Rais wa Rwanda Paul Kagame amemuonya Rais Cyril Ramaphosa akisema Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepotosha mazungumzo yao ya Faragha waliofanya na kusema kama Afrika Kusini inataka makabiliano basi Rwanda iko tayari kujibu.
Katika waraka wake mzito alioandika kwenye Mtandao wake wa X, Rais Kagame amesema alifanya mazungumzo mawili wiki hii na mapema jana na Rais Ramaphosa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC, akisema kuwa kile kilichosemwa na maafisa wa Afrika Kusini na Rais Ramaphosa mwenyewe kuhusu mazungumzo yao kwenye vyombo vya habari kimejaa upotoshaji mwingi.
Rais Kagame amesema ikiwa maneno yanaweza kubadilika kiasi hicho kutoka kwenye mazungumzo hadi kwenye tamko la umma, inasema mengi kuhusu jinsi masuala haya muhimu yanavyoshughulikiwa.
Rais Kagame amesema ikiwa Afrika Kusini inataka kuchangia suluhisho la amani huko Mashariki mwa DRC hilo ni jambo jema, lakini haina nafasi ya kuchukua jukumu la mpatanishi au msuluhishi. Na iwapo Afrika Kusini itataka makabiliano, Rwanda iko tayari kujibu hilo.
#KitengeUpdates
View attachment 3218375
Sent from my TECNO KG5j using
JamiiForums mobile app