Iko siku hii clip ya Magufuli itapata viewers wengi sana. Naitunza hapa

Iko siku hii clip ya Magufuli itapata viewers wengi sana. Naitunza hapa

Swali la kuuliza wanaoshangilia hii hotuba ni nani aliyeanzisha vyama vyingi na je hao wanaoitwa waropokaji wanakuwa wanaongea mawazo yasiyo na mantiki?

Nchi zinazojulikana kuwa na chama kimoja tu ni China na Cuba.

Russia hata wawepo wapinzani wote huishia kuswekwa jela na mtu yeyote anayemkosoa Putin kama hatapigwa risasi basi atanyweshwa sumu hata akikimbilia nje ya nchi.

Huyu mwanakwendazake mliona alivyofanya kwenye uchaguzi wa 2020 na tulishuhudia yaliyomkuta na kundi lake.
 
Hapana huo ulikuwa ni ujumbe kwa wasaliti wengine pia. Wakati anaongea haya tayari mawasiliano ya tundulissu yalidukuliwa na TISS akiomba nyaraka kutoka Barrick ili awasaidie namna ya kupambana na serikali.

Kwa lugha nyingine tundulissu aliamini anapambana n Magufuli badala ya kupambania taifa. Hiyo mentality ya kuamini anapambana na mtu ndio iliyomletea ulemavu wa kudumu. Vinginevyo hadi sasa angeendelea kusimama kwenye vizimba vya mahakama akiwapambania watanzania.

Hao Tiss wako kunasa tu mawasiliano ya Tundu Lisu, hawakuona mikataba ya kihuni ya madini? Hawaoni uhuni unaondelea bandarini? Kuna yule mtu alijiunganishia bomba la mafuta na hakuna hatua ya wazi iliyochukuliwa, je hao usalama wa taifa ni kwa ajili ya kuwakomoa wapinzani wa viongozi walioko madarakani?
 
Baada hata ya miaka 1000, hii clip itaonyesha kwamba msaliti wa taifa anapaswa kuuawa! Na Magufuli at aonekana ni kiongozi bora sana aliyetimiza hilo la kudeal na wasaliti wa taifa.
Yeye alisaliti nani mbona yuko mavumbini na lissu yuko majuu anakula bata
 
Kama Magufuli aliweza kumshambulia Lissu katika kipindi hicho bila kuhofia kujulikana kwamba atakuwa ni yeye sasa ni sababu ipi iliyofanya asimmalizie baada ya kujulikana Lissu hakufa ni kwamba aliogopa nini ambacho hakikiogopa mwanzo?
Ni hicho kitu cha ajabu, Dkt Magufuli asingeweza kumuua Lisu ila ni wahuni tu kama wale waliomteka Mo
 
Kwa chini weka Kauli ya Samia pia....

Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania....

Huenda ikawa lost in translation au kutokuelewa maana ila ndio hivyo tena kama tunaunganisha statements na matukio ya baadae...

Ofcourse don't get me wrong statement ya JPM haikuwa statement ya kutoa head of state sababu indirectly vichaa wanaweza wakatumia hio statement na kufanya mambo ya ajabu wakidhani wanafanya for the country....

 
Hapana huo ulikuwa ni ujumbe kwa wasaliti wengine pia. Wakati anaongea haya tayari mawasiliano ya tundulissu yalidukuliwa na TISS akiomba nyaraka kutoka Barrick ili awasaidie namna ya kupambana na serikali.

Kwa lugha nyingine tundulissu aliamini anapambana n Magufuli badala ya kupambania taifa. Hiyo mentality ya kuamini anapambana na mtu ndio iliyomletea ulemavu wa kudumu. Vinginevyo hadi sasa angeendelea kusimama kwenye vizimba vya mahakama akiwapambania watanzania.
Barikiwa
 
Kwa wendawazimu wenzie kama alivyokuwa yeye Magufuli na wajinga kweli ni hotuba bora. Lakini kwa watu wenye akili kwenye ubongo wanakudharau. Huwezi kupanga operesheni ovu halafu ukaweka na ushahidi wa maneno kwenye hotuba.

Ila wazungu wanasema "Karma never misses a location"
Ushachanganyikiwa wewe.
 
Hii kauli aliyoitoa Magufuli kumwambia Spika awatimue wasaliti bungeni ili wakiwa nje washughulikiwe nae, inaonesha hapa ndipo polisi wetu walipotakiwa kuanzia uchunguzi wao dhidi ya shambulio la Lissu, ajabu polisi bado wanamsubiri Lissu arudi ili wamfanyie mahojiano.

Maneno mengi aliyozungumza Magufuli kwenye hiyo video yana viashiria vingi vya mtu aliyetaka kulipa kisasi, mfano anapomwambia Spika; "watoe huku nje tuwashughulikie, kwa sababu wakiwa kule bungeni wana immunity, wanaweza kuzungumza chochote".

Anaendelea kusema; "hatuwezi kuwa vitani, halafu tukiwa mstari wa mbele, anajitokeza mmoja wetu na kuanza kuwashambulia askari wetu, huyu tuta deal nae; bora unyamaze kimya, au ukalale".

Mpaka hapo, inashangaza bado polisi wetu hawakuona mahala pa kuanzia uchunguzi wao kuhusu shambulio dhidi ya Lissu, maneno yao yamekuwa ya kisiasa sana.
Yule marehemu alikuwa na roho ya koboko
 
Tatizo maagizo aliyatoa public na kunji define jinsi alivyo. Operator mkuu hakumfunda jinsi kagame anavyo dili na anaodili nao.

Kivyovyote vile mshahara wa dhambi ni mauti kama alitoa order bila shaka ameshapata adhabu yake. Na kama kweli lissu alikuwa kwenye njia ya kusaliti taifa naye amesha pata ijara yake

Hakika!
 
Kwa ulivyoandika,inamaana angetuma watu wakamuue hospitali?Unaona ilikua rahisi hivyo?
Ugumu upo wapi maana wasingetumia silaha kama wameweza kumshambulia kwa risasi mchana kweupe bila woga ndio waogope kummaliza tu kiulaini hospitali tena akiwa hali mbaya?
 
Angetaka mara ngapi? Si alitaka na akashindwa. Kudra za Mungu huwezi kuzishinda.
Alishindwa vp sasa na wakati shambulizi ni moja tu lilofanywa bahati hakufa hivyo bado kulikuwa na nafasi ya kummaliza ila haikufanyika hivyo sasa wewe unasemaje wameshindwa.
 
Back
Top Bottom