Prof Phraoh AI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 1,269
- 2,311
hayo maandiko ungeyajuaje wewe usiyefungamana na dhehebu lolotemimi imani yangu imejengwa kwa misingi ya ushuhuda wa yesu kristo ushuda wa yesu kristo ndio roho ya unabii, kwasababu imeandikwa kwenye unabii wenye ushuhuda wa yesu kristo ndio watakao okolewa "ASOMAE NA AFAHAMU"
Mimi nina mshuhudia yesu hakuwa msabato nina mshuhudia yesu hakuwa mkatoliki wala mlokole, wala hao mitume na manabii wote, nina shuhudia kweli yote kuwa hakuna andiko au maelekezo yanayo nitaka kujiunga na dhehebu lolote lile je wewe unaniuliza nipo kwenye dhehebu gani kwa maagizo ya nani ?
jiulize na wewe upo kwenye dhehebu flani kwa maagizo ya nani ndivyo mungu alivyotuagiza hivi au upo upo tu unaamini lakini huelewi ?
ujuzi na hekima ni kipaji na hivitoki kwenye makanisa pekee inategemea na mtu mwenyewe,hayo maandiko ungeyajuaje wewe usiyefungamana na dhehebu lolote
kanisa lilohifadi na kutumia nguvu kubwa kusambaza habari njema kwa watu wote,
alafu dhehebu ni machipukizi na matawi hayo ambayo kimsingi yametokana na kanisa la kwanza, Kanisa Katoliki sio dhehebu
Wewe unaamini tu kuwa kuandika yesu kwa erufi kubwa ni kutoa heshima kwa yesu lakini niki kuuliza ni vipi erufi kubwa inaleta heshima huwezi kunijibu nina uwakika kwasababu wewe unauelewa mdogo sana, mtizamo wako wa kiimani ni hasi hakuna uhusiano wowote kati erufi kubwa na ndogo kuhusisha na suala la heshima so negativeKingine lipe basi hili jina heshima yake stahiki.
Huwa inaleta maana nzuri zaidi likiandikwa ”Yesu Kristo”.
ni watu wanaokusanyika pamoja kumuomba Mungu kwa pamojaujuzi na hekima ni kipaji na hivitoki kwenye makanisa pekee inategemea na mtu mwenyewe,
hebu niambie nini maana ya kanisa usi Google niambie wewe unaelewaje ?
kumbe wewe ni mbumbumbu hiviKingine lipe basi hili jina heshima yake stahiki.
Huwa inaleta maana nzuri zaidi likiandikwa ”Yesu Kristo”.
safi hiyo ndio maana ya kanisa sio jengo bali ni watu mfano mimi na wewe, ni vyema pia kukusanyika kufanya ibada lakini sharti watu unaokusanyika nao wanafuata ibada sahihi na miongozo ya kibiblia, lakini unapo kusanyika tu kwenye dhehebu flani ambalo alifuati biblia bali utaratibu wa uzushi unapo fanya nao ibada unakuwa muasi kwa mungu.ni watu wanaokusanyika pamoja kumuomba Mungu kwa pamoja
"wanapokusanyika wawili au watatu nipo kati yao"
Umesema waprotestant wanaamini kuwa hakuna haja ya kuwa na kiongozi mkuu wa kanisa kwakuwa Yesu anatosha.Ndugu zangu wa Kanisa kubwa duniani, Kanisa Katoliki - poleni sana kwa msiba mzito. Wakati maombolezo yakiendelea, naomba tuongee kiutu uzima; kwa heshima na upendo.
Kwanza ninawapongeza: mkiwa Kanisani, mnaonyesha heshima kubwa kwa Mungu. Sasa naomba mnijibu swali hilo: Je, ni kweli kwamba Mtume Petro ndiye Papa Mtakatifu wa Kwanza?
Nimesikia mnafundisha kwamba Mtume Petro ndiye aliyeteuliwa na Yesu kuwa msingi wa Kanisa au Papa wa kwanza. Mnanukuu Mathayo 16:18 na kusema kwamba katika Andiko hilo Yesu alimwambia Petro, “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu.” Kwa tafsiri yenu, “mwamba” huo ni Petro mwenyewe, na hivyo mnamuona kama Papa wa kwanza. Mnaamini kwamba, mamlaka ya Petro kama kiongozi wa mitume yaliendelezwa na Mapapa waliomfuata, wakiwa viongozi wa juu wa Kanisa la Kristo duniani. Ni kweli?
Kama ni kweli, mbona mtazamo wa Kiprostestanti unatofautiana na mafundisho yenu. Waprotestanti wanasisitiza kuwa msingi wa Kanisa sio mtu binafsi, bali ni Yesu Kristo mwenyewe (1 Wakorintho 3:11), na kwamba “mwamba” aliouzungumzia Yesu ni Yeye mwenyewe(Yesu) kama Petro alivyokiri: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16).
Kwa mtazamo wa Kiprostestanti, Petro hakuwa Papa, kwa sababu hakuna ushahidi wa kibiblia unaoonyesha kuwa alipewa mamlaka ya kipekee juu ya mitume wengine. Na wakati wa Kanisa la kwanza mfumo uliopo leo wa kipapa, haukuwepo.
Waprotestanti wanaeleza tena kwamba Viongozi wa kwanza wa Kanisa walifanya maamuzi yao kwa ushirikiano (Mdo 15), sio kwa mamlaka ya mtu mmoja(Papa). Wanasimama na Andiko la Waefeso 5:23 linalosema kwamba Yesu ndiye Kichwa cha Kanisa. Wanaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeliongoza Kanisa lote sasa, na sio kiongozi mmoja wa kimwili. Wananukuu Yohana 16:13
"Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote."
Hoja hizo mnazijibuje?
Ntashukuru sana nikipata majibu ya swali langu na majibu kuhusu hoja hizo za Kiprotestanti. Majibu yajengwe kwenye Maandiko Matakatifu(Biblia). Tumsifu Yesu Kristo.
Utakuwa na shida mahali mkuu hauko sawa.mimi imani yangu imejengwa kwa misingi ya ushuhuda wa yesu kristo ushuda wa yesu kristo ndio roho ya unabii, kwasababu imeandikwa kwenye unabii wenye ushuhuda wa yesu kristo ndio watakao okolewa "ASOMAE NA AFAHAMU"
Mimi nina mshuhudia yesu hakuwa msabato nina mshuhudia yesu hakuwa mkatoliki wala mlokole, wala hao mitume na manabii wote, nina shuhudia kweli yote kuwa hakuna andiko au maelekezo yanayo nitaka kujiunga na dhehebu lolote lile je wewe unaniuliza nipo kwenye dhehebu gani kwa maagizo ya nani ?
jiulize na wewe upo kwenye dhehebu flani kwa maagizo ya nani ndivyo mungu alivyotuagiza hivi au upo upo tu unaamini lakini huelewi ?
Hujanielewa vizuri. Mzizi wa hoja yangu uko kwenye cheo cha Papa. Viongozi wengine kama Maaskofu, na Wachungaji, wametajwa kwenye Biblia. Lakini Papa simuoni kwenye Maandiko.Umesema waprotestant wanaamini kuwa hakuna haja ya kuwa na kiongozi mkuu wa kanisa kwakuwa Yesu anatisha.
Naomba uwaulize kwanini wana viongozi makanisani mwao?
unamaanisha kina nani hao ambao hawafuati biblia?safi hiyo ndio maana ya kanisa sio jengo bali ni watu mfano mimi na wewe, ni vyema pia kukusanyika kufanya ibada lakini sharti watu unaokusanyika nao wanafuata ibada sahihi na miongozo ya kibiblia, lakini unapo kusanyika tu kwenye dhehebu flani ambalo alifuati biblia bali utaratibu wa uzushi unapo fanya nao ibada unakuwa muasi kwa mungu.
Rc mchanga naomba kukuzwa kiimani.
Nisaidie vifunngu vinavyoagiza kusali rozari
Je Yesu alisali rozari?
Pale tunapomsujudia maria, na kumuomba atuombee, kuna ushahidi wa kimaandiko kuhalalisha hayo?
Umesema waprotestant wanaamini kuwa hakuna haja ya kuwa na kiongozi mkuu wa kanisa kwakuwa Yesu anatisha.
Naomba uwaulize kwanini wana viongozi makanisani mwao?
ili kujua kanisa lako kuwa linafuata biblia au alifuati soma biblia nzima kwanza, pili angalia na ufuatili chanzo cha taratibu zote za ibada kama kuna sehemu kwenye biblia imeagizwa kama hakuna ujue kanisa alifuati biblia bali mapokeo na maagizo ya mtu binafsi.unamaanisha kina nani hao ambao hawafuati biblia?
kama unamaanisha Kanisa Katoliki ndo halifati biblia basi wewe ndo huijui biblila
kama nilivyokwambia ujue jua Kanisa Katoliki ndo lililo kusanya maandiko matakatifu na kupanga vitabu 73 kwenye vikae kwenye biblia
Je unajua maandiko ambayo hayajawekwa kwenye biblia yameandikwa nini ?
Kanisa Katoliki Pia lina mapokeo, haya ni mambo yalikua yanafanyika na wakristo wa mwanzo ikijumuisha pia mafundisho ambayo yalijua yanarithishwa kwa njia ya mdomo oral
vitu vingi nyie hamna na hamvijui
Kanisa Katoliki lipo complex na lina baraka zote ndo maana limeendelea kuwepo namba moja na kutawala ukristo kwa miaka 2000
au wewe mwenyewe hujiulizi unawezaje ku dominate kwa miaka elfu mbili ?
zimekuja Empire zenye nguvu ma zika pita nchi zenge nguvu zikapita
Kanisa Katoliki lipo lina Control Ukristo kwa muaka 2000 mfululizo
lina msingi imara sio wa dunia hii.
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
🤝🏾Wewe unaamini tu kuwa kuandika yesu kwa erufi kubwa ni kutoa heshima kwa yesu lakini niki kuuliza ni vipi erufi kubwa inaleta heshima huwezi kunijibu nina uwakika kwasababu wewe unauelewa mdogo sana, mtizamo wako wa kiimani ni hasi hakuna uhusiano wowote kati erufi kubwa na ndogo kuhusisha na suala la heshima so negative
Leta andiko kuwa petro ni papa wa kwanza acha porojo.Bibilia iliandikwa na nani si hao hao wakatoliki ndio waliandika
Alietafsiri bibilia toka lugha za awali kwenda kilatini si hao hao wakatoliki
Mbona unachekesha sana
Aliyeandika ni huyo huyo na vipande alivyounganisha kupata bibilia anavyo yeye mwenyewe sasa unabishana na mmiliki wa mbuzi
Mwanzo bibilia waliandika bila aya wala mistari wakatoliki hao hao
Wakaja wakatuwekea sura,aya na mistari hao hao wakatoliki
Hao hao vipande vya maandishi kabla ya kuviunganisha wanavyo pale vatikani kwenye makumbusho yao na unaruhusiwa kuviona bure kabisa
Si uende Vatican ukaone maandishi ya kigiriki na kiyunani yalikusanywa wapi na wapi na na nani
Petro ni kiongozi mkuu wa kanisa la mwanzo aliachiwa mamlaka na Yesu Kristo kanisa hilo la mwanzo limekuannw viongozi wengine wengi wapatao 260 waliofuata baada ya Petro ambao ndo viongozi wakuu wa kanisa na baada ya miaka mingi kiti hicho hicho ndo alicho nacho papa ikiwa papa francis ni kiongozi mkuu wa kanisa wa takriban 260 tangu Petro. Petro akiwa wa kwanza na aliteuliwa na Yesu KrisoLeta andiko kuwa petro ni papa wa kwanza acha porojo.
Ukristo umejengwa kutoka kwa Yesu Jesus Christ, Yesu KristoNdugu zangu Wakatoliki bado hamjajibu swali langu. Mliojaribu kujibu, mmetaja mstari ule ule wa Mt 16:18
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."
Siamini kwamba katika mstari huo au kifungu hicho Mwamba ni Petro. Siamini kwa sababu katika Maandiko yafuatayo imeelezwa wazi kuwa Mwamba ni Mungu. Haya ni Maandiko ya Agano la Kale. Wakati huo Petro alikuwa bado hajazaliwa:
Zaburi 62:6
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.
Zaburi 18:2
Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu;
Isaya 26:4
Mtumaini Mwenyezi Mungu milele, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwamba wa milele.
Maandiko hayo yanaonyesha pasina shaka kwamba Mwamba ni Mungu. Na Yesu kwakuwa ni Mungu Mwana, Yeye pia ni Mwamba. Ndio sababu katika 1 Wakorintho 10:4 Yesu ametajwa kuwa ni mwamba
"Wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo."
Biblia inasema kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa(2 Kor 13:1). Daudi, Isaya na Petro mwenyewe wamesema kwamba Mwamba ni Mungu - Mwamba ni Yesu. Kwahiyo ni dhahiri hata katika mstari ule wa Mt 16:18, mwamba ni Yesu. Kwa maana hiyo Petro hastahili kuitwa Mwamba na kwakuwa sio Mwamba, hastahili pia kuitwa Papa. Kwa mantiki hiyo, sio kweli kwamba Mtume Petro ni Papa Mtakatifu wa kwanza. Nope!
Hayo ni maoni yangu kulingana na Maandiko.
Karibuni wote mliochangia uzi huu tuendelee kujadiliana:
Lwiva Phaul Lior Eyce Chasaga Genius Man The Worst pharao Munamuge Mnywani mgen publito KimMinA Mufupi Monetary doctor mubhwe geniesama Ozone_ Mwambwaro Che mittoga JF Member Freyzem Paspii0 Madumbikaya Demi Powder Saint Ivuga Hassanjk matunduizi hahaha always done Zabron Hamis Shadow7 mdesi Msudu Kida ze great Barca Enthusiastic kitali Deinstein 01 Farolito Daudi1 Rozela Beira Boy NAMBA MOJA AJAYE NCHINI Mwami Ntale UMBEEE Vyamavingi Proved okiwira Sangamwalogesha Lupweko tungatagaga MwananchiOG Intuition Tumwesige senior Erickb52 GEBA2013 Pascal Mayalla adriz Manjagata Rabbon Rogojin The Idiot Mbaga Jr Infropreneur na wengine...
Ila naomba tusirudie kusema tuliyoyaongea. Hoja zetu za sasa tuzijenge kwenye vifungu hivyo vipya na tujibu swali hili: "Je, Mwamba anayetajwa na Daudi na Isaya ni Petro? Mbona Petro alikuwa bado hajazaliwa wakati huo?"
Unarudia pointi zile zile. Nimekuuliza: Daudi na Isaya wamesema kwamba Mwamba ni Yesu.Ukristo umejengwa kutoka kwa Yesu Jesus Christ, Yesu Kristo
wanaomuamini Kristo ndio wanaitwa wakristo
Yesu Kristo ndio alimwambia Petro
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
kabla hakukua na Ukristo Baada ya Happ Ukristo Ulizaliwa
hatakama alirejsea mwamba na sehemu yoyote ile ila hakukua na Ukristo alijenga kanisa la kikristo juu ya Petro na kumwambia
"Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
Je ukatoliki umetikisika hadi leo ? haujawai hata siku moja au kwa bahati mbaya haujawahi
kanisa lilianza kama kanisa na bila jina ni " kanisa " kama alivyosema Yesu juu ya mwamba huu nalijenga kanisa.
baada ya miaka mingi na lina julikana kama kanisa la Roma lililoenea duniani
( Roman Catholic )
ikaanzatokea mgawanyiko ndani ya kanisa kukawa na kanisa la magharibi na la mashariki, kanisa hili na Orthodox
Bado La Roma likazidi ku dominate
baada ya miaka mingi zaidi ikatokea mgawanyiko ulioanza kuleta tofauti.
( hapo ni miaka ya 1500 kumbuka kanisa likikua stable kwa miaka yote hiyo )
baada ya mgawanyiko huo tuka pata kanisa kutoka kwa padre Martin Luther
huyu alikua padre aliyeweza kuleta mgawanyiko mkubwa
( ambapo baadae alijuta na kuomba msamaha kwa kuleta mgawanyiko kwenye kanisa)
baadhi ya migawanyiko ndo ilitambulika kua mgawanyiko wa kanisa huenda ilikwepo mingi isiyo ma madhara kwa kanisa
pia baada ya muda mwingi kwenda kuna madhehebu mengine yakaibuka kutoka huko kwingine mfano kutoka Lutheran etc
ila kanisa limebaki kama shina Kanisa Takatifu Katoliki La Mitume.
Bila kujali unacho waza ni ukweli kua,
ukristo umejengwa kutokana na imani ya kumuamini Kristo.
na Kristo ndie aliyemuambia Petro maneno hayo
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni..."
Ukristo Ukaanza Rasmi, Sasa sijui unachopinga haswa ?
kama anglican au kanisa ni lolote Tofauti na Catholic ndo lililoshika msingi mtuambie ni Lipi turudi mwenye historia
Nami nasema ni Kanisa Takatifu Katoliki La Mitume ndo msingi wa Ukristo Duniani
Yesu hajajipinga kwakua yeye ni mwamba alimkabidhi mamlaka Petro.Unarudia pointi zile zile. Nimekuuliza: Daudi na Isaya wamesema kwamba Mwamba ni Yesu.
Yesu hawezi kujipinga kwa kumwita Petro Mwamba.
Soma tena Andiko hili:
Zaburi 73:26
"Hata nikikosa nguvu mwilini na rohoni, wewe, ee Mungu, u mwamba wangu.."
Halafu umekiri mwenyewe kwamba kulitokea migawanyiko. Sasa jiulize: Yesu alisema milango ya kuzimu haitalishinda. Ilikuwaje sasa migawanyiko ikatokea? Migawanyiko ni ishara ya ushindi?