Jeshi la Polisi: Bado tunamsubiri Tundu Lissu na dereva wake ili kufanya uchunguzi

Kwa hiyo Lisu na dreva wake ni waharifu ambao wanatafutwa na polisi ?.

..baada ya kusikia dereva amesalimika walitaka wamkamate wambambikie kesi.

..sasa dereva hakupatikana. Na wao walishajitokeza hadharani wakiashiria kuwa dereva ni mtuhumiwa.

..kwa sasa hivi hawana namna ya kuja hadharani na kutengua kauli na hisia walizozijenga awali.

..Lissu alikuwepo Tz lakini hawakumpa wito akatoe ushahidi. Alikwenda mpaka ofisini kwa RPC Dodoma hakuhojiwa. Alikamatwa na Polisi akapelekwa Central hakuhojiwa.
 
Mungu ni Mungu tu
Risasi 30 mtu kapona
Yule aliyesema sijaribiwi [emoji777][emoji777][emoji777][emoji375][emoji375][emoji375]
 
Wanajua walichokifanya
 
Kwa kweli Tundu Lissu akisikia dereva wake naye anasubiriwa ili aje ahojiwe KAMWE Lissu hatarudi nchini isipokuwa tu kuja kwenye mradi wa kugombea urais na kurudi uhamishoni. Anajua dereva anafahamu kila kitu na atakapoeleza yaliyokuwa nyuma ya kushambuliwa kwake kutakuwepo kuadhirika kwa wengi. Kumbuka pale Dodoma baada ya shambulizi dereva alisema kuwa wakati anaona watu wanamfuata alimweleza boss wake lakini Lissu alimwambia hakuna wasiwasi waendelee tu. Cha ajabu kule Ubeljiji dereva huyohuyo alihojiwa na waandishi wa DW TV akabadili kauli na kusema wakati gari inamfuata hakumtaarifu boss wake kwa sababu alijua usalama upo alikokuwa akielekea. Dereva bado yuko mafunzoni kuelimishwa aeleze nini akihojiwa na polisi wa TZ. Inaelekea hatokaa afaulu hilo soma na kamwe hatarudi na Lissu.
 
Bado mnapoteza muda kumjadili huyo jamaa,
Huyo kurudi harudi na siasa zake mwisho ni Youtube.
Kashanogewa na maisha ya kulelewa huko.
Arudi kuja kuendelea kuyaongoza manyumbu ya nini.
 
Nacomment nafuta, nacomment nafuta.
Polisi acheni u..........
 

Sirro alitangazia ulimwengu kuna gari iliyoungua Morogoro ukihusishwa na tukio! Imeishia wapi

Polisi hawaelezi kwanini siku hiyo walinzi waliondolewa, na kwanini Camera ziliondolewa

Huu utetezi wa kumtafuta dereva ni wa kipuuzi unalidhalilisha jeshi la Polisi

Kwavile hawajui na hawawezi kufanya uchunguzi kwanini wasiite wachunguzi wa nje ?

Scotland yard walikuja BoT ilipoungua. FBI walikuja kuonyesha nyumba ilipotengenezwa bomu lililolipua ubalozi 1998. Hili la Lissu lina tatizo gani tukijua Polisi wetu hawana uwezo ?
 
Kupigwa upigwe wewe alafu kuhojiwa unataka wakahojiwe wengine ??

Yani aliyekuwa anakuendesha unamficha mazima kabisaaa alafu nyumbu wanaona hili ni sawa?

.
Gari wakilolitumia kushambulia wameliteketeza kupoteza ushahidi, pia huyo dereva watammaliza kupoteza ushahidi vile vile, kulindwa ni lazima mpaka muda muafaka
 
Apeleke nini?
Ndugu, huyu Kulwa Jilala kwa uandishi wake tu na namna anavyojenga hoja zake unaweza kuelewa moja kwa moja kuwa hili ni toto tu la form One lililoshindwa shule...!

I am sure, this guy has nothing upstairs zaidi kuwa labda huandika akiwa amekula pombe na bhangi zake za AR maana ni crystal clear that, hafikirii kwa makini kabla ya kumwaga ujinga wake kwanza....
 

..hiki ulichoandika ni UONGO.

..kama dereva ametoroka basi Polisi wa Tz waripoti kwa INTERPOL ili dereva huyo akamatwe na kurejeshwa Tz.

..Kwasababu Polisi wa Tz hawajachukua hatua hizo maana yake ni kwamba hawamhitaji dereva wa Lissu.
 
ukishakua polis wa chama hapa tz automatically unakua mbumbumbu, unaongea kama huna akili, kwahio wangekufa uchunguz usingefanyika
 
Kati ya Lisu na dereva wake kutoa maelezo yao polisi na wewe kuandika bandiko refu namna hii ipi ni kazi ngumu zaidi?
Lissu anatoa maelezo gani? Hakuondoa walinzi wala Camera. TL alisikia tu risasi zikiingia mwilini, aeleze nini

Sirro aeleze ile Nissani nyeupe iliyoungua Morogoro imefikia wapi?

Sirro atoe maelezo camera zilikwenda wapi? kwanini walinzi waliondolewa

Kwanini isiwe mwendazake, si unakumbuka alisema nini saa 5 na nini kilitokea baadaye

Jeshi la Polisi, kuliko kutoa utetezi wa dereva likae kimya, linajidhalilisha sana
 
Hili jeshi tukisema tunaonekana tunadharau
 
Yani apigwe Lisu alafu maelezo atoe Sirro ? Una akili kweli wewe
TL si alikuwa anavuja damu, atasema nini.

Sirro alisimama na kusema haya
Gari imekamatwa Morogoro ikihusishwa na tukio. Sasa atoe maelezogari hilo limeishia wapi
Sirro alisema Camera zipo, aeleze zipo wapi
Sirro anajua walinzi wa eneo wanafanyaje kazi, aeleze siku hiyo walikuwa wapi

Saa 5 kuna mtu alitoa agizo masaa 2 TL anashindiliwa mirisasi.
Na dereva wa Lisu aliyeowaona kwa nini asitoe maelezo?

Au Sirro ndiyo alikuwa dereva wa Lisu?
Huna hoja, risasa zinarindima dereva aliwaona wapi.
Camera zipo wapi ili kusaidia uchunguzi

Katika nchi zilizoendelea Sirro na JPM wangeitwa kutoa maelezo!
 
Alikuwepo nchini 2020 na akafanya mikutano Lukuki na hao hao askari wakieeka ulinzi dhidhi yake! Ilikuwaje wasimkamate wakamhoji.
Hii ni kichekesho hatari.! Acheni kuwadanganya watu kuwa mnafanya kazi kiuadilifu!!
 
Tulishasema pia aje pamoja na dereva wake ili tupate maelezo yao kwani yatatusaidia kusonga mbele katika uchunguzi wetu,”amesema Misime.
Kwa majibu haya ni wazi kwamba polisi ya nchi iko hovyo sana.

Mafunzo yao yamejikita ktk kubambikizia watu kesi na kula rushwa tu.

Mambo ya kitaalamu haiyawezi.
 
“......Huu ni mwaka wa tano kuishi nje sio jambo dogo, kufanya maandalizi kunahitaji muda na fedha pia, Rais aliahidi kunilipa fedha za matibabu lakini hazijalipwa hadi leo licha ya kusema niandike madai yangu,” amesema Lissu
Huyu jamaa si aliutangazia umma wa dunia kwamba tayari serikali ya Tanzania imemplipe madai yake yote, mbona anakanusha tena?

Alifikiri urafiki waliokuwa wanaufanya na ahadi hewa zingetokea kirahisi tu kwa utashi wao?

Kuna siku wanaomdhihaki JPM ambaye hayupo kujitetea kutokana na yote anayozushiwa watatamani dunia ipasuke iwameze maana haki ndipo itakapo dhihirika kwa vitendo dhidi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…