Uandishi kama huu unaashiria matatizo makubwa kwenye ubongo na nafsi yako.
Wenye akili timamu na utu, wanaofahamu thamani ya uhai wa mwanadamu, wanashukuru kuona hili limewezekana. China, Pakistan, Egypt, na mataifa mengi, wote wameshukuru hili limetokea. Trump alitishia kushambulia kuanzia alfajiri ya leo, Iran ikaomba iongezewe masaa 11 ili kutafakari zaidi masharti ya USA. Pakistani na Egypt ikapeleka proposal yake ya kutaka mapigano yasitishwe kwa wiki 2, ikayapeleka kwa Trump na kwa Iran. China ikaishauri sana Iran iridhie mapendekezo ya Pakistan, Iran ikaridhia. Trump akaongea na Netanyahu, wote wameridhia. Maisha ya waliokuwa hatarini kuuawa yameokolewa, mafuta yanaanza kupita kwenye mkondo wa Hormuz, na nchi zote zilizokubwa na uhaba wa mafuta, zinaanza kupata mafuta. Hili ni jambo jema kwa kila mwenye akili timamu na anayejua thamani ya uhai wa mwanafamu mwenzake. Inasikitisha sana msio na akili wala utu mnapobwabwaja kuashiria mlitaka watu wafe.
Wenye akili na roho wa Mungu wanaombea mambo yasiishie kwenye wiki mbili bali, mapigano yakome moja kwa moja, uhasama na uadui uishe, urafiki na mahusiano ya kirafiki yajengeke miongoni mwa mataifa adui.