SIRRO na mkuu wa Intellijensia wote wafutwe kazi maana malalamiko, uonevu, mauaji na ubambikiaji kesi watu umeshika kasi kwenye uongozi wa hawa watu wawili.

Hivyo naunga mkono hoja eitha wajiuzuru ama wafutwe kazi kwa ulazima.
 
 
Nimeona kwa nyakati tofauti huyo IGP Simon Nyakoro Sirro akiongea na wananchi, yupo defensive, amejaa dharau kwa viongozi wake. Kwa mfano akiwa huko mkoani Tanga amesema Police hawapo responsible kwa vifo vingine ila kwa wale wahusika wa moja kwa moja KAMA WALE WALIOMUUA MFANYABIASHARA HUKO MTWARA.
Je ina maana huyo Sirro hajui pia kazi ya police ni kuwa na intelligensia ya kuzuia vitendo viovu? Mbona wakati wa kuzuia mikutano ya CHADEMA wanakuwa tayari wana intelligensia yao? Vipi mbona watu wengi wanaendelea kupotea mikononi mwa police lakini yeye yupo kimya????
IGP Simon Nyakoro Sirro ameshindwa kazi, viatu hivyo ni vikubwa sana kwake, hawezi na hana uwezo wa kuongoza jeshi la polisi! Huyo Masauni pia ni dhaifu kwa Sirro ni kama anamuogopa.
Kuna kipindi alikuzogoa mheshimiwa rais, alikukashifu akisema kwa mafumbo kuwa kila lawama wanatumiwa polisi wakati wao pia wanaumizwa. Ni wakati ule ulivyowaambia polisi wasitumie nguvu za kupita kiasi.
Mheshimiwa rais, mfukuze Sirro, aondoke na hiyo pensheni yake wala hastahili huyo mwizi mkubwa.
 
Habari zenu wakuu.

Kwa hali ya kiusalama ilivo sasa sioni haja ya huyu ndugu yangu Sirro kubakia ofisini...hana maarifa wala ufanisi mwingine wa kutuvusha katika hali ya sasa.

Hali imekuwa mbaya sana, kwa sisi ambao tuna vibiashara vyetu huku mtaani tunaishi kwa wasiwasi sana. Majambazi na vibaka ni kama wako huru sasa kufanya chochote wanachotaka kwa mda wowote.

Matukio ya mauaji yameshakuwa kawaida masikioni mwa wengi sasa..na hakuna jitihada zozote za kukomesha ndio kwanza yanaongezeka.,

Kwa sasa ni vigumu kutofautisha kati ya kibaka, Jambazi na Afisa wa jeshi la polisi, wote wana lengo moja na ukicheza wanakuua.

Sirro umekabidhiwa Ua - GP kutulinda Ila kwa sasa ni kama una bet na maisha yetu. Ni bora uondoke tu uendelee kula keki ya Taifa ukiwa kwako kuliko kuchezea usalama wa maisha ya watanzania
 
Huku mkoani kwetu hali ni shwari tu,lawama zipelekeni kwa RPC wenu Simon Sirro ni wa kitaifa.
 
anasubiri afukuzwe sio ajifukuzishe kwani unadhani yeyeZIRO haijui NJAA?
 
Wenzetu Kenya nafasi kama hiyo ya IGP inatangazwa kwa uwazi wenye Sifa wanaomba,

Kunakuwa na usaili wa uwazi hadi anapatikana
Mtu mahili wa kufaa kutimiza majukumu kwa manufaa ya wananchi.

Lakini huku bado mambo yanafanyika kienyeji enyeji kwa kujuana tu kujikomba kama sio kujipendekeza.
 
 
Polisi walibebwa såna na Mwendazake, utaona wanakiburi kabisa na waliweza kuficha lolote.Wakajiona nao ni Jeshi
 
Kwa uozo uliopo ndani ya chombo unachokisimamia Kama mkuu wake huoni kuwa huenda umechoka na kuishiwa mbinu kiasi kwamba imekuwa fedheha kwako Kama kiongozi jitathimini hata ukisimama mbele ya Mh Rais uone aibu jeshi limepoteza WELEDI kwa kasi sana Tangu IGP MAHITA alipokuwepo na wewe ndio umelipeleka porini kabisaa chukua KALAMU NA KARATASI UMSHUKURU MH RAIS ILI MTAANI UHESHIMIWE MUDA NI MWALIMU MZURI UTAKUUMBUA JIUZULU ASANTE
 
Hahaaa!!njaa babaaa, ki ukweli kwa sasa jeshi la polisi limerudi enzi zile za mahita!!Said mwema alijitahidi sana kulirudisha kwenye mstari na akafanikiwa kabisa!!sasa huyu yeye ana amini ktk nguvu na vitisho tu, na sio kwenye weredi!!ila mama kwa kutoa maagizo ya kuundwa kamati ya uchunguzi, na ripoti yake ikafanyiwa kazi inaweza leta mabadiriko, chanzo ni awamu ya 5, kwani jiwe naye aliamini zaidi kwenye utumiaji nguvu na vitisho!!Kama vipi huyo kamishina mpya (Awadhi)wa jeshi la polisi zanzibar apewe u IGP, tu, kwani umakini wake unajulikana sana, wakati akiwa dar, waulize madreva wa daldala habari zake wanazo!!Siro kwa sasa mbinu zimemuishia kabisa, japo huko nyuma alionekana mtu makini sana, kabla hajawa igp!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…