Mimi sileti labda labda bali nahoji ila mnaoleta labda labda ni nyie mnaojifanya mnajua hadi walichokuwa wanakiwaza hao wahusika, mimi tu naona ule haukuwa muda sahihi kufanya shambulizi na tena inashangaza shambulizi lenyewe risasi mchana kweupe katika eneo kama lile, kulikuwa na ulazima gani hao wahusika kulazimika kufanya vile kwa mtu ambaye walikuwa wakimfuatilia kwa muda?
Inashangaza.
..hoja zako zina maana kwa watu wasio na mamlaka.
..kwa wenye mamlaka au dola wanaweza kufanya tukio lolote wakati wowote mahala popote.
..eneo la tukio liliandaliwa kwa maana ya walinzi kuondolewa na Cctv nazo zimefichwa.