Uislamu umebainisha njia moja TU Ambayo Ni Quran na Sunnah ..mwenye kupita nje ya mafundisho hayo anapewa nasaha iliyonjema asipotaka kufuata juu yake...
Humo humo kwenye usilam kuna mkundi mengi yamejitokeza, ila main ni Wasunni na washia.
Tusiende mbali koote....tuanzie humohumo kwenye wasunni kuna makundi kama ma4 yamejitokeza yenye mafundisho tofauti tofauti
Kuna Hanafi,Maliki,Sha'afi,Hanbali
Hawa wote wasunni ila wanatofautiana kwenye kutafsiri Quran na maagizo ya sunnah
Mfano kwenye kuswali
Maliki wanaswali mikono ikiwa pembeni
Hanafi wanaume wanaswali ikiwa chini ya kitovu na wanawake ikiwa kifuani
Sha'afi wanasema Bismillah kwa sauti,wengine hawasemi
Hanafi wanasema ni wajibu mwanamke kufunika mikono,miguu,uso
Maliki na Sha'afi wanasema mwanamke anaruhusiwa kuachia uso,miguu na mikono wazi akiswali
Hanbali wao wanasema mwanamke haruhusiwi kuachia wazi sehemu yoyote kasoro uso wazi kipindi anaswali
Nk. nk.
Na hizo ni tofauti tu kwenye kuswali,lakini ukifuatilia utakuta wanatofautiana karibia kila sekta.
Hapo bado hatujaja kwa makundi mengine kama ahmadiya,ibadi,wasufi nk.
Sasa tuchukulie Ni dhambi mwanamke kuswali huku umeachia uso wazi..Basi inamaana kuna kundi kubwa la wasunni wasiofunika uso wanamchukiza Mungu kila wakiswali.
Haya yote wanatoa kwenye Quran na Sunna humohumo...
Sasa huoni kuwa Mungu hii njia ya maandishi inachanganya sana watu na njia mbovu sana aliyotumia kufikisha ujumbe wake?