Hotuba ya Rais Samia Bungeni: Kuboresha Kilimo na Uvuvi, Kukutana na Wanasiasa, Awaonya wanaopotosha Mitandaoni, ATCL kulindwa, Wanawake kuzingatiwa

Mimi nimeona kama ujanjaunja hivi sikumsikia waliofanyiwa makosa sakata la uvuvi haram matokeo yake wahanga tukawa wenye vyombo halali sasa nashangaa kusema wataboresha watu gani?wapya ? ambao watakopeshwa au tutafute tena waje wachome nakuzishikilia mali hadi sasa kwakweli kama hamtotulipa mlaniwe navizazi vyenu siwezi kukata leseni na nikapewa kwa kitu haram
 
Katika hotuba yake Mheshimiwa SSH ametanabaisha kwamba Rais wa awamu ya tano alipoteza maisha(RIP) kutokana na matatizo ya Moyo(ripoti ya Madaktari waliokua wanamtibu).

Hivyo wale wote waliokua wanabuni chanzo cha kifo chake mtulizane na acheni mara moja KUDEMKA. Lakini kama kuna ushahidi tofauti na waliotoa Madaktari waliopewa KAZI na serikali ya kumtibu hayati basi wakaripoti serikalini na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mheshimiwa SSH itazishughulikia taarifa hizo Kwa uwazi na ukweli.
 

..wananchi hawawezi kuamini Jpm amekufa kwa matatizo ya moyo wakati walimshuhudia akipiga push-up utafikiri ni mkufunzi wa karate na judo.

..wangeambiwa tangu mwanzo raisi wao ana matatizo ya moyo ingekuwa rahisi kuelewa kilichomtokea.

..kwa sasa hivi ni rahisi zaidi kuamini habari za uzushi kuliko taarifa za serikali kuhusu kilichomuondoa Jpm.
 
Hata zikiwa hutuba 200 haina shida, tusirudi tu enzi za jiwe za kubinya uhuru wa watu.
 
Ila bora hata huyu alikuwa anahutubia, na pia hotuba yake ina matumaini walau kwa kiasi fulani.

Yule mtangulizi wake alikuwa ni kufoka foka tu mwanzo mwisho!! Na pia kutuchimba mikwara mbuzi, na kutoa maagizo yaliyojaa mihemko!
 
Tuko Pamoja Mh. Rais.

Tuna matumaini sasa.
 
Mama kazingua leo🤔🤔🤔unajua sijaamini kabisa,yaani wizara ya elimu kaisamaraizi hatari🤣🤣!
Kwa hii hotuba Watumishi wa Umma tuendelee kukaza mkanda,huyu si yeye!
TUMECHOKA maneno Sasa tunataka MATENDO.
Anaongea vitu hata havifanyiki!!!
Mama anafanya siasa Mipasho.
 
Tuko Pamoja Mh. Rais.

Tuna matumaini sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…