Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Tofautisha mwanamke msomi na yule wa kipindi cha nyuma, hawa wenye ajira ni jeuri,kiburi,na usawa wa kijinsia kwamba 50/50.
Mwanamke ni yule yule hajawahi badilika!!huyu msomi amechafuka ubongo baada ya kujazwa ujinga wa 50/50!!

Warudi kwenye misingi!
 
Nahudumia pale ninapotaka na sio lazima kama mume yupo na anao uwezo wa kucover kila kitu.
Kwa nn isiwe wajibu wako hali yakuwa familia ni ya kwetu sote?
 
Usaidizi hauna mjadala!!yaani hilo ni amri kuu ya uumbaji!!

Binafsi mke wangu anashiriki ipasavyo Kila jambo!!coz ni msaidizi wangu mkuu!!

Swala la kiburi ,dharau,usaliti na mengineyo yakijitokeza huo ni uzembe binafsi hauna uhusiano na majukumu ya Kila siku!!
 
Kila mtu awajibike kwa familia yake, be proud kuhudumia familia yako. Ukishaweka material things mblele na ubinafsi kwenye ndoa yako unaharibu ustawi wa familia yako.
 
Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wake
Hivi kwanini mawazo yawe mwanaume afariki kwanza na siyo mwanamke?
 
Mimi ni housewife. Nafanya shughuli zote za nyumbani unazozijua wewe yeye jukumu lake ni kusupport financially. Akitaka na mimi nianze kutoa pesa zangu basi akubali na yeye kuosha vyombo. Ipo hivyo.
Sisi tunaongelea wanawake wanao shindwa kutimiza majukumu yao ya kiasili kwa sababu ya ubize wa kutafuta hela.
 
Sisi tunaongelea wanawake wanao shindwa kutimiza majukumu yao ya kiasili kwa sababu ya ubize wa kutafuta hela.
Mada inasema kuchangia kifedha.
 
Kwa akili yako wewe unadhani kazi ya mwanamke ni nini kwenye familia
Kazi ya mwanamke ni kusaidia kujenga familia kiuchumi, kijamii, na kihisia. Hata hivyo, kuchangia fedha sio lazima; kila mmoja anachangia kwa njia yake, na usawa na umoja kwenye familia ni muhimu zaidi kuliko kutegemea michango ya kifedha pekee.
 
Nafanyia mambo binafsi ambayo yeye alishindwa kuyatekeleza. Na zingine nanunua mahitaji ya nyumbani hasa ya jikoni.
Sasa hapo si tiyari kipato chako kimechangia majukumu ya kufamilia?

Sisi tunaongelea wanawake wasio taka pesa yake kuguswa.
 
Vijana hawa watoto wa masingle mother hawakuelewi, wengi baba zao waliterekeza familia mama kabaki anapambana na maisha mwenyewe, baba anarudi anakuta watoto wamekuwa, hivyo na wao wanataka wake zao waishi maisha hayo kwasababu mama zao waliishi hivyo, utakuta mzazi anamwambia kijana oa mke mwenye kazi, kwahiyo siku kazi imeisha sijui amfukuze !
 
“Kila familia ina mpangilio wake. Muda wa kutunza familia haujapimwi kwa masaa, bali ni jinsi gani kila mmoja anavyochangia kwa pamoja.”
Kutunza familia ni suala jumuishi, iweje unajiona unawajibika kwingine kote isipokua hapo kwenye hela tu?
 
Jukumu la mke kuhudumia familia (ahudumie mume, watoto na ku ndugu za mume/zake wa karbu )

Sasa inapotekea muda wake anautumia kuzalisha mali (kufanyakaz) inamaan anapaswa kushirk maendeleo ya familia kwakutoa pesa au kipato sio chini ya 60% ku replace majukumu ya ndoa.
 
Ikiwa tunaongelea 50/50, basi inapaswa kuwa sawa kwa pande zote. Kama mwanamke anachangia kifedha na kazi za nyumbani, basi ni haki pia mwanaume achangie katika malezi ya watoto na majukumu ya familia. Usawa unapaswa kuwa katika kila eneo la ndoa, sio tu kwenye pesa, bali pia katika kulea watoto na kusaidiana kwa kila mmoja. Kila mmoja anapaswa kuchukua jukumu lake bila kumwacha mwingine kubeba mzigo peke yake.
 
Hii ni mojawapo ya fikra za kimasikini, familia ya watu 10 kumtegemea mtu mmoja kwa kilakitu wakati mwenza anaingiza kipato ni upuuzi wa kiwango Cha juu cha mwisho.

Labda niwaulize swali jepesi, huu utaratibu mmeutoa wapi?

Niwakumbushe naona mnataka kujisahaulisha:-

Wazee wetu, mume na mke walishiriki kujenga uchumi wa familia. Kama ni wafugaji mke alishiriki kikamilifu kwenye ufugaji hakuwa mama wa nyumbani, na kwa wakulima mama alishiriki kikamilifu kuhakikisha mji wake una chakula cha kutosha.

Mazao yaliyolimwa na mke ndiyo yalinunua mahitaji mbalimbali ya familia, mifugo iliyosimamiwa na mke ndiyo pesa yake ilinunua mahitaji mbalimbali ya familia.

Kwa zamani kilimo na ufugaji ndizo zilikuwa shughuli za kiuchumi. Wanafamilia wote walishiriki kuhakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu.

Sasa huu utaratibu wa uchumi wa familia kujengwa na mwanaume pekeake ninyi mmeutoa wapi??? Huu utaratibu wa pesa ya mwanamke inafanya mambo yake binafsi tena nje ya ndoa mmeutolea wapi?
 
Mwanaume ;
Kiongozi
- Atunze familia kikipato, kiuongozi & kiulinzi

Mwanamke;
Msaidizi
  • Atunze mume, & kufanya nyumba iwe nyumbani
  • Abeba mimba, zaa kwa uchungu na kulea
Hii ndio 50/50

Ukitaka mke atoe hela, unataka iwe 75% mchango wake na wako uwe 25%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…