Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Kuanza kuhoji tu undani wa hizo dini zenu inaonesha tayr akil yako imeanza kufanya kazi kutoka kwenye vifungo vya iman za kishenz ambazo zlikuja kuiharibu akili ya mtu mweusi.

Kwa wengine wa imani zenu ni kufuru kuuliza ama kuhoji maswal kama yako maana utaonekana mpagani na mtu asiyemuogopa huyo Mungu wa peponi sjui mbinguni.

Kimsingi imani na dini zote si sahihi maana ukifuatilia zote kiundan zinamakosa na zote zipo chini ya lengo moja na muanzilishi mmoja aliekuwa na targets zake kwa jamii fulani.

Kiuhalisia dini zote asili yake ni imani za kishirikina ambazo ziliabudiwa na mababu wa kiafrika ya kale yaani misri na sehem zingine baran Africa, na baada ya ujio wa races za watu weupe na kuanza kustaharabika wakazicopy hizo imani na kuzistaharabisha kwa kubadili histories, majina na wahusika wa hizo imani na ndipo ujio wa dini na misahafu ukaanzia hapo.

Uwez sema asiemuamini Allah atachomwa moto wakat hiyo dini imaenza juzi tu miaka ya 1400 iliyopita, na kabla yake kuna maelfu ya imani zilikuwepo kabla yake.

Na huwez sema asiyemuamn yesu atachomwa moto wakat kbla ya miaka 2000 kuna wakina Osiris, azazel, Krishna waliwai kuwepo kabla yake na walikuwa na miujiza kama ya huyo yesu na hawa ndio origin copies za stories za jesus ambao nao asili yao ni miungu ya waafrika wa kale.

Hakuna ukwel ktk dini ndiomaana mnapingana ninyi kwa ninyi.

Ni bora usiamin dini na miungu yake, kulko kuwa mpumbavu usiyejua nini unachokiabudu na kuipa sifa jamii fulani iliyokuletea uo upuuzi.

Mungu yupo lkn si huyo mnaemuabdu ktk magenge yenu ya dini.

Muumba wa kweli hana haja na dini ili umjue, bali kufuata sheria za uumbaji, upendo kwa viumbe wake na kutii sheria za , jamii yako unayokuzunguka.

Mbingu na motoni hazipo na hazitowai kuwepo maana ziliundwa na hao wana dini ili kuwatisha watu na kuwafanya waoga na watumwa wa imani.

Mtakesha kusubiri ujio wa hivyo viumbe vyenu na havitorudiii maana havijawai kuwepo.

Kupinga mafundisho ya dini isiwe kigezo cha kumuita mtu mpagani, maana hata wew unakuwa mpagani kwa kuikana imani ya uafrica na kukumbatia imani za mtu mweupe ambazo ni uongo na copy ya ile origin ya imani za babu zako.
View attachment 2201191
Kama ni kweli usemavyo kuwa Afrika ilipoteza asili yake kwa kuacha kuabudu Mungu wa asili yao na kuabudu imani za watu wengine nanidhahiri kuwa ndicho chanzo cha mkanganyiko na matokeo ya maisha yetu ya leo kiimani na kifizikia.

Je kuna haja gani ya kuchimbua makaburi ya nyuma na kuanza kuitaabisha jamii ambayo tiyari imeshajengwa kwa kipindi kirefu katika ustaarabu fulani wa kiimani kubadili imani yake ambayo sote tunajua faida zake mpaka sasa katika jamii hizo husika hata kama tunajua imani hizo hazina ukweli ama zina mapungufu kadhaa?

Je, tutakapofata huo uafrika na dini ya kikwetu tutanufaika na nini cha tofauti na tulichokuwa tukikipata huku kwenye uislamu na ukristo?

Je, si kweli kuwa tunaenda kuanzisha mkanganyiko mpya wa Mungu wa Afrika na utitiri wa makanisa na imani nyingine tena duniani nakuzidi kuwa na uwalakini na uwepo wa Mungu?

Je, waafrika kuirudia asili yetu na Mungu wetu unahisi ndiyo muarobaini wa kumaliza mkanganyiko wa kidini na uwepo wa Mungu wa ukweli katika imani zote tulizoaminishwa?
 
Unaona ndugu, huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na ninajaribu sana kujiepusha na mjadala ambao hautakuwa na tija ili nisije kuharibu funga yangu kwani uzoefu nilionao juu ya watu waongo na wazushi wa aina hii ni kutumia lugha chafu pindi watakapozidiwa na hoja.

Kwanza Kumwita mtu jina lisilokuwa lake hiyo ni kama tusi, sisi ni Waisilamu wa Ahmadiyya, tunajiita hivyo na tunajulikana hivyo na tungependa tujulikane hivyo, jina jingine la kupewa na wapinzani wa Jumuiya ya Ahmadiyya ni katika njia ile ile ya kuthibitisha midomo michafu ya wapinzani hao dhidi yetu.

Uongo mwingine ni huu; kwamba Swala yetu ni kinyume na jinsi wanavyoswali Waislamu wengine na hilo anadai linapatikana katika vitabu vyetu na magazeti yetu, sasa mwambie kama yeye ni mkweli aonyesha kitabu chetu cha Swala au gazeti letu ambamo tunaweza kupata ushahidi wa hicho anachosema ----kwani njia ya muongo ni fupi.

Ipo hivi; jumuiyya ya Waislamu wa Ahmadiyya ni jumuiyya inayokua kwa kasi kubwa DUNIANI kuliko Jumuiyya za DINI ZOTE, hilo ni jambo linalowapa khofu kubwa sana Wapinzani wa Jumuiya ya Ahmadiyya licha ya upinzani wao wameshindwa kuzuia maendeleo ya hii jumuiya wamebaki kutukana, kulalama na macho, povu na mashipa ya shingo inawatoka hawajui cha kufanya.
 
Mwenyezi Mungu ni mmoja, kwanza tuelewane jina lake ni nani?

Kama tunakubaliana Mwenyezi Mungu ni mmoja basi hatuna budi kukubaliana pia kuwa Dini ni moja. Haiwezekani Mwenyezi Mungu mmoja awe na dini nyingi kwa maagizo tofauti tofauti.

Binafsi Nnaamini Mwenyezi Mungu ni mmoja na Dini ni moja tu, nayo ni Uislam. Dini na madhehebu yake mengine yote ni mambo ya tamaa za kibinaadam za wagawe uwatawale (Divide and rule).

Tokea mwanzo mpaka mwisho umemaliza vizuri sana kasoro pale tu "Dini ni moja tu, nayo ni uislam" hii inadhihirisha ni namna gani bado hauko tiyari kufikia muafaka wa jambo hili. Labda nikupe maoni yangu binafsi ni kuwa hili upate suluhu katika hili nilazima ujikane kwanza(uvae viatu vya wengine) na kama ukishindwa kufanya hivyo FaizaFoxy basi kubaliana na walioleta confusion hiyo na dogma inayowataabisha sasa kuwa walitumia akili kubwa mno na mtaendelea kuifuata milele mpaka siku mtakapoamua isiwe hivyo kwa sababu ndiyo lilikuwa kusudio lao katika kuifanya iimarike na iwe na ushindani sokoni kwa kipindi cha muda mrefu zaidi.
 
Makadiani wanapingana na Qur'aan na mafundisho ya Mtume,
Unachofanya ndugu kisai ni kuweka madai tu ilhali kila mtu anaweza kuwa na madai yake.

Kama ambavyo watu wanasema salafi wanaingiza watu motoni hayo ni madai kama yalivyo madai yako.

Kuthibitisha madai hayo inatakiwa watu walete ushahidi wapi salafi wanaingiza watu motoni.

Na wewe kuthibitisha madai yako unatakiwa uweke ushahidi wapi kadiani amempinga mtume na KUipinga qurani ?

Unaweza kuweka aya moja au hadithi moja kuonesha ambapo kadiani wamempinga mtume ili kufanya madai yako yawe na maana.
 
Hii ni namna ambayo wewe binafsi umeamua kuitafsiri dini

Kuna member anaitwa ROBERT HERIEL huyu anakuambia ukristo ni upendo, kwa maana hiyo hata wewe hapo ni mkristo endapo una upendo wa jambo lolote
Mkuu huu uzi waliufuta ?

Nakumbuka ulinitag kule ila sikuuona tena..
 
Unachofanya ndugu kisai ni kuweka madai tu ilhali kila mtu anaweza kuwa na madai yake.

Kama ambavyo watu wanasema salafi wanaingiza watu motoni hayo ni madai kama yalivyo madai yako.

Kuthibitisha madai hayo inatakiwa watu walete ushahidi wapi salafi wanaingiza watu motoni.

Na wewe kuthibitisha madai yako unatakiwa uweke ushahidi wapi kadiani amempinga mtume na KUipinga qurani ?

Unaweza kuweka aya moja au hadithi moja kuonesha ambapo kadiani wamempinga mtume ili kufanya madai yako yawe na maana.
Huyu jamaa kwa sheria zake na namna ambavyo anatafsiri uislam anaweza kujikuta JF nzima muislam ni yeye peke yake
 
Unaona ndugu, huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani na ninajaribu sana kujiepusha na mjadala ambao hautakuwa na tija ili nisije kuharibu funga yangu kwani uzoefu nilionao juu ya watu waongo na wazushi wa aina hii ni kutumia lugha chafu pindi watakapozidiwa na hoja.

Kwanza Kumwita mtu jina lisilokuwa lake hiyo ni kama tusi, sisi ni Waisilamu wa Ahmadiyya, tunajiita hivyo na tunajulikana hivyo na tungependa tujulikane hivyo, jina jingine la kupewa na wapinzani wa Jumuiya ya Ahmadiyya ni katika njia ile ile ya kuthibitisha midomo michafu ya wapinzani hao dhidi yetu.

Uongo mwingine ni huu; kwamba Swala yetu ni kinyume na jinsi wanavyoswali Waislamu wengine na hilo anadai linapatikana katika vitabu vyetu na magazeti yetu, sasa mwambie kama yeye ni mkweli aonyesha kitabu chetu cha Swala au gazeti letu ambamo tunaweza kupata ushahidi wa hicho anachosema ----kwani njia ya muongo ni fupi.

Ipo hivi; jumuiyya ya Waislamu wa Ahmadiyya ni jumuiyya inayokua kwa kasi kubwa DUNIANI kuliko Jumuiyya za DINI ZOTE, hilo ni jambo linalowapa khofu kubwa sana Wapinzani wa Jumuiya ya Ahmadiyya licha ya upinzani wao wameshindwa kuzuia maendeleo ya hii jumuiya wamebaki kutukana, kulalama na macho, povu na mashipa ya shingo inawatoka hawajui cha kufanya.
At least angejitahidi kuwa politely kwenye hoja ange sound vyema, kutumia maneno machafu kutetea visafi ni confusion
 
uliamishiwa jukwaa la dini kwani hauna access ya jukwaa la dini?

Mara nyingi nyuzi zikipelekwa kule ndio huwa mwisho wake kwasababu wengi haana access
Unafanyaje kuingia huko..
 
At least angejitahidi kuwa politely kwenye hoja ange sound vyema, kutumia maneno machafu kutetea visafi ni confusion

Sifa zote mbili za ukali na upole zinafaa isipokuwa tu lazima ujue ni mahali gani, wakati gani na kwa nani upole au ukali unafaa.--- unaangalia historia na uzoefu ili kujua mtu huyu anahitaji politeness or rudeness na njia zote hizo zinaweza kumrekebisha mtu.

Allah ni mpole, mkarimu, mrehemevu nk, lakini kuna kipindi inapobidi anakuwa mkali sana wa kuadhibu na mwenye hasira na mbora wa kufanya hila kwa wafanyao hila.
 
Tokea mwanzo mpaka mwisho umemaliza vizuri sana kasoro pale tu "Dini ni moja tu, nayo ni uislam" hii inadhihirisha ni namna gani bado hauko tiyari kufikia muafaka wa jambo hili. Labda nikupe maoni yangu binafsi ni kuwa hili upate suluhu katika hili nilazima ujikane kwanza(uvae viatu vya wengine) na kama ukishindwa kufanya hivyo FaizaFoxy basi kubaliana na walioleta confusion hiyo na dogma inayowataabisha sasa kuwa walitumia akili kubwa mno na mtaendelea kuifuata milele mpaka siku mtakapoamua isiwe hivyo kwa sababu ndiyo lilikuwa kusudio lao katika kuifanya iimarike na iwe na ushindani sokoni kwa kipindi cha muda mrefu zaidi.
Huo ndio ukweli, ikiwa tu unaelewa maana ya neno "dini".
 
Thibitisha haya maneno yako uliyobwabwaja hapa.

Mk 12:29-31 SUV​

Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
 
Unaiamini biblia?
 
Sifahamu zaidi ya kujua kuwa ni dini
Maana ya Neno Uislamu Kilugha

Kilugha, Uislamu unamaanisha kujisalimisha, kunyenyekea na kutii. Dini hii ndio inaitwa Uislamu kwa sababu ni dini yenye msingi wa kusalimu amri za Allah na kuzitii.

Maana Yake Kiistilahi

Ni njia ya maisha, mfumo wenye misingi ya imani na matendo ya kuwafanya watu wapate furaha kamili duniani na ahera, iliyotumwa na Allah na kufikishiwa watu kupitia kwa mitume. Uislamu ni sheria ya kiungu inayowaongoza watu wenye akili kuelekea mambo mazuri kulingana na hiari zao.

Yaliyomo katika Uislamu

Maana ya Uislamu ni kujisalimisha: kujisalimsha kwenye amri na makatazo ya Allah. Uislamu hautakuwepo bila ya kujisalimisha kwenye hukumu za Allah. (Angalia al-An'am, 162 na an-Nisa, 65) Mwanadamu ni mja aliyeumbwa na Allah.

Kwa kuwa Allah amekizingira kila kitu kwa elimu Yake na kwa kuwa Yeye ana hekima, sharti la utumwa ni kujisalimisha Kwake. Sheria za uhai humshurutisha mwanadamu kujisalimisha kwa Allah kwa sababu Allah ndiye anayezijua zaidi sheria hizo na anamjua zaidi mwanadamu.

Ulimwengu na kila kilichomo ndani mwake hutii sheria za Muumbaji huyo. Kwa hivyo, dini ya ulimwengu wote ni Uislamu. Jua, mwezi na nyota, vyote hivyo vinafuata Uislamu. Kwa kuwa Uislamu unamaanisha kumtii Allah na kujisalimisha Kwake, tunaona kwamba viumbe vyote hivyo vinamtii Allah bila ya kuasi. Yaani, tunashuhudia kwamba vinajisalimisha na kwamba vyote vinafuata Uislamu.

“Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumtii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?" (Aal-i Imran, 3/83)

Soma zaidi: Uislamu ni nini? Unaweza kutoa maelezo ya kina kuhusu Uislamu? | Maswali juu ya Uislamu
 
Back
Top Bottom