APEFACE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2016
- 5,316
- 9,596
Mkuu kishuleshule mara nyingi ilikuwa ni Vibwengo, hii ilivuma sana, kuna kipindi tulikuwa kwenye Hall moja tunasoma usiku ka saa 9 hivi, mwamba mmoja akapayuka "kibwengo" tulipoteana vibaya mno, mixer wengine kuumia kwa kujigonga kwenye madawati. Yaani nilivofika dom ndo nikajua nimejigonga na mlango kwenye paji la uso.Ahhh wewe kweli legend 😁. Nakumbuka tulikuwa tunaogopa kwenda shule mapema sababu ya majini..
Kwamba kuna wanafunzi waliskia harufu ya pilau, walipoifuatilia hadi chooni wakakutana na sinia limejaa pilau kuku. Kimasikhara wakaanza kula lakini chakula hakiishi. Mara paap jini akatokea na akawashurutisha wale hadi wamalize. Mwisho wa siku wakapasuka tumbo 😁😁..
Hapo ukiangalia shuleni kuna vyoo havitumiki na vimezungushiwa miti ya miba.. Unaamini 😁