Mwanza ni mji mkubwa mno kuucompare na Arusha, zote zina manispaa mbili japo Arusha bado hata manispaa yake ya pili haijafikia hadhi kamili,
Mwanza unaonekana kama mji uliopooza kwa sababu ya kutokuwa na shughuli nyingi za utalii kama Arusha hivyo ukiwa mwanza usitegemee sana kupata huduma nyingi za starehe kama mahoteli ya kitalii, clubs, biashara ya vinyago na pombe,tour companies,kumbi kubwa za mikutano, na makao ya jumuiya mbalimbali.
Ila tofauti na hili la utalii ambalo Arusha inaongoza baada ya kuhodhi biashara ya utalii kutoka katika mikoa jirani mfano sehemu kubwa ya mbuga ya Serengeti ipo Mara lakini Mara haitambuliki wala haifaidiki, sawa na mapato na faida za kitalii za hifadhi ya mlima Kilimanjaro n.k
Hakuna kingine Arusha kama jiji unaweza kulicompare na Mwanza jiji ukianzia ukubwa wa mji yaani idadi ya makazi na watu, viwanda, shughuli mbalimbali za uchumi na biashara.
ubora wa makazi huwezi kukuta mwanza mjini mitaa kama ungalimited, sinoni, sombetini, matejoo nakadhalika ambapo kuna nyumba nyingi duni ambazo ni mchanganyiko wa mabanda ya tope, miti na mabati wanaishimo binadamu na ukiingia deep uswahilini ng'ombe wana mazizi mjini,
gharama za maisha mwanza ziko chini ukikompare na Arusha chumba cha tope uswahilini ni elfu 15 mpaka 30 hii kwa mwanza utakuwa kwenye chumba safi kabisa anachopaswa kuishi mwanadamu, achilia mbali hupatikanaji wa vyakula na huduma za msingi mtaani.
Posh areas (mitaa ya kidosi) hapa Arusha inaongoza ukilinganisha na Mwanza, hivyo gap la kipato katika mji wa Arusha ni kubwa kati ya masikini na tajiri ukilinganisha na Mwanza.
Miundombinu na msingi bado mwanza inaongoza katika hili, kwa maana ya stendi bora za magari, mtandao wa barabara za mitaani, urahisi wa usafiri mfano uwepo wa costa nyingi, hiace na tax unlike Arusha ni hiace tu ndo nyingi wakati mwingine pia nauli hazitabiriki hasa jioni na ukiwa mjini lazima uzitafute zilipojirundika kama zizini kule kilombero stendi ya vumbi na ukiwa mgeni ni changamoto kubwa.
Mwanza ina hospitali kubwa ya rufaa ya bugando, kiwanja kikubwa cha ndege siyo airstrip, chuo kikuu kikubwa cha SAUT, Mall kubwa tz, usambazaji mkubwa wa huduma ya maji safi mjini, usafiri wa majini na biashara ya minofu ya samaki nje ya nchi, masoko mazuri n.k
City center(CBD) kati ya mwanza na Arusha kiufupi Arusha inachapwa mbali katika wingi wa idadi ya majengo ya ghorofa na coverage, shughuli za kibiashara na wingi wa watu, mpangilio wa CBD kwa mwanza tiyari unaelekea pazuri uwezi kukuta mrundikano wa huduma zote sehemu moja kama vile kijijini yaani hapohapo stendi ya mabasi ya mikoani pembeni kiwanja cha mpira, stendi kuu ya daladala ya vumbi, huku soko kuu hatua kidogo soko bovu la mitumba, mara makaburi yasiyojengewa wala kuwa na uzio nayo yapo city center,achilia mbali mrundikano wa guest bubu n.k
Mandhari, kiufupi katika hili kila jiji hapa lina sifa yake nzuri tofauti na lingine, Arusha ni mlima meru, hali ya kijani kibichi, majengo marefu kadhaa mazuri, mitaa kadhaa yenye mpangilio mzuri na magheto makali/yakifahari mfano njiro. Mwanza ni ile hali ya milima na nyumba juu ya miamba, ziwa Victoria,rock city mall, hifadhi ya kisiwa cha sanane, muonekano wa jiji nyakati za usiku hasa ukiwa sehemu za mlimani au ghorofani,kijani kibichi na hali ya hewa nzuri kwa mwaka mzima hakuna joto kali sana au vumbi la poda kama Arusha.
Future ya hapo baadae kwa miji hii itakavyokuwa bado ni kitendawili kwa Arusha kuipiku Mwanza kwa hizi major project zinazoendelea ikiwemo kufufua na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa mizigo na watu ziwa Victoria hasa na Uganda pia kenya, daraja la busisi, soko la kisasa,stendi bora za kisasa, kiwanja cha kimataifa cha ndege, SGR, kuimarika kwa masoko na pato la biashara ya dhahabu, kuletwa kwa ndege za kusafirisha mizigo especially kwa ajili ya minofu ya samaki, kutambuliwa kwa kisesa kama mji na manispaa ndani ya jiji la mwanza, uwepo wa mpango wa kuwa na BRT achilia mbali ongezeko kubwa la idadi ya watu au birth rate kanda ya ziwa ukilinganisha na kaskazini n.k labda mji utakaompa mwanza challenge mbeleni ni Dodoma pekee na siyo Arusha.