Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.



Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi

View attachment 2896880
Atawafungulia kesi ya madai ya usumbufu, labda nako hakimu atapewa maelekezo.
4, 4, 4 ,4.
 
Tatizo Lisu Hana self control hazingatii kanuni za TCRA akiongea vyombo vya habari

Ni mtu risk Kwa vyombo vya habari vyaweza fungiwa na TCRA labda mahojiano yafanyike Private wahariri ndio warushe Lakini akiongea Live Kuna uwezekano mkubwa chombo Cha habari kufungiwa na TCRA Kwa kukiuka maadili
Maafili gani ? Anaongeaga uwongo ? Nimekuelewa mzee lakini wameoversee risk , kutokana na ulivyosema basi wamedeal na ishue accordingly, basi kama ndio hivyo basi this country is not as free as it has been preached by people..
 
Back
Top Bottom