Umeongea kweli kabisa mkuu Mtibeli, hicho kitabu kusema ukweli hakitasomwa na wengi na kitawahi kuchuja sana masikioni mwa watanzania kama tu ilivyokuwa kwa kitabu cha wale jamaa kina Meena na wenzake.
Suala la watanzania kumpenda Magu liko wazi sana sijajua watu wengine wanachangamana na watanzania kwa kiwango gani maana kila penye mikusanyiko ya watu huwezi kukuta Magu anasemwa kwa mabaya na mpaka kuna baadhi ya sehemu watu bado wanapiga mpunga kila wiki kwa kuweka tu mkusanyiko wa hotuba za jamaa na kuna siku maalumu ya kusikiliza na watu wanajaa ukumbini.
Magu ni rais pekee nchi hii ambaye ameonyesha uthubutu wa kusimamia rasilimali za nchi na zikaleta manufaa makubwa ndani ya muda mfupi, kwa watanzania Magu ni kielelezo cha maamuzi magumu.
Nenda mashuleni kote asilimia kubwa kunapokuwa na debate zinazohusu uzalendo mfano pekee inaotumika wa kuwaonyesha watanzania uzalendo ni jina la mwamba JPM. Na mpaka wanashauri viongozi wetu wawe wachapakazi, wathubutu na wazalendo kama Magu.
Ukiacha udhaifu mkubwa wa kuogopa challenge Magu alilitendea vyema sana taifa hili kuliko kiongozi mwingine yeyote nisijue sana kwa Nyerere ila ukipitia mitandaoni na mijadala mbalimbali Magu ni kama anakubalika kwa kiwango kikubwa sana. Na hata ikifanyika poll yoyote humu au popote bado Magu atawaacha mbali sana kina Mkwere na Samia. Kumbuka hata utafiti waliofanya gazeti la mwananchi ulitoa matokeo ya Magu kushinda japo watawala waliopo hawakuridhishwa nao ikabidi mwananchi waombe msamaha.
Magu hachafuki kwa vitabu labda itokee flyover za Dar zivunjwe zote, SGR ihujumiwe, bwawa la Nyerere lipotee mazingira ya kutatanisha, mahospitali aliyojenga tuamue kufugia kuku, stand na masoko makubwa aliyoyajenga tusiyatumie, ikulu ya chamwino tuichome moto, daraja la busisi lipigwe bomu liteketee, ukarabati mkubwa wa shule kongwe uliofanyika uharibiwe makusudi, barabara alizojenga zisipitike, ukuta wa mererani tuuvunje, watu waliowekewa umeme kwa gharama ya Tshs 27000 wahamishwe wote nchini iwekwe imani nyingine kwa wakazi wapya watakaoletwa, ndege alizonunua tuzihujumu zote na mengine mazuri mengi aliyofanya ndipo tunaweza tukamsahau huyu mtu mchapakazi ambaye hajawahi kutokea nchini mwetu.