Labda niseme hivi; Mungu hawezi kutaka kitu kitakacho mvunjia utukufu wake na heshima. Mfano ndio huo kwamba Mungu hawezi kutaka kuumba Mungu mwingine wafanane naye kwa kila kitu, hilo haliwezekani kwake kwani sifa kuu ya Mungu ni upekee, umoja, oneness na hakuna kitu kinachoweza kufanana naye isitoshe hata kama ataweza kumuumba huyo Mungu hawataweza kufanana kwani huyo aliyeumbwa atakuwa bado ni kiumbe wake hivyo asilani Mungu hawezi kuumba Mungu mwingine kama yeye na wafanane kila kitu ndio maana nasema hawezi kufikiria kutaka kufanya jambo hilo kwakuwa hawezi kulitekeleza.