Je, LBL sio Matapeli kama Matapeli wengine?
Status
Not open for further replies.
Mimi nimeweka ela ya kuchukua kila mwezi na nina account mbili na nishatoa ela niliyoweka nakula faida tu. Ila sialiki mtu kwa sababu najua muda wowote itabuma maana huu ni utapeli, ni pyramid scheme ya kuvutia watu. Wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. si ya kwanza wala ya mwisho. ni same kabisa na kalynda na nyingine nyingi tu hata hii ikiisha itakuja nyingine.
Sasa wana scheme ya kuwekeza mwa miezi 3, 6 na mwaka ambapo faida utakuwa unaiona lakini huwezi kuitoa. ukiwekeza mwaka unapata return ya over 1600%, kwani celine hajakwambia kuhusu hili?
Sasa hapo ndipo nadhani wizi utakuwepo. Kuna watu wanaweza ahdi chukua mkopo waweke na watu hao ni kama wewe ambaye tayari wamekuonjesha asali, unaweka tusema milioni 5 ukitegemea kuvuna milion zaidi ya themanini na kitu. hizi utazikuta kwenye kipengele cha wealth fund.
Hapo ndipo watu watapigwa an kulia na ksuaga meno. Hawa na matapeli, wa kwanza kula wa mwisho kuliwa. LBL imeanza nadhani mwezi wa saba, hizi raha uanze nazo sio ishafikisha mieiz 6 unaweka ela nyingi kuna watakao kuja kulia. kama si sasa baadaye lakini ni utapeli.
Bora umeandika ukweli
 
Najua itakavyoisha kwa sababu mimi nimeingia vikampuni uchwara vingi vya hivi na mwisho wake naujua. Sasa hivi kwanza siwezi mwalika mtu ajiunge kwasababu ishatimiza miezi kadhaa na muda wowote inaweza kubuma ikasepa na ela ya mtu akakulaumu. ndo maana sialiki mtu. hizo akaunti zangu nimejialika mwenyewe kutokea kwenye akaunti moja.
Yani unajikiona lbl ni kile kile cha kalynda tofauti huko ulikuwa unaambiwa na process orders, lbl unatazama video ambazo unakuta ni zile zile week nzima.
LBL unaambiwa kampuni imesajiliwa sijui london. Hivi kama uwekezaji ungekuwa rahisi hivi, unadhani balkshire wangeenda kuwekaza dollar milioni 260 kwenye kampuni ambayo faida yake itaanza kutengenezwa baada ya miaka 10 na huenda ikafa kwa sababu ni startup?
Nachosema, kama umewekeza huko kula ila kwa kuita watu wakaweka pesa kuna ambao wataweka na itabuma kabla ya hata kurudisha fedha yao na watakulaumu. Mimi ni mtu ambaye sipendi lawama. Na nimeweka fedha nikijua risk zake.
Pia ingelikuwa ni kampuni genuine ela ingekwua inawekwa kwa lipa namba, sio kuituma kama unamtumia mtu na kila wakati jina tofauti ili sever isome msg zilizopokelewa ilinganishe na namba iliyotuma hiyo fedha ndo iupdate.
Haya maisha ni betting kwa kila kitu, ndo maana huwa namshangaa mtu anayemcheka mtu anayebet mechi za mpira huku yeye mwenyewe amelima shamba au anakodisha chumba ili afanye biashara, anakodi shamba, ananunua mbegu, mbolea na anaweka vibarua kana kwamba anajua mvua itanyesha inayohitajika, nzige hawatakuwepo, soko litakuwa shwari, nk. ukishawaza hivyo unaweza usilime wala kufanya chochote, usitishe watu wasifanye biashara au kilimo kisa wewe ulipofanya mara mbili hukufanikiwa.
 
Narudia tena, mtu aingie akijua kuwa huu ni utapeli muda wowote utaisha. Mimi nimeingia nikijua kuwa ni utapeli muda wowote unaweza kupoteza ela yote na hiyo ni lazima. Ipo siku tutarudi kwenye thread hii wakishasepa na kijiji.
So, mimi sialiki watu kwa sababu najua muda wowote inaweza kuisha na mtu akanilaumu. mtu kama anaingia aingie mwenyewe kwa mapenzi yake.
Niliona kipindi cha kalynda watu hadi wakakimbia jiji kwa kudaiwa na waliowaingiza.
 
Naomba nielekeze hapa kwenye kuwa na akaunti zaidi ya moja. Nikitumia line nyingine yenye jina langu ilani mtandao mwingine itakubalika au inabidi nitafute line yenye jina tofauti?
 
Naomba nielekeze hapa kwenye kuwa na akaunti zaidi ya moja. Nikitumia line nyingine yenye jina langu ilani mtandao mwingine itakubalika au inabidi nitafute line yenye jina tofauti?
Itakubali ila wakikugundua watakufungia
 
ni suala la muda tu sasahivi mtaanza kulia watanzania hua hawajifunzi
 
Naona mnaitana tu ili bomu likilipuka mfe wengi🤣🤣
 
kuna kulia na kucheka, mimi hadi saiz nachekelea tu
Wanawapa nyinyi wa kwanza kwanza ili mshawishike na kuvutia wengine si unaona hizo link mnasambaza za kupata commission mkishajaa jaa wanasepa mazima. Hata kutega ndege lazima uweke mtama au pumba na wazilezile ili wajae kabla hujavuta kamba.

Kila la kheri
 
Whatever
 
Nikampuni ambayo ukiweka pesa kidogo kuna pesa unalipwa mwaka mzima kilasiku. Kuna video ukazaa unatakiwa uzi view. Ila sijaielewa vizuri. Naomba maelezo kwa mwenye kuijua
Halafu mnarudi kuja kufungua uzi mkisha tapeliwa...ukitaka hela izae ukiwa umelala nunua Bond za serikali na Wekeza kwenye fixed account haya mambo ya vikampuni uchwara utapigwa tuu MATAPELI.
 
wewe umo tena kwa akaunti 3 afu unawatisha wenzio wasije ili ule pesa pekeyako!!, Mimi ninazo 2 zote P3 na nahamasisha watu watu waje tupige pesa kwa pamoja.
Sasa kuna nyingine hiyo ina faida kinoma kama kawaida wa kwanza kula wa mwisho kuliwa nisharuka nayo. hiyo 200k inakupa 28500 kila siku na hufanyi chochote. imeanza tarehe nne nimeiwahi mapema msemo ni ule ule wa kwanza kula wa mwisho kuliwa.
 
ipi hiyo? naitaka
 
Nikampuni ambayo ukiweka pesa kidogo kuna pesa unalipwa mwaka mzima kilasiku. Kuna video ukazaa unatakiwa uzi view. Ila sijaielewa vizuri. Naomba maelezo kwa mwenye kuijua
We unaijua, sema unataka nasi tuijue!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom