Jiji la Mwanza vs Jiji la Arusha: Lipi ni zaidi kwenye hili?


KIA haipo Arusha kwa mji kama mji. Hesabu uwanja wenu wa Arusha ambao wa Mwanza ambao upo under construction ukikamilika sidhani kama Arusha itafika hiyo level

Usafiri wa reli vipi ??.. na kampuni za usafirishaji ambazo zinahudumia zaidi lake zone ??...


Media industry unaiongelea star tv tu, vipi kuhusu rfa upande wa Radio. Usisahau kuna Jembe fm ma Lake fm ambazo zina uwezo wa kuandaa festivals kubwa na kuleta wasanii hadi kutoka Nigeria. What about Arusha ??...
 
Sahara imejifia
Akina mwoleka wanalia njaa
 
Nigeria ina GDP kubwa kuliko South Africa, nchi ipi kati ya hizi mbili ina uchumi bora? Au ipo bora kiuchumi?

Kwa miji ambayo inakatwa kodi sawa (under the same tax regime) unafikiri kwanini mji mmoja uwe unachangia kodi mara mbili ya mji mwingine?

Jibu ni kwamba, economic vibrancy, hela inatembea mno Arusha kulinganisha na Mwanza. Jiji la Mwanza hsalizalishi hela kama Jiji la Arusha. Jiji la mwanza ni sawa na Kariakoo tu kwa revenue.

Nitafutie quarter ambapo Mwanza ilitoa mapato makubwa kuliko Arusha na hutopata kwa sababu haijawahi kutokea.
Kwa hiyo, kujibu swali la mtoa mada, Arusha is by far more economically vibrant than Mwanza.
 
sahara media imejifia,ukishakuwa tawi la ccm kama channel ten sijui nanai atakusikiliza..Sijasema kia ipo arusha ila inasevu arusha zaidi kuliko kwingineko.
Huo uwanja wa mwanza hata ukikamilika wengi wa watu huko hawana pesa za kupanda ndege tofauti na Arusha iliyojaa watalii na wageni wa kila aina.Ishu ya reli ni suala la mda tuu na huku reli ya sgr itataoka tanga arusha hadi musoma ko is not a big deal ..
 
Lol...Dg em kalale aisee
 
Hauna akili wewe
 
Arusha kuna redio kadhaa pia,Sunrise,Triple A,arusha one fm,sauti ya injili,radio safina,kuna sauti ya wakulima(ors)tanzanite radio na nyingine nimezisahau!! Ila tv station hakuna aisee,kwa arusha kila kitu kitu kipo under one roof!!ndiyo maana wana arusha huwaambii kitu na arusha yao, na wanajua ku spend kiukweli,kijana wa arusha ukimpa laki saa moja jioni,ukaja kumuuliza saa moja kesho yake asubuhi ana ngapi,utakuwa unamuonea bure!! Kama ana nyingi ni 10,000/ mwanza unaweza ukampa mtu sh 10,000,baada ya wiki ukamkuta badi ana chenji sh 6,000/ huwa nayatamani maisha ya mwanza niyaishi arusha ila nimeshindwa kabisa.
 
Lol...Dg em kalale aisee
Huo ndiyo ukweli, ukiondoa misaada na mikopo, hivyo vituo vya afya na hela wanazolipwa walimu, kodi kutoka Arusha ni miongoni mwa vyanzo vikuu.
Data ndiyo hizo.
 
Mkuu kwenye makusanyo ya kodi kwenye jiji la Mwanza wanachokifanya kwenye uwasilishaji huwa wanatenganisha kati ya Ilemela na Nyamagana ndo maana maana unaona kama Mwanza haikusanyi kodi nyingi ila waki-combine inakuwa nyingi zaidi wakati kwa Arusha ni eneo moja, refer Waziri Jaffo ripoti yake
Angalia revenue ndo itakuokupa picha halisi, Arusha ina watu wachache Zaid ya mwanza Ila Ina shughuli nyingi za kibiashara kuliko mwanza, ndo maana imeipita mwanza kwenye revenue
 
What a comment comrade! Umemaliza chief
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…