Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Ni vile tu naogopa kuonekana akili za kitoto kwa kuzingatia angalizo lako. Lakini kimsingi sijaelewa leo umeandika nini... Umejaribu kutumia lugha fikirishi lakini ndio umepotea kabisa bro... Sijajua ni nidhamu ya uoga?? Au umo miongoni mwao lakini hupendi uonevu?? Unaogopa kukosa nafasi kesho?? Au shida nini bro...??? Trust me hata wachangiaji hutawapata wa kiasi kile kutokana na kuweka mada 'fungwa'... Open it up, toa wigo mpana wa michango...Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo!
Simple Mind Discuss People
Ordinary Mind Discuss Events
Great Minds Discuss Idears。
Hili ni moja ya mabandiko yangu ya kiutu uzima,ya ku discuss ideas, hakuna kutaja majina,wala ku discuss watu!。
Naomba wachangiaji tujadili hoja tuu ya msingi bila kutaja jina la mtu yoyote!。
Na ukijisikia kuwashwa washwa kutaja majina,wewe ujijue bado ni mtoto,bandiko hili sii saizi,mode ukiona mtu yoyote kataja jina lolote,futilia mbali hiyo post,tuanze kutenganisha mambo kikubwa na mambo ya watoto。
hili ni bandiko la swali,huu ni mwaka wa uchaguzi,kuna vitu tumekuwa tunaviomba vifanyike kabla ya uchaguzi wa mwaka huu wa 2025, mpaka tunaingia mwaka wa uchaguzi, vitu hivyo havijafanyika!,hii imepelekea mimi kujiuliza,hivi Inawezekana ni kiburi na jeuri ya sifanyi,kwani nisipo fanya, nisipo wasikiliza, mtanifanya nini?。Na kiukweli katiba yetu imemruhusu,anaruhusiwa kushauriwa tuu na yeyote,lakini kwenye kufikia maamuzi,atafikia maamuzi yeye kama yeye,na hawezi kuhojiwa na mamlaka yoyote!。 Na hata ikitokea akafanya maamuzi yoyote yenye makosa ya kisheria,tumempa kinga ya kutokushitakiwa popote,uless kama makosa hayo ni ya ukiukwaji na uvunjaji wa katiba ya JMT,then anashitakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 56A ya katiba!。Swali ni mara ngapi viongozi wetu wamekiuka katiba,na mahakama imetamka wazi jambo fulani ni kinyume na katiba,lakini viongozi wetu wanalitenda lakini hawafanywi lolote?。
Au ni kweli kabisa yuko real very busy sana,na hapati kabisa muda wa kutusoma?,kututazama na kutusikiliza,anawategemea wasaidizi wake tuu!,hao wasaidizi wake nao wako busy,hawajapata nafasi ya kumwambia ukweli wa ubatili wa katiba yetu na ubatili wa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyoisaini mwaka jana kuwa ni sheria batili inauokwenda kinyume cha katiba ya JMT?, hivyo tunamuonea bure tuu,kumbe masikini wa watu hajui?!。
Kwa vile huu ndio mwaka wa uchaguzi,hii sheria mpya ya uchaguzi,ni sheria batili kwasababu ina vifungu fulani ni vifungu batili,viko kinyume cha katiba ya JMT,ya mwaka 197
katiba yetu ni katiba batilifu,kutokana na awamu za nyuma,kuchomekea ubatili fulani ndani ya katiba yetu,na ubatili huo,umechomekewa kiubatili。
Mahakama Kuu
Tufanye Nini Kupata Haki?
Subject to correction...