Hii kauli aliyoitoa Magufuli kumwambia Spika awatimue wasaliti bungeni ili wakiwa nje washughulikiwe nae, inaonesha hapa ndipo polisi wetu walipotakiwa kuanzia uchunguzi wao dhidi ya shambulio la Lissu, ajabu polisi bado wanamsubiri Lissu arudi ili wamfanyie mahojiano.
Maneno mengi aliyozungumza Magufuli kwenye hiyo video yana viashiria vingi vya mtu aliyetaka kulipa kisasi, mfano anapomwambia Spika; "watoe huku nje tuwashughulikie, kwa sababu wakiwa kule bungeni wana immunity, wanaweza kuzungumza chochote".
Anaendelea kusema; "hatuwezi kuwa vitani, halafu tukiwa mstari wa mbele, anajitokeza mmoja wetu na kuanza kuwashambulia askari wetu, huyu tuta deal nae; bora unyamaze kimya, au ukalale".
Mpaka hapo, inashangaza bado polisi wetu hawakuona mahala pa kuanzia uchunguzi wao kuhusu shambulio dhidi ya Lissu, maneno yao yamekuwa ya kisiasa sana.