Kampeni dhidi ya Diamond Platnumz: Wanaharakati kuweni serious kidogo
Wasanii wanaojitambua duniani hawafanyu ujinga unaofanywa na wasanii wetu hapa Tz, wengi hujiweka mbali na siasa ili kuepuka kuwavuruga fans wao wanaoweza kuwa na itikadi tofauti.

Hawa wetu walizubaa akili zao muda mrefu sana sasa ndio wanaamshwa, next stop kwa wale wajinga bongo movie kina Steve Nyerere, Wema, Uwoya, na wenzao, hakuna kununua movie zao.
Ulishawahi kununua au una-burn CD tu?
Mikwara tu hamna lolote. Wateja wa hizi movies ni watu flani hivi uswahilini wala hawafahamu hizi vita zenu, movie zinanunuliwa Kama kawa.
 
Shida ni yeye kuamua kujiunga na watesi wa jamii ya Tanzania,ilhali msanii anajiita kama ni kioo
cha jamii.Kwa hilo tuu amepoteza uhalali wa kuendelea kusimamia imani hiyo.Zaidi tutamwita msimamia au mpigania maslahi yake binafsi huku akiihitaji jamii kupata mafanikio yake binafsi.
Kwahiyo na Harmonize, Zuchu mmewasusia? Vipi na wasanii wengine Kama wote walioshiriki campaign za CCM?
 
Ahhh.. Kumbe!..

Sasa mbona ccm haifi kwa presha za chadema?
Wanapindua meza kila uchaguzi jiwe kwenye uchaguzi wa 2020 alikiri wabunge wasijisifu kujipeleka wenyewe bungeni ila wamepelekwa Mungu akafanya yake.
 
... cheki mashairi yake objectively utabaki mdomo wazi! "Wapinzani piga risasi"!

Magufuli baba lao, Makonda baba lao...
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!
Ulitaka amuimbe mwenyekiti wa UDP...

Nikiangalia objectively naona ametumia metaphor just like any musician
 
Vipi hawa "Wapuuzi" wasipo puuzwa Mondi amejipangaje kwa mengine yajayo?
Kibinadamu kuwa na mbadala ni muhimu.
Mshaurini na hilo pia
Watashindwa inshalah.

Ila ikitokea asikate tamaa, achukulie kama ajali tu aendeleze ubunifu wa kazi zake abaki Msanii kinara Africa Mashariki.
 
Mkuu hayo ni maoni yako na yanaheshimiwa. JPM kama asingekuwa jasiri asingefanya mengi huko mikoani.

SGR isingefika ilipofika, ndege zisingenunuliwa, lile jengo la kupokea wageni airport lisingemalizika kwa wakati.

JPM alikuwa jasiri na marais wengine wa afrika waliuona uthubutu wake ndio maana alipoenda Ethiopia wakawa wanamzunguka.

Hiyo habari ya yeye kuwa mrundi ni hadithi za kitoto za humu jukwaani sehemu iliyojaa CHADEMA na wengi waliobaniwa mianya yao ya kutajirikia maofisini.

Uhuru wa habari uwe na faida kwa kila upande, huwezi kupewa uhuru halafu ukawa siku zote unaihujumu nchi yako. Wakati wa vita ya ugaidi kule MKIRU mtu anafanyia kazi wageni yaani anaihujumu nchi aliyozaliwa!. JPM hakutaka kabisa huo ujinga.

Ameshalala na hataamka, lakini naamini aliwagusa watu wengi, asingeweza kuuvuta umati ule pale uwanja wa ndege siku jeneza lake lilipoenda Zanzibar kama kweli alikuwa na roho mbaya.
Wewe ndiyo mmoja kati ya wanaofanya Watanzania wengi waitwe wapumbavu. Yaani maiti imewekwa uwanjani, na Serikali imesema ni mapumziko, kwa nini unashangaa watu wanakwenda kuaga?
Ubora wa mtu haupimwi na watu waliokwenda kuaga kwa kuwa Afrika hata wachawi na wezi huwa tunakwenda kuwaaga.
Watu mtaani kwenda kuaga maiti ya marehemu ni mila za Kiafrika. Hapa Dar hata Marehemu Stephen Kanumba naye alifunga mtaa kwenye msiba wake.

Hata Ruge Mutahaba naye alifunga nyomi
 
Chadema na watu wake ni wagonjwa wa akili isipokuwa Mbowe anajitambua kidogo
 
Shalom from Jerusalem,

Awali ya yote napenda niweke wazi kuwa sikumpenda kabisa Magufuli kutokana na ukatili wake ambao uliumiza wengi Tanzania. Lakini ukweli usiopingika ni kwamba ukatili wa Magufuli waafrika wengi nje ya Tanzania na hata ndani ya nchi hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kiufupi kulikuwa na kitu kama brainwashing iliyowafanya wengi kutokuona maovu ya rais huyo dikteta.

Nimepata wakati mgumu sana kuwaaminisha watu (waafrika wa nchi nyingine mbali na Tanzania) kuwa Magufuli hakufaa na kwamba alikuwa muuaji, alikandamiza wapinzani, alibambikiza kesi wapinzani na uovu unaofanana na huo.

Hivyo kujitokeza kwa wanaharakati wakiongozwa na Maria Sarungi wanaotaka BET imwondoe Diamond eti kwa sababu alimuunga mkono Magufuli , "kipenzi cha waafrika", kunaweza kusieleweke kwa waafrika wengi ambao ndiyo hasa wapiga kura kwenye tuzo za 2021 za BET.

Wala siyo siri weusi wengi huku ugaibuni wanamwona Magufuli alikuwa shujaa na ni ngumu sana kuwaaminisha vinginevyo.

Jambo baya zaidi wanalolifanya akina Maria ni kumpinga Diamond lakini wakati huo huo na kwa nguvu isiyo na mfano kumuunga mkono Burna Boy. BET inaweza isiwaelewe na inaweza kuona kuwa wanatumika.

Imani yangu ni kwamba hata ikiwa Diamond atashindwa basi siyo kwa sababu ya akina Maria bali ni ushindani wa kawaida kabisa wa mziki.

ANGALIZO: KUPENDWA KWA HAYATI MAGUFULI TANZANIA NA AFRIKA HAKUMAANISHI KWAMBA ALIKUWA NI KIONGOZI MZURI LA HASHA, BALI NI UJINGA WA WATU KUTOKUTAMBUA YALIYOKUWA YANAENDELEA NYUMA YA PAZIA. KWA WAELEWA WA MAMBO MAGUFULI HAKUWA KIONGOZI MZURI HATA KIDOGO.

Alimbambikizia kesi Nani. Nguvu ya Rais wa Tz. Anahitaji kuzunguka kufanya jambo. Ukatili gani amefanya. Mana nyie mnasisitiza haki ya asili ya kujitetea. Ushahidi nk.
 
Leo umekiri kwa kinywa chako kuwa Mwendazake alikuwa katili ? Mtakiri sana lakini hafufuki jamani kashaenda Bora mtafute kazi zingine za kufanya mataga .
 
Wewe ndiyo mmoja kati ya wanaofanya Watanzania wengi waitwe wapumbavu. Yaani maiti imewekwa uwanjani, na Serikali imesema ni mapumziko, kwa nini unashangaa watu wanakwenda kuaga?
Ubora wa mtu haupimwi na watu waliokwenda kuaga kwa kuwa Afrika hata wachawi na wezi huwa tunakwenda kuwaaga.
Watu mtaani kwenda kuaga maiti ya marehemu ni mila za Kiafrika. Hapa Dar hata Marehemu Stephen Kanumba naye alifunga mtaa kwenye msiba wake.

Hata Ruge Mutahaba naye alifunga nyomi
JPM alikuwa kiongozi shupavu huko mtaani walimuelewa sana.

Hata wewe unaweza kuwa na hiyo sifa ya upumbavu. Hapo ni Nigeria wenye akili timamu na wenye kujua kupima mioyo ya viongozi wanamuongelea.
 

Attachments

  • 228EC3FF-C6A2-4090-A5C4-E4324B04EF18.MP4
    10.7 MB
Waafrica wapi wewe lofa? Umelalia kifua cha mumeo hapo ndio akakudanganya hivyo? Mpuuzi kweli kweli!!!
Alimbambikizia kesi Nani. Nguvu ya Rais wa Tz. Anahitaji kuzunguka kufanya jambo. Ukatili gani amefanya. Mana nyie mnasisitiza haki ya asili ya kujitetea. Ushahidi nk.
Wew kama sio Sabaya basi ni Libashite na naongea kwa Staili ile ya Mkuu wa wilaya ya Iringa kuwa Tuliza mat...wewee. Magufuli ni muharifu tuu kama genge lake alilo unda la Sabaya na Makonda alistahili muda huu kuwa huko aliko Sabaya ila Mungu akaona kwa Ukatili na mauaji aliyo yafanya ni vema Amfyekelee mbali yeye mwenyewe kuliko kusubili mahakama za dunia.
Yaani huwa kila niamkapo asubuhi namshukuru Mungu kwa kuondoa utopolo huu uchwara
 
Watashindwa inshalah.

Ila ikitokea asikate tamaa, achukulie kama ajali tu aendeleze ubunifu wa kazi zake abaki Msanii kinara Africa Mashariki.
Malipo ni hapa duniani,yaani huyu kijana katoka kumdhalilisha baba yake hapa majuzi wakisaidiana na mama,machozi ya mtu hua hayapotei bure
 
Yuko sahihi kwa asilimia nyingi, hata mimi hitimisho langu kutokana na majadiliano na watu wengi nje ya nchi yetu wengi wanaamini dikteta mwendazake alikuwa kiongozi safi na mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine barani Afrika.
Nilikuwa nikijaribu sana kuwaelimisha kinachoendelea lakini nadhani alifanikiwa sana katika kuhadaa watu wengi(mataifa mengi) na hata raia(blacks) wa nchi za Ulaya na Amerika ya Kaskazini wanaofuatilia siasa za Afrika walimuona kama shujaa dikteta mwendazake.

..hilo siyo jambo la kushangaza.

..hata kati yetu Watz kuna watu wanaomhusudu Robert Mugabe, lakini ukikutana na Wazimbabwe watakupa story nyingine kabisa.
 
ndugu zanguni hiyo kitu wanamfanyia diamond imebackfire ndo imempaisha zaidi, this guy is way tooo fucking influencial🤣🤣🤣🤣🤣 hata mm sikua na mzuka wa kumpigia kura (sio kwa chuki binafsi lakini, mda tu. napenda kazi zake ) ila daa he's all over the place yaani inabidi tu mwisho wa siku umpigie kura
 

licha ya ukatili wake,​

Just a moment...! Mpaka hapo unakiri kuwa mwendazake alikuwa mkatili, au siyo? Kwamba vitendo anavyotuhumiwa navyo ni kweli! Hivyo na waliomuunga mkono kwa namna fulani ni wahusika.

Afrika ilimpenda Magufuli,​

What...? Je na waliofanyiwa ukatili nao walimpenda? Kwamba pamoja na ukatili wake, Waafrika walimpenda! Kwa hiyo ukatili Afrika ni moja katika sifa inayokubalika katika uongozi au siyo?

mtaangukia pua vita yenu dhidi ya Diamond​

My God...! Yaani kitakachowafanya waangukie pua ni kule kupinga na kulaani ukatili na kukataa kuwaunga mkono wanaofumbia macho vitendo vya kikatili? Masikini Afrika!
 
Back
Top Bottom