Kuna vitu vingine tunahoji ambavyo havina mantiki. Nonsense.
Kwa maelezo ya CDF , hali ya afya ya Magufuli ilikuwa imebadilika. Ni kawaida kwa mwanadamu anapokabiliana na kifo kutanga tanga na kutafuta ahueni na namna ya kukimbia kifo. Binafsi sioni makosa ya mtu kama yule kwa hali ya afya yake ilivyokuwa. Kama baada ya masaa tu alifariki, unamuhukumuje na kumlaumu mtu ambaye ni dhahiri kabisa alikuwa ktk hatua za mwisho kuiaga dunia????
Ni kawaida kwa mwanadamu kupitia hali aliyoipitia Magufuli. Wapo wengine wakikaribia kifo huita ndugu na watu wao wa karibu sana kisha kuwaachia wosia. Hujawahi kukutana na Mgonjwa anataka labda chakula fulani???? Au anamtaka mtu fulani??? Na unakuta analazimisha kabisa?
Mkuu,
Tatizo wabongo wengi washamba hawajui instruments za basic human right zinazobeba roght of dying with dignity.
Hi ni pamoja na mtu anayeona maisha hayana maana tena (anaona anaendeleza siku za kuishi tu, lakini hana quality of life) kuamua afe tu.
Hii ni pamoja na mtu anayetumia madawa makali kama morphine ya kupunguza maumivu tu kwenye saratani, wakati ni lazima afe katika muda mfupi tu, hatoboi, kuamua afe mapema.
Hii ni pamoja na mtu ambaye anaona siku zake za kufa zimekaribia kupatiwa viongozi wa kiimani kufanya last rites anavyotaka,
Hii ni pamoja na mgonjwa aliyefikia stage hiyo kuamua afie nyumbani kwake akiwa amezungukwa na ndugu zake awaage kwa dignity ya kufia nyumbani kwake, si kufa kazungukwa na madaktari hata hawajui.
Sasa, wabongo wengi hawajasomasoma mambo haya, wanakwenda kwa kufosi tu kwamba "kwa nini afie Chato?" kama vile Chato ni sehemu isiyostahili heshima.
Ni ukimbukeni wa hali ya juu kumkatalia marehemu kufia sehemu anayotaka.
Look. Naelewa inawezekana kukawa na sababu za kumkatalia mgonjwa ombi hilo.
Mfano, kama mgonjwa anaumwa sana kiasi cha kufanya hiyo safari yenyewe ihatarishe maisha yake afie njiani, au kama kwa mfano mgonjwa anaumwa Covid na kumfanyia isolation nyumbani inaweza kuwa kazi ngumu kuliko hospitalini. Hapo ita make sense madaktari kukataa. Na hii nafikiri ndiyo ilikuwa sababu kwa upande wa Magufuli.
Lakini vinginevyo, wamemnyima mzee wa watu ombi lake la mwisho la kufa nyumbani kwake akizungukwa na familia yake.