Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Kijanaa Mkuu wa Majeshi alipaswa kudictate Wakuu wa Mzena wamtoe akafie nyumbani,sasa Daktari angeanza vipi kuwaambia wakubwa wa Mzena.
Mtu anatibiwa alafu cdf aseme arudishwe nyumbani ili mumwangushie jumba bovu ripoti kama hiyo inatakiwa aitoe dr.
 
Na tunao watu wanaodhani kujua kila kitu kama wewe msakatonge wa Chadema!

Afya ya mtu ni suala binafsi na inapofikia hatua ya umauti mfa mtarajiwa hubakia yeye nafsi yake pamoja na Mungu wake na sio katiba hizi siasa za kipumbavu za kibongo kupitia kwenye simu zinaongeza ujinga zaidi bila kutumia maarifa wala hekima.
 
Yote hiyo ni ina describe namna Magufuli alivyokuwa ana operate nje ya mfumo rasmi.

Makamu wa Rais Samia alikuwa kama picha tu, au boya. Watu ambao Magufuli alikuwa anawashirikisha mambo nyeti ya nchi ni akina Bashiru Ally, Makonda, Dotto James etc.

Kwa hiyo hata akina Mabeyo, Diwani na IGP hawakuona sababu ya kumjulisha Samia
 
Uchambuzi mzuri sana Mimi naziona possibilities zote tatu kuwa Vichwani mwa hao matop walikuwa wanamzunguka Rais kwenye Wakati wake wa mwisho, Inashangaza Sana Serikali ya Kiraia ambapo VP ni second in command anaachwa Kuwa informed mapema mpaka mzee anakufa akiwa Mikononi mwa makamanda, VP ilipaswa awa Part and parcel of the Plan
I smell something fishy
 
Huu ndiyo ukweli
 
Lakini mi navoona Vp kwa bongo ni cheo ila kipo kipo tu hakina nguvu, hata kipindi cha magu kwenye kutumbua kama sio Magu basi ni majaliwa basi hatujawahi kumsikia hangaya akimtumbua hata mjumbe wa nyumba 10.
 
Hii ni laana na ndio maana hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa viongozi wa aina hii!
 
Story za vijiweni sio ndio zilisema Magufuli kafariki siku tano Kabla ya serekali kutangaza, unaachaje kuamini taarifa za vijiweni zenye ukweli wa hivyo?
Wewe kama unaamini story za vijiwen basi kuna shida maana hao hao wa vijiwen walisha sema mzee amekufa na akawaumbua kwa kuibukia ikulu, haya maneno ya vijiweni yanaweza kukua hata wewe ungali hai
 
Wewe kama unaamini story za vijiwen basi kuna shida maana hao hao wa vijiwen walisha sema mzee amekufa na akawaumbua kwa kuibukia ikulu, haya maneno ya vijiweni yanaweza kukua hata wewe ungali hai
Hata waziri mkuu alisema rais ni mzima na anachapa kazi, kuna tofauti gani na hizo story za vijiweni? Ww ndio uendelee kuamini hizo taarifa za serekali ambazo nyingi ni za kupika.
 
Usipate mkanganyiko mkuu. Aliyekua na mamlaka ya mwisho kwakipindi hicho labda hakutaka msaidizi wake ashirikishwe kwa ukaribu
 
Logic ni moja tu kwamba Rais anakuwemo ndani ya itifaki ambayo inaangalia na kuzingatia kila kitu kiende kwa usalama na amani na ulinzi wa hali ya juu !
Hivyo basi akiwa mzima au akiwa mgonjwa Hiyo itifaki inaendelea kuwa applied, na kwamba sio kila kitu atakachotaka kufanya atakubaliwa kwa sababu kitu kinachoangaliwa zaidi ni Usalama wake kwanza !!

Mkuu wa Nchi ana umuhimu katika usalama wa Nchi kuliko tunavyoweza kufikiria,
Ndio maana ulinzi wao huwa ni wa hali ya juu sana katika Nchi yeyote humu Duniani !
Na yapo maneno mengine huwa hayaelezwi hadharani ndio maana utaona watu wanajiuliza maswali mengi kwamba mbona kasema hivi na kwanini haikuwa hivi !
Sio kila kitu huwa kinawekwa hadharani !
Vingine ni Confidential !!
 
Lakini mi navoona Vp kwa bongo ni cheo ila kipo kipo tu hakina nguvu, hata kipindi cha magu kwenye kutumbua kama sio Magu basi ni majaliwa basi hatujawahi kumsikia hangaya akimtumbua hata mjumbe wa nyumba 10.
Kutumbua ndiyo nini? Ni ujinga tu alioanzisha Magufuli kisha wananchi wajinga wakawa wanaitikia kama chorus.

Kwa mfano alimtumbua Wilson Kabwe akiwa anazindua daraja la Nyerere pale Kigamboni. Kisha Wilson Kabwe akafariki baada ya siku chache. Je wewe Raia mpya ulipata nini kwa kitendo hicho
 
Sasa mtu anakufa, madaktari washaona huyu hatoboi anakufa, unamfanyia itifaki ya usalama wa hali ya juu asiende kufa nyumbani kwake, akibaki hospitali ndiyo utazuia asife?

Itifaki haifanywi kwa sababu ya itifaki tu, inafanywa kwa rationale.

Ukiondoa hizo sababu possible nilizozitaja, rationale ya kumzuia rais anayetaka kwenda kufia nyumbani kwake asiende kufia nyumbani kwake ni ipi?
 
Tulia. 2025 kabla ya uchaguzi ndo utausikia ukweli wenyewe; Mabeyo anawaandaa tu Kisaikolojia. Mtakayoyasikia mtalazimika kumpumzisha mtu. Tulia
 
Kwa mujibu wa CDF Mabeyo Makamu wa Rais alirukwa kabisa kwenye updates za kutoka hospitalini, habari alikuwa anapewa Waziri Mkuu Majaliwa. Licha ya kwamba Makamu wa Rais ndiye mrithi wa Rais, ikiwa Rais atafariki, kikatiba.
Mkuu Kiranga Mabeyo hajazungumza kuhusu swala la Waziri mkuu kuwa anapewa updates ya Hali ya afya ya Magufuli, Ila ameelezea baada ya Magufuli Kufariki ni Majaliwa na Bashiru Alli ndio walikuwa wakwanza kabisa kutaalifiwa kwamba Magufuli katutoka kabla ya Rais Samia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…