Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Sijui nakushauri vibaya au lah

Lakini huyo mwanaume hakufai
Usitishwe na maneno ya watu ya kuitwa single mother kheri uwe single mother kuliko kua single married

Ondoka hapo acha aendelee kulala akiona haupo na wa kumuhudumia hamna atachagua yeye sasa afe njaa au atoke njee akatafute

Binti wanaume ni wabinafsi sana kama hujui thamani yako utayumbishwa mpaka useme hiki ni nini?

Hivi umewahi kuona mwanaume akiacha ndoto zake au mipango yake kisa mwanamke

Sisi ndio deileee tunajitilisha huruma
Na kuishia kutumika na kunyanyaswa kihisia na muda mwingine tunaacha ndoto zetu na mipango yatu kisa wanaume

Wao hata huku jukwaani kila siku wanapandishiana nyuzi kushauriana
Utasiki man to man fanya hivi

Sisi huku nyuma ya keyboard kudanganyana
Shoga angu vumilia wanaume ndivyo walivyo upuuzi tu

Usivumilie upumbavu ondoka mapema angali una nguvu za kujitafutia na kujilea mwenyewe sio unavumilia unakuja kukumbuka kuondoka umekua ajuza

Jifunze kumsoma mwanaume muongo mbinafsi na mlagai kimbia upesi usimpe hata sekunde ya kuendelea kunyonya energy yako 🙏

Narudia jifunze kusoma mtu una em date macho yako usiyatoe kwenye macho yake muangalie kama anachozongumza kinatoka ndani

Ukiwa makini na timamu Mwanaume tapeli hachukui round una mdaka
Acheni kujazana upumbavu. Hakuna mahusiano ambayo yapo perfect.
 
Sikuwahi wala sitowahi kufanya hivyo na katika vitu ambavyo siwezi kumnyima mtu ni chakula, nitakunyima pesa ila sio chakula!

Nb: ninachoandika hapa hakina uhusiano na maisha yangu dear lads.
basi irl nikiwowa binti yako, nitamwambia tuhamie nyumbani kwa mama mkwe, hapo tutakuwa tunakura na kurara kwenye makochi yako hadi yachakae chakaaaaaaaaa
 
Yaani mwanaume mzima alale ndani bila sababu za msingi kisa alitoa ka milion ka mtaji serious

Yaan haumwi wala hana kilema
Kwa sababu kapata uraibu wa kuhudumiwa ndio asinyanyuke kutafuta kazi hivi nyie wanaume kwanini mnajipa u special sana ?
Kwani kutafuta kazi mpaka mtu akazulule mitaani. Haujui kuna mitandao ya kijamii?
 
Kmmk ntawawaua! Kula mtakula ila mkatafute vya kwenu😏
nahakikisha huyo binti nimemshika akili kisawasawa, awe hakusikilizi kwa chochote utakachomwambia. na hapo ukweni hatuishii tu kura na kurara, tunaendelea kukufyatulia wajukuu wa kutosha, na wakifikia umri wa kwenda shule tunakuomba hela ya ada.
 
Sisi tunajadili hoja iliyo mezani
Kaka nikuambie sio huyu tu wa mleta mada wanaume kutohudumia familia na kutaka kulelewa limekua janga
Hayo ni matokeo ya usawa wa kijinsia mlioupigania nyie wenyewe. Mnavyotaka nanyi kujumuishwa kwenye kinyang'anyiro cha fursa za kiuchumi lazima mjue kuna kundi la wanaume watakosa nafasi, kwa sababu uchumi wetu hauwezi ku-accommodate population yote ya wanaume na wanawake. Kwahiyo lazima nanyi muanze kuona ni kawaida ku-settle na mwanaume ambae umemzidi kipato au hana kipato kabisa.
 
Aiseee. Hapa najikuta nakosa namna nzuri ya kuliweka hili, ila wanaume tunakuaga selective sana kwenye kazi. Hata mimi siwezi kua mlinzi, bora niwe tapeli.

Skia dada angu, mimi ni shuhuda wa hiyo hali. Nimewahi kuipitia, na mwanamke nilozaanae watoto wawili akatumia muda mwingi kuninyanyasa kisaikolojia badala ya kuniokoa. Ni mbaya mno hii, lakini nilipita kwenye mikono moaka sasa ni mtu mpya.

Nakusihi dada angu njia nzuri hapo ni mazungumzo tu, huyu jamaa ana mzigo ambao ameshindwa kuubeba na anakufa taratibu. Amekata tamaa ya maisha huyo, mpaka anenda kula ukweni aiseee!!!!! Yupo tayari kuuza roho yake kwa shetani, haoni thamn ya kua hai, kasahau nini maana ya uanaume,anahisi dunia imemsaliti, ndo maana anajifungia ndani asionane na dunia maana anajua haita muelewa wala kumsaidi. Hivyo ndivyo anavyo jiona.

Mimi nilikaa ndani mpaka ikafika kipindi nikitoka nikionana na watu nashindwa kuwatazama usoni, nilibadili hadi njia, nilikua napita machokoroni ili tu niwe pekeangu. DARK FASE ni nyakati ngumu kuliko zote ambazo mwanaume anaweza pitia. Hamjui tu
Eti nini 😁😁 Huwezi kuwa mlinzi? Sikia nikuambie, it's okay kuwa selective...maisha ni yako na una haki ya kuishi vile upendavyo, kusubiria kazi itakayokupa amani hata kama utaipata ukiwa na miaka 50. Lakini hali ni tofauti pale unapokuwa unategemewa hasa unapokuwa na watoto, mwanamke akiwa hawezani na mitazamo yako anaweza kwenda lakini mtoto ni jukumu lako huna pa kukwepea... kesho unayoipambania sio kwaajili yako tu bali ni kwaajili ya hao viumbe uliowaleta duniani kwa starehe zako
Ushauri wa mwisho kwa vijana kama unaona huna future inayoeleweka na huwezi kuacha uzinzi tafadhali tumia condom.
 
Nyie! Hapana sina huo uvumilivu nitawatoa hata kwa fimbo!
na unaanzia wapi kumpiga bakora mtu mzima na mindevu yake
tena nikiwa kwako ukweni nanunua na vile vi earpods,sivitoi masikioni from dawn to dusk, na muda wote nipo sebuleni na remote mkononi, ole wake niskie mtu ananiletea usumbufu. siku hiyo nitatembeza mkong'oto kuanzia mama mkwe hadi wajukuu zake.
 
Hayo ni matokeo ya usawa wa kijinsia mlioupigania nyie wenyewe. Mnavyotaka nanyi kujumuishwa kwenye kinyang'anyiro cha fursa za kiuchumi lazima mjue kuna kundi la wanaume watakosa nafasi, kwa sababu uchumi wetu hauwezi ku-accommodate population yote ya wanaume na wanawake. Kwahiyo lazima nanyi muanze kuona ni kawaida ku-settle na mwanaume ambae umemzidi kipato au hana kipato kabisa.
Kwamba wanawake kuamua kufanya kazi tunasababisha uhaba wa kazi kwa wanaume?
 
na unaanzia wapi kumpiga bakora mtu mzima na mindevu yake
tena nikiwa kwako ukweni nanunua na vile vi earpods,sivitoi masikioni from dawn to dusk, na muda wote nipo sebuleni na remote mkononi, ole wake niskie mtu ananiletea usumbufu. siku hiyo nitatembeza mkong'oto kuanzia mama mkwe hadi wajukuu zake.
Hehehe nahisi uko ndotoni kijana! Au unasimlia real life yako eeh? Yani ntakusweka ndani hutoamini!
 
Hehehe nahisi uko ndotoni kijana! Au unasimlia real life yako eeh? Yani ntakusweka ndani hutoamini!
uchungu wa mwana aujuaye mzazi
najua mwanano akikulilia hautathubutu kufanya mambo yatakayomuuza, na mimi wakati huo nahakikisha mwanao akili yake nimeikamata barabara, kila ninachomwambia anafanya. tukiona unazingua sana , namshauri tuanze kuuza vitu vya ndani kimoja baada ya kingine.
 
Hao wazazi wa zamani labda, kwangu haitakaa ikatokea! Labda sio mimi!
 
Back
Top Bottom