Mkuu at least nimeona umeongea point, kuwa suala mtu kuwa Muslim au christians ni Imani, hapa nakupa 100% lakini Imani zipo aina 2, inayo ingia akilini na isiyo ingia akilini, na ndio maana wale wahindi wanao abudu ngo'mbe, mbuzi, nyani, nk tunawashangaa, inawezekana vipi ng'ombe au mbuzi akupe baraka Eti una oga mkojo wa ng'ombe, hii haingii akilini hata kidogo,Ni kweli kuna vitabu vimeandikwa na Paulo.
Miongoni mwa vitabu hivyo ni Warumi,Wakorinto, Waefeso, Wagalatia, Wafilipi,Wathesalonike n.k
Na vyote vipo kwenye Agano jipya.
Hakuna ubaya wowote wa uwepo wa hivi vitabu kwenye Biblia kwa sababu kwa sehemu kubwa vinamuelezea Yesu Kristo.
Wakati Yesu anaishi duniani hakuitwa Kristo, watu wengi walimwita Yesu mwana wa yusufu na wengine walipendelea kumwita Yesu wa Nazareth. Hili jina la Kristo limekuja kutumika sana baada ya kusulubishwa msalabani na kufufuka katika wafu.Tunamuita Kristo kwa sababu yeye ni wa kipekee (chosen). Alikuja ulimwenguni na kufa kwa ajili ya dhambi zetu ili sisi tuokolewe.
Ni kweli kuna baadhi ya vitabu kwenye Biblia ambavyo mwandishi wake hajulikani mfano haijulikani aliye andika kitabu cha Joshua.
Mimi naona ili mtu uwe Mkristo au Muislam unapaswa kuwa na Imani pia. Kwa sababu hata kwenye Quran mambo ni Yale Yale tu mfano wewe ukitaka kumshawishi mtu awe Muislam utamwaminishaje kwamba Quran ilishushwa na Mwenyezi Mungu ? Na pia mtu anaweza akakwambia kwamba ata amini vipi kuwa Mtume Mohammed aliishi duniani ?
Kuhusu sinagogi huo ni utamaduni wa watu. Yesu alikuwa akisali kwenye Sinagogi kwa sababu alizaliwa na kuishi kwenye Uyahudi. Wayahudi walikuwa wakienda kwenye Masinagogi kufanya ibada zao (hasa siku za Sabbath).
Watu watahukumiwa kwa Matendo yao na sio kuangalia walikuwa wakisali kwenye Jengo la Muundo upi. Mimi naamini kuna Wayahudi watakaotupwa motoni japokuwa wanasali kwenye Sinagogi.
Kwenye Wagalatia 3:15 hapo Paulo alikuwa akiongelea sana kuhusu vitabu alivyoandika (ikiwemo wagalatia yenyewe ) na sio Biblia yote kwa ujumla.
Hivi
ukisoma bibilia kwa umakini mkubwa na ukisoma quraan utaona kipi ni sahihi, tena nakushauri soma Quran then fanya utafiti na sayansi ya leo utapata mwanga, kuwa muislamu hayo ni maamuzi yako hakuna anayekupangia
Ikiwa YESU aliishi ktk mila za kiyahudi na alisali na wayahudi na hakuubiri ukristo, sasa nyie ukristo mmeutoa wapi kama si kwa Paulo?,
Kuhusu Quran kushushwa (kuteremshwa) hyo mbona ipo wazi mkuu, okay nenda kwenye kamusi ya kiswahili kaangalia hayo maneno tafsiri yake, alafu rudi ktk Quran tukio la lenyewe, mtume Muhammad (s.w) alitokewa na malaika jibril (a.s) akaambiwa asome (iqra), na mtume akawa hajui asome nini, lakini kwa sababu ya shinikizo la jibril aka anza kusoma hiyo sura (iqra bismi rab bikal lazee khaaq........) , tuishie hapa kwanza, haya hebu tupate majibu
Jibril (a.s) Katumwa na ALLAH (s.w) ashuke duniani tena aje kwa mtu maalum na amshushie maneno maalum, in short dhana n maana ya kusema Quran kariim imeshushwa ipo hapo, na usisahu huyo jibril haishi duniani na ndio mwalimu wa mtume pia yale maneno mtume aliyatamka kwa uwezo wa ALLAH, nafikiri nimekujibu Kwa 100% ingawaje siyo topic yetu