Nani kakuambia kuwa Mungu anaweza kila kitu??, Mungu hawezi kuiba, hawezi kusema uongo, hawezi kudhulumu, hawezi kunyima haki ya mtu nk, Mungu HAWEZI kutenda mambo yote mabaya.
Ni hivi; Mungu amepanga na hakuna wa kupangua, amepanga kumuumba mtu na hatimaye huyo mtu aende akhera baada ya kufariki dunia na kufuliwa huko akhera, huko akhera kuna moto na pepo, katika moto wataingizwa wakosefu ili dhambi zao zichomwe na zikiisha ndipo wataingia peponi, ili mtu aingie peponi ni lazima afanye jitihada ya kushika mafundisho ya manabii (general case), mafundisho hayo ndio mengine yamehifadhiwa katika mfumo wa vitabu ili mtu asome na kuelewa Mungu anataka nini, kumekuwepo na mikorogano mingi katika kila dini juu ya hayo mafundisho hii inatokana na uelewa wa binadamu kuwa tofauti kwa kujua hilo ndipo Mungu kupitia dini ya kiisilamu akamtuma nabii mfuasi ili aje kufundisha dini sahihi ya Uisilamu, Uisilamu ulianzishwa na mtukufu mtume Muhammad (saw) na nabii wake Mfuasi ni Hadhrat mirza Ghulam Ahmad (as) nabii aliyeahidiwa kufika kuwaleta watu wa dini zote chini ya bendera ya Uisilamu, huyo nabii Mfuasi ndiye aliyeanzisha kwa amri ya Mungu jumuiyya ya Waisilamu wa Ahmadiyya duniani, Jumuiya hii imekuja kuvunja makundi ya dini zote duniani na kuwa kundi moja, hivyo ili kuondoa mtafaruku na miss understanding za mafundisho ya kidini hakuna haja ya kuja malaika wala Mungu kumuongezea mtu akili nk, kwani akili alizonazo binadamu Mungu mwenyewe ndiye kampa na anajua zinamtosha ili kujua neno lake.
Sasa ili umjue Mungu na mafundidho yake sahihi yasiyo na mkanganyiko ingia katika jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya .
Okay kumbe uwezo wa Mungu ni limited..ina maana kuna mambo hawezi na inawezekana hata hilo jambo la kutafuta njia bora alishindwa...Sawa.
Tuje kwenye point yako...kwa maelezo yako, nilivyokuelewa ni kuwa Mungu alikosea mwanzo kuleta maandiko yake, Watu kutokana na uwezo wao wa kuelewa wakapotoka na kukatokea makundi meengi yenye mafundisho tofauti tofauti.... Sasa Mungu akashtuka kuwa hali ni mbaya akaamua alete nabii mwingine tena mwenye maelezo mengine tena? (Maana Sidhani kama kuna dhehebu/dini nyingine iliyokuwepo yenye mafundisho sawa 100% na Ahmadiya)
Kwahyo watu wote kabla ya huyo Ghulam walikosea kutafsiri mafundisho ya Mungu.
Mungu akashtuka alipofeli ndio akamleta Ghulam arekebishe si ndio?
kutokana na Maelezo yako tunaweza kuconclude kuwa.
A:
1.Mungu alikosea/Mungu hukosea
2.Mungu hujirekebisha baada ya kukosea
3.Kama Mungu anakosea inamaana hakujua kama anachofanya kitakosanisha na kutenganisha watu, (Angejua asingeleta mafundisho yeyote angemleta tu Ghulam tokea Mwanzo)..Kwahyo Mungu hajui kila kitu
4.Kama hajui kila kitu ina maana hana uwezo wa kila kitu
Sasa kama Hana uwezo wa kila kitu na hajui kila kitu, kwanini hata tunamuita Mungu?
B:
Bado njia aliyotumia kurekebisha amefeli maana wewe unasema Ghulam ndio mwisho wa reli, Wasabato wanasema Ellen Gm white ndio mwisho wa reli, Wasunni wanasema Muhamad ndio mwisho wa reli, Waroma husema Papa ndio mwisho wa reli, Wafuasi wake husema Mwamposa ndio mwisho wa reli..
Kwahyo bado tatizo liko palepale, Ghulam hajasaidia, ila ameongezea tatizo maana nayeye ameongeza kundi lingine tena..Na sasa waahmadiya wanauliwa na wasunni huko middle east.
Inamaana Mungu ameshindwa kufikiria njia bora kuliko hawa manabii na vitabu itakayofanya binadamu wote duniani waamini kitu kimoja?