Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Humphrey Polepole: Rostam ni mfadhili mkuu wa wanamtandao, alipora 'Channel Ten', kauziwa kihuni mgodi wa Makaa ya Mawe na Serikali

Huyo aliepiga simu kutoka juu Rostam apewe mgodi wa makaa ya mawe ni nani?

Polepole kesho funguka tunajua unamjua japo hapa hujamtaja.
Rostam makandokando yake yanafahamika, si jambo geni sana ktk masikio ya watanzania. Ukakasi kwangu ninao upata kwanini kwa ubaya huu wa Rostam bado JPM alimpa tena uwekezaji wa Gas, na kuanzisha taifa gas? Hawakujua ni mfadhili wa wahuni?
 
Anaandika Humprey Polepole kwenye Mtandao wa Instagram

Kisa cha wana wa Israeli waliotaka kurudi Misri wakiwa jangwani katika safari ya kuelekea nchi ya ahadi. Leo Channel 10, TV ya Chama imempa heshima Rostam Aziz kutoa nukuu baada ya taarifa ya habari akinibananga mie, nimeona niwakumbushe Channel 10 tulikotoka nao.

Rostam ni sehemu ya CCM Mtandao, genge la kihuni linalo bagaza na kubananga CCM, Serikali, Bunge, Mahakama, Nchi na Taifa letu. Ifike pahala sote tuseme kataa wahuni

View attachment 3447453

===
Baadhi ya mambo aliyozungumza;

Akishishirikiana na wanamtandao wengine, Rostam Aziz alipora chaneli ten inayimilikiwa na chama cha mapinduzi hadi pale Hayati Magufuli apochunguza na kuirudisha kwa CCM.

Ni Mfanyabiadshara dalali, ameuziwa Mgodi wa Madini kinyemelea pasipo kufuata sheria.

Ni mfadhiri mkuu wa kundi la wanamtandao.

Ana kashfa kila kona, ndiyo maana miaka ya 2011 alijivua gamba.

Ni mbagazaji mkuu wa nchi ya Tanzania, Serikali na CCM.
Huu ni uhuni sawa na uhuni mwingine tu. haya makaa ya mawe yalikuweko Tanzania hata kabla ya uhuru, wakati wa uhuru, baada ya uhuru wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia. Kama kungekuwa na mwekezaji aliyenyimwa kuchimba makaa ya mawe hata sisi tungejua. Hata Magufuli alishindwa kupata mwekezaji kwenye makaa ya mawe.

Hii sio habari wacha makaa ya mawe yachimbwe tupate hata hela ya maji tu kuliko kuyatazama pale wakati dunia inahama kutoka matumizi ya makaa ya mawe ili kulinda mazingira. Tusipoyachimba sasa yatabaki pale ardhini milele pale dunia itakapoanza kuyapiga marufuku.
 
Kwamba Rostam ametakatisha pesa Zambia, Kenya,Tanzania nk ambako ameitwa ikulu au?

Kama huna pesa za kutakatisha hatuna Cha kukusaidia.
..tanzania ndio kichaka chake kufanya utakatishaji, huko kwingine ni km route za kutolea kinachotakatishwa tanzania.
 
Polepole muongo, rostam alianza kununua magazeti ya jenerali ulimwengu 'rai' akaja malizia channel ten,kisha CCM wakainunua channel ten, ulimwengu alianzisha raia mwema
Kumbuka polepole alikua mwenezi na wewe ni binadamu wakawaida tu aka ordinary people
 
Huu ni uhuni sawa na uhuni mwingine tu. haya makaa ya mawe yalikuweko Tanzania hata kabla ya uhuru, wakati wa uhuru, baada ya uhuru wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia. Kama kungekuwa na mwekezaji aliyenyimwa kuchimba makaa ya mawe hata sisi tungejua. Hata Magufuli alishindwa kupata mwekezaji kwenye makaa ya mawe.

Hii sio habari wacha makaa ya mawe yachimbwe tupate hata hela ya maji tu kuliko kuyatazama pale wakati dunia inahama kutoka matumizi ya makaa ya mawe ili kulinda mazingira. Tusipoyachimba sasa yatabaki pale ardhini milele pale dunia itakapoanza kuyapiga marufuku.
..pima kwanza kiwango cha ujinga na upumbavu uliopo Tanzania kutofahamu coal itumike wapi, aliyeweka coal hapa anajua vile inatakiwa itumike, siyo kuuza!
 
Gods time is the best. We rebuke every evil plans over our nation.

Ephesians 5 verse 11 to 15. Evil exposed .
 
Kuna "vyombo" vinatakiwa vijiulize kama vina ulazima wa kuwepo nchini wakati mtu mmoja amegeuza nchi mali yake.Yaani mahakama mmepigiwa simu mna taka kumnyonga mwenzenu kwa ajili ya kulinda wageni?wana ccm tukishapewa elfu 2 2 za chumvi basi hatuwezi uliza maswali magumu no wonder ule utafiti wa 2015 uli onyesha wanachama wa ccm ni wajinga na wazee.
Ni vyombo vya kuchunguza chadema tu.
 
Ulimwengu walimpora tu magazeti yake baada ya partner wake Salva Rweyimamu ku-join na wahuni ambao Jenerali alishatofautiana nao baada kuwa anaibua kashfa kadha wa kadha kuhusu wahuni (wanamtandao). However, you're right, Channel ten ilikuwa ya Francesco Tramontano under African Media Group, haikuwa ya ccm.
Huwezi porwa magazeti bwashee,waliuza
Ndiyo nashangaa polepole kudai channel ten ilikua ya ccm
 
Wewe ndiyo muongo acha kujitoa fahamu kisa ni mnufaika wa haya mateso kwa chadema
Ccm haikuwahi miliki channel ten kabla,hapo kadanganya, rostam alianza kununua magazeti ya jenerali ulimwengu,ikafuata channel ten,akawauzia CCM,hiyo ni kabla 2015
 
Uwe unakuwa na akili wewe msiwe mnatetea ujinga kisa mnabugia keki ya Taifa uhuni wa Rostamu si waleo

Kuanzia SHIVACOM zile Vocha za jero jero ! Kuja kwenye biashara za magendo yeye na Diodorys Kamala


Tuna mengi sana

Britanicca
Sasa ni kosa rostam kuwa na shivacom!?..kosa kufanya biashara!?..mimi mtu wa tabora,naijua caspian ya rostam toka 1990s,ni kosa kwake kufanya biashara?!
 
Tuambie na habari za Rostam azizi kumuua yule mxungu aliye kuja kuchunguza UJANGILI kwa kumtungua kwenye helicopter na zile shehena za siraha walizo kamatwa nazo bunduki zaidi ya 100
Silaha siyo siraha
Pili wewe sasa ndiyo utuambie kuhusu hilo maana una details
 
Rostam alinunua "Habari Corparation" kukufisha media hii kuichallenge serikati ya kikwete kuibua ufisadi,baada ya hapo waandishi nguli km Joseph Mihangwa,Johnson Mbwambo na Ulimwengu mwenyewe wakagoma kuandika habari kwa maelekezo ya Rostam... hii ndio sababu ya kuanzia Raia Mwema..
Uuze gazeti lako halafu uwe mwandishi wa hilo gazeti chini ya uliyemuuzia,try harder nigga
Ulimwengu alianzisha raia mwema right away
 
Lisu alipogusia tu ishu ya Makaa ya Mawe, uhaini ndo ukaanzia hapo? Si bure tunaambiwa hii nchi ni kama haina mwenyewe
Sio mbaya kama ajira za watanzania zinapatikana . shida nayoiona ni kwasababu gani sasa tusichimbe Chuma ili tuache kuagiza chuma maana kazi ya ujenzi wa SGR bado inahitajika reli iende mpaka Burundi, DRC na kwingine Africa na Mashariki. Kiwanda kianze na wanufaika walipe kodi basi sote tugawane hicho kidogo.
 
Vyomb vya ulinzi na usalama vijitafakari kama kweli vinaistahili hii nchi, haiwezekani mtu mmoja tena sio indigenous ashikilie uchumi wa nchi kwa kuhodhi biashara zote za maliasili yetu kuanzia gesi, chuma ,makaa ya mawe na dhahabu. How comes vyombo vimeacha hili jambo kuendelea miaka yote hii? Yaani mtu mmoja kashikilia sekta yoye ya energy na wako kimya tu?!! Hawaoni hatari ya kuingiza nchi kwenye resources curse kama ya DRC na Nigeria?

Pia kuna conflict of interests. Hatari ni kwamba mmiliki mmoja anaweza kumanipulate serikali na nchi kirahisi. Kama kuongeza bei za hizo bidhaa sababu ya monopoly yake.

Asingeweza kufanya hivyo bila kushirikiana na viongozi wa juu kabisa wa serikali, usalama na CCM. Hawa viongozi ni washirika wake wapo nyuma na mbele yake, wakimlinda na kumkingia kifua

Sababu ni uongozi wa juu kabisa unaotoa maamuzi kuhusu rasilimali, miradi hii ya kimkakati.
 
Back
Top Bottom