Lissu aliitwa kwenye interview WASAFI nakugfanya kila mtu kuwa makini kutaka kujua atakacho zungumza. , ghafla wakamchelewesha na kutomjuza kinachoendelea.
Uongozi wa WASAFI FM Watamueleza Lissu, na wasipotaka waache vile vile na ikiwezekana akitoka hapo achapishe tweet/post moja nzito sana kueleza huo upumbavu wao.
Kwa kuwa mtaji wa mwanasiasa ni watu, Tundu Lissu anao hao watu, awaeleze watu wake huo mchezo wa WASAFI kwa kushirikiana na dola katili la CCM.
Wasafi walitumia jina la Tundu Lissu kuvuta wasikilizaji katika kipindi chao leo. Wameuza maudhui kupitia jina la Tundu Lissu.
Watu wengi leo wamewasha radio wamsikilize Tundu Lissu (watu ambao siyo wasikilizaji wa WASAFI FM). Wameishia kulishwa habari za Bashite na matangazo ya kubeti.
Mwanasiasa makini lazima alinde hisia za watu wake ambao waliwasha radio tangu saa 11 alfajiri ili wamsikilize na wameishia kuambiwa mahojiano yamehairishwa kutoka juu.
Lakini moreover ni nzuri zaidi kisiasa kwamba Tanzania hakuna uhuru wa vyombo vya habari na kwamba waziri wa habari anaweza kupiga simu kuzuia mahojiano ya mpinzani yasifanyike.
Mwanasiasa mkubwa mwenye sifa na jina la Tundu Lissu anazo ratiba zake za kila siku, unapompa taarifa kwamba kutakuwa na kipindi cha radio, anajianda na kuvunja ratiba nyingine, ghafla asubuhi unahairisha. Ni utovu wa nidhamu.