Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Usiniamini mimi, fuatilia fact.
Binafsi najua fact nyingi sio hear say za watu, nikiona mtu anasema uongo inanipa shida kidogo.

amini katika hili la Tancoal, HP kadanganya na aamini pia HP hayajui mengi hana ukweli wa mengi, nimemsikiliza toka day 1 kwenye hizo episodes zake, nimegundua hajui mengi na hana power.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
Hana power..wewe unayo?
 
Sio rahisi kuvishinda hivi vita ulivyoanzisha ndugu Polepole

Angalia madhira anayopitia Tundu Lissu kisa kujaribu kubadirisha mfumo ambao hao Wanamtandao ndiyo wanaufaika wakuu

Wamewalipa Vijana wengi humu mitandaoni kwaajili ya kuhakikisha wanafifisha mawazo mbadala

Hata humu JF pitia majukwaani utajionea
Nina imani mleta bandiko hili wewe ni mkenya ya Tanzania hayakuhusu. Kama yanakuhusu upo upande upi, wa wale vijana uanodai wapo mtandaoni kufifisha maelezo ya Polepole ama upo upande wa kutafuta mbinu ya kuhakikisha mawazo ya Polepole yanaeleweka kwa watanzania wengi ili wachukue hatua stahiki?
 
Nina imani mleta bandiko hili wewe ni mkenya ya Tanzania hayakuhusu. Kama yanakuhusu upo upande upi, wa wale vijana uanodai wapo mtandaoni kufifisha maelezo ya Polepole ama upo upande wa kutafuta mbinu ya kuhakikisha mawazo ya Polepole yanaeleweka kwa watanzania wengi ili wachukue hatua stahiki?
Mada ya wizi wa Rostam jadili haijalisha imeletwa na nani wewe kama ni mcha mungu kataa wizi wake mara moja
 
Duh, mambo mengine Polepole anadanganya sasa, hapo ndio ninapogundua kuna vitu pia huyu Polepole hana taarifa sahihi.

Mgodi wa makaa ya mawe mahakama ndio iliyoamua baada ya kampuni ya Caspian kuwa wanamdai Tancoal kiasi kikubwa cha hela baada ya Tancoal kupewa huduma kwa muda mrefu na kushindwa kulipa deni, sio Caspian tu, Tancoal walikuwa wanamadeni mengi baada ya kupewa huduma na kushindwa kulipa madeni na makampuni tofautitofauti.

Caspian alikuwa anatoa huduma ya haulage pale na alipeleka mitambo yake kufanya kazi kwa muda mrefu, Tancoal akawa na financial crisis na kushindwa kulipa madeni.
Kesi ikaenda mahakamani deni likaonekana ni kubwa Tancoal hawezi kulipa ikabidi wakubaliane Tancoal amaliziwe hela ili abwage hisa zake.

Tuwe tunatafuta taarifa sahihi ya baadhi ya mambo pamoja na ugomvi wetu na CCM.
Yale yale ya uongo wa Lissu na kifo cha mlinzi wa JPM pale BBC au uongo wa Dr Slaa na bomba la gas lililopita baharini kwenda Dubai.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
Kwani mkataba ulikua unasemaje?ndani ya mkataba serikali ilikua na nafasi ipi kama nayo ilikua na hisa??changanya ubongo wako
 
Narudia tena, HP inaonekana hana taarifa nyingi sahihi, hata lini Mtandao ulianza hajuia kadanganya, alichonacho ni hear says, inaonekana haujua vizuri Mtandao kama ambavyo hata marehemu JPM alivyokuwa haujui vizuri Mtandao na kujikuta anaamini baadhi ya watu kumbe nao ni Mtandao.
Kama una taarifa unazijua zaidi na Pole Pole labda hazijui sawa sawa si uziweke hapa ili tulitibu taifa hili dhidi ya uhuni? 🤔
 
kwa hiyo rostam anaijua biashara ya coal kuliko hao unaodai walishindwa kulipa suppliers? waliwezaje kuanza wakashindwa kuendelea..na serikali km mbia mwenza nayo ilishindwa kuwalipa suppliers..? yeye rostam anatengeneza pesa? au amespecialize kununua makampuni na miradi inayofeli Tanzania..?

Unapomtaja Rostam tambua ni mtu anayemiliki makampuni yaliyoajili Experts wa kada mbalimbali, Rostam haendi site wala hayuko kwenye operations zaidi yakuwa owner wa makampuni.

Hayo makampuni yake yote yana CEO's, COO's, Managers nk. sasa unapozungumzia utalaam hapo haumzungumzii Rostam unazungumzia team yake.

Maelezo yako yanaonyesha hauna uzoefu wa hizi biashara kubwa, kufail kwa biashara uliyoianzisha ni jambo la kawaida sana na yapo makampuni makubwa Dunia yaliyoshindwa na kuuzwa na waliyoyanunua wameyaendesha Kwa ufanisi.
Kufail kwa biashara Kuna factors nyingi.

Tancoal walitetereka baada ya soko la Coal kuanguka na gharama za uzarishaji kuwa kubwa na pembeni yake Kuna 40% hisa za serikali ambaye hachangii chochote kuanzia kwenye mtaji na operation costs.
Caspian (Taifa/Rostam) kama mtoa huduma alikuwa hana namna maana anamdai Tancoal na Tancoal hana uwezo wa kulipa, MLITAKA AFANYE NINI NA AMETOA HUDUMA MIAKA NENDA RUDI?

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
 
Kumbe ndo hii imeleta kizaazaa ina ukweli ndani yake sio kwa purukushani hizi wahuni sio watu wazuri wapigwe vita kokote waliko wasibaki salama ​
Kaka nimeona umeandika I'D Yako kijereshii

Ni ile kijereshii ya pale MWANZA.. umenikumbusha kijereshi ma hood enzi izo daladala za baiskeli.
 
Tunafanya Doria mitandaoni ili kuwabaini wahuni na wahaini kama nyie
Hiyo haitamuokoa Rostam na lawama kwani mmechelewa sana tayari baba yako Rostam ana pressure huko alipo mda huu
 
Back
Top Bottom