwa choice yako tu..kunakuwa hakuna haja ya kwenda kusoma sehemu au kufundishana matangopori.
4.Nk. Nk.......

Anything is possible actually, yeye si Mungu bana.
Yani kuna infinite possibilities.
 
Mkuu hebu fungua kidogo uelewa wako..
Mimi majibu naweza kuwa nayo au nisiwe nayo lakini hii haibatilishi hoja yangu kuwa hii njia aliyotumia amefeli.

Sasa kama amefeli ina maana ametumia njia mbovu, kwahyo ili kufaulu angetumia njia bora.

Mimi niwe naijua au siijui hiyo njia haimati kwasababu yeye ni mungu muweza wa kila kitu...Hawezi kushindwa si ndio?

Imefeli kwa kigezo kipi??-- kwani mtu anapofeli mtihani si kunakuwa na.marking scheme??, the marking scheme saves as a comparator for the correct answer, wewe comparator yako kwamba Mungu kafeli iko based wapi??, kwa kadiri huna njia mbadala basi njia Ya Mungu itabaki successful
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hapo mbona umeshajijibu mwenyewe!!--- zamani watu walivaa magome leo tunavaa nguo za pamba, hariri nk, sasa hapo unaweza sema pamba ni bora kuliko magome, hebu niambie ni njia gani bora ambayo Mungu angeitumia kutufikishia ujumbe wake kuliko njia hiyo ya vitabu (manabii)??!
Zamani za kale hakukuwa na simu, kwahyo mawasiliano ilikuwa ni kwa mdomo tu.
Wakaja watu wakagundua simu.
Sasa kipindi kile hakuna simu kulikuwa na nini cha kulinganisha na mawasiliano ya mdomo?

Kwahyo kipindi kile mtu angesema kuwa "hii njia ya kuwasiliana kwa mdomo Ina mapungufu yake kwakuwa siwezi kuwasiliana na mtu aliye mbali"
na wao wangebisha kama wewe hivi kuwa kama hamna kitu bora cha kulinganisha na mdomo basi hiki kilichopo (mdomo) ni bora?
 
1. Malaika wawe visible...si huwa wanasema kila mtu ana malaika wake?
Sasa kila malaika anakuwa visible anakuwa anakufundisha Mambo ya Mungu kila saa ukiuliza.
Inakuwa haina haja ya kwenda kanisa hili au lile kupotoshwa na mwanadamu mwenzako maana utakuwa unapata directly from the source.

2.Aongeze uelewa wa binadamu ili wawe wanaelewa maandiko yake kama alivyokusudia ili kuepusha madhehebu kibao na mitafaruku.

3. Awabandike binadamu mafundisho yake akilini mwao, yani unazaliwa ukipata ufahamu tu automatically unakuwa unajua kila kitu kuhusu Mungu anataka nini, ila inakuwa choice yako tu..kunakuwa hakuna haja ya kwenda kusoma sehemu au kufundishana matangopori.
4.Nk. Nk.......

Anything is possible actually, yeye si Mungu bana.
Yani kuna infinite possibilities.

Kabla sijakujibu ningependa kujua wewe.ni dini gani??
 
Tembo hana "conscious mind" speciality ya kitu chochote, wanyama wote wapo chini ya himaya ya binadamu na ndio maana tunaweza kuwachinja na kuwala bila wao kujitambua kwakuwa intelligencce yao ni ndogo na hivyo wanakuwa na low consciousness , wao wanakuwa driven by instincts, hapo ndipo superiority yetu inapokuja.
Kuwachinja na kuwala ndio inatufanya kuwa special?
Unadhani ukichinja mbuzi hajitambui kuwa hapa anachinjwa? Hata kama asipojitambua sio case.

Mbona simba anamla swala tu kama kawaida na si ajabu.

Wewe kuendeshwa na conscious sijui mind haikufanyi uwe spesho kumzidi asiye na hiyo mind...
Hiyo mind yako ndio inakudanganya ujifanye kama wewe ni spesho sana.
ila ukienda mbugani wanyama wengine wanakuona kama mnyama mwingine tu.
 
Zamani za kale hakukuwa na simu, kwahyo mawasiliano ilikuwa ni kwa mdomo tu.
Wakaja watu wakagundua simu.
Sasa kipindi kile hakuna simu kulikuwa na nini cha kulinganisha na mawasiliano ya mdomo?

Kwahyo kipindi kile mtu angesema kuwa "hii njia ya kuwasiliana kwa mdomo Ina mapungufu yake kwakuwa siwezi kuwasiliana na mtu aliye mbali"
na wao wangebisha kama wewe hivi kuwa kama hamna kitu bora cha kulinganisha na mdomo basi hiki kilichopo (mdomo) ni bora?

Sasa nilichotaka ujibu si umeshajibu!!, umedai Mungu atumie malaika, atuongezeee akili ya kujua maneno yake nk, si ndio!!, mbona ulikuwa unaogopa kutoa majibu??!, bila shaka ulijua kuwa njia zako zingekuwa dhaifu sana kuliko njia ya Mungu, na ni dhaifu mno.
 
Imefeli kwa kigezo kipi??-- kwani mtu anapofeli mtihani si kunakuwa na.marking scheme??, the marking scheme saves as a comparator for the correct answer, wewe comparator yako kwamba Mungu kafeli iko based wapi??, kwa kadiri huna njia mbadala basi njia Ya Mungu itabaki successful
Mkuu em soma post ya kwanza nimeeleza failures za hii njia ya maandishi.

Kitendo tu cha kuwepo madhehebu kibao yanayosoma maandishi yaleyale na kupishana uelewa ni failure ya hiyo njia.

Alikosa njia ambayo binadamu wote duniani wataelewa anataka nini na anatakaje bila kutofautiana?

Sasa wasabato wanaamini usipotunza jumamosi hauendi mbinguni, walokole wanasema siku yoyote tu ni sabato.
Je kama Mungu mwenyewe alikuwa upande wa wasabato? Ina maana siku ya kiama hawa walokole wanaenda motoni kwa kukosea kuelewa maandiko yake?

Mifano ni mingi mno.
 
Back
Top Bottom