... bila unafiki, kwa nia njema kabisa kutoka mioyoni mwenu, tupeni tafsri ya mashairi hayo hapo chini; wimbo wa Diamond huo! "Wapinzani piga risasi", halafu wapinzani wam-support! How? Shida tumejawa unafiki, hayo mashairi yamejaa uchafu mwingi.
Kwa nchi inayojali usawa huo wimbo haukutakiwa kuruhusiwa ila kwa kuwa ni kwa faida ya "chama chetu, tena tuna jeshi", watafanya nini? Of course, hawana cha kufanya, ila hata chuki? Kutwa kucha mnapandikiza chuki wenyewe na huyo mtu wenu ambaye leo anaomba support ya kila mtu ili "ashinde"!
Magufuli baba lao, Makonda baba lao...
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!