Sijamuelewa Polepole kwenye hili la makaa ya mawe, katika nadharia hizi mbili:
- Hakubaliani kwa Mradi huo kumilikiwa na mtu binafsi badala ya serikali.
- Au Hakubaliani kwa mradi huo kumilikiwa na Rostam Aziz kama Rostam.
Kama alitaka mradi huo kumilikiwa na serikali, binafsi nalipinga hilo kwa asilimia 100. Kwa sababu mashirika karibia asilimia 85 ya kibiashara yanayoendeshwa na serikali, yanaendeshwa kwa hasara. Matokeo yake, hii pesa ya mlipa kodi ndio wanapewa ili kuendesha miradi hiyo. Mabadiliko katika mtazamo wa uchumi wa Tanzania Tokea kwa Ali Hassan Mwinyi, Mkapa mpaka leo ni kuipunguzia mzigo serikali ya kuendesha makampuni/miradi ya kibiashara ambayo watu binafsi wanaweza kuiendesha.
Serikali ibaki kwenye shughuli za huduma kwa wananchi kama shule na hospitali n.k.
Tusikubali kurudi kule tulikotoka.
Kama suala la utaratibu haukufuatwa, hilo ni tatizo kubwa kwa nchi nzima. RUSHWA, RUSHWA, RUSHWA......
Hapa kuna hitajika ufumbuzi wa kitaifa. Na hapa naomba niwe muwazi kabisa kuwa VIONGOZI WA KUCHAGULIWA (wenyeviti wa mitaa, madiwani na wabunge) wanaposhindana kutoa rushwa kwa wajumbe, au kwa namna moja au nyingine TAMISEMI ikavuruga mchakato wa uchaguzi na kuwa pitisha wagombea wasio takiwa na wananchi. Hapa usitegemee eti viongozi hawa watapinga RUSHWA katika nafsi zao.
Vile vile mpango wa serikali kununua wabunge toka vyama vya upinzani hakuna tofauti na mbunge aliyeshinda kwa kutoa RUSHWA. Hivyo serikali hiyo haiwezi KUTOKOMEZA RUSHWA KATIKA JAMII.