Kuna siku nilikuambia wekeni jedwali kuonyesha ujenzi wa hivyo vituo vya afya 234 vilivyojengwa kwa tozo. Baada ya jedwali lile kuwekwa mbali ya kutokuonyesha muda wa ujenzi kuanza wa hivyo vituo, bado vituo vingi kwenye lile jedwali vilikuwepo kabla ya tozo, ile ni kiashiria hata serikali hii ya Samia inaendelea na tabia ya Magufuli ya kupika data ili kupata sifa za kijinga za kisiasa. Yaani ni bonge la aibu. Hilo moja.
La pili, Haya unayosema ya watu kuzuiwa kuongea kwenye TV huyasemi kwa bahati mbaya, bali unajua fika kwakuwa taarifa nyingi ni za kupika, unajua fika ukweli utajulikana, na sifa zo uongo unazotaka mama Samia azipate hatazipata, jambo ambalo litakuumiza nafsi yako. Ni hivi, ni ngumu kuendelea kutawala watu kwa kutegemea kulinda uongo kwa vitisho, fahamu kuwa mtaji wa wajinga huwa unaisha.