Kanisa Katoliki Ujerumani kuanza kubariki ndoa za jinsia moja kuanzia 2026

Kanisa Katoliki Ujerumani kuanza kubariki ndoa za jinsia moja kuanzia 2026

Ni lazima kama waafrica tuwe na misimamo yetu katika ngazi za familia ili kulinda tamaduni zetu...Hii hata waseme linaweza lisiwe na athari kibaya ni kundi linajikuta ni wazungu .

Movement zote sijui feminism ni uzungu tu basi hamna jinsi hata elimu tunategemea kutoka kwamba ... Mbaya sana kwa vile muingiliano ni mkubwa na tunakosa ushawishi kabisa tulichobaki kufauta watu wa nje.

Maisha yetu ni jadi kabisa nchi zetu ombaomba katima mambo kama haya hazina usemi kabisa .
Umasikini mbaya sana...

Na huyu mama yetu anategemea mikopo ya hao hao mashoga ili kuendesha nchi...

Najua hakubaliani na hili lakini mpaka leo kimya maana anafikiria akiwa kama mama, akinyimwa hiyo mikopo atalisha nini wanae (wanaokula kulingana na urefu wa kamba zao) ambao hata mishahara tu wanategemea mikopo?

Tumezingirwa!
 
Tujitafakari sana na hizi denu zetu

Inawezekana uwepo wa MUNGU hauhusiani na DINI yapo mambo ya kuzingatia ili kupinga immorals kama hii same sex marriage. ikiwa sasa DINI ina propel huo ufuska what esle can we rely on kupinga ufuska ??
 
Sawa..! Lakini nyie huwa mkiingia kwenye 18 za Muumba huwa ndo wa kwanza kulia na huku mkiomba watu wawaombea kwa Mungu aidha kwa ugonjwa au shida yoyote, lakini hapa ni wepesi kukanusha.
Mungu hajawai kuweka dini.....dini ni binadamu kaanzisha
 
Hizi imani inabidi turudi kwenye imani za mababu zetu za kuabudu milima,miti mikubwa na mizimu,huku tuelekeapo si kuzuri kwa kweli.
Kusema kwamba turudi kwenye imani za mababu zetu siyo sahihi..

Hebu nikuulize swali...
Mmiliki wa Kampuni ya Google anaunga mkono mapenzi ya Jinsia moja,

Pia mmiliki wa Facebook naye kadhalika.... Je umeacha kutumia hiyo mitandao kwa maana wamiliki wake wanaunga mkono Ushoga?
 
Jambo gumu ni kwamba still upande dhaifu bado watu wanatengana kabisa.

Unakumbuka Makonda alipopigwa ban kisa hizo ishu baada ya kuanza kufuatilia wanaojihusisha na kusema atadili..Basi hapa bongo wapo walikuwa wanamkandia
Dunia inakwenda kupasuka vipande viwili.

Waabudu shetani vs waabudu Mungu.

Dini zote, za waislamu na Wakristo zinarnda kubanwa kupitisha USHETANI,

Wanaosali catholicesa wakiamini wanamwabudu Mungu wakati viongozi wanahalalisha USHETANI wanajidanganya .

Wajitenge na DINI zilizochafuliwa.
 
Ukatoliki unatiwa doa na watu wa juu wenye mamlaka jambo ambalo lina wafedhehesha waumini wake wenye misimamo mikali dhidi ya uchafu huu
Wazikimbie, Shetani ameshasimama madhabahuni.

Yesu hakuwahi kuanzisha Dini yoyote.
 
Huku ndio Ulaya wamefikia na wanataka kutulaximisha..

Afrika ikatae na ijitenge na huu upuuzi hata kama Papa wa Vatican yeye anasema Iko sawa.

Mbona Papa alikwishatoa msimamo wa Kanisa kuwa mashoga wavumiliwe, wasibaguliwe au kutengwa, lakini ushoga ni dhambi, na Kanisa halituruhusu ndoa za jinsia moja kwa sababu ni kinyume cha mpango wa Mungu.

EUROPE

German Catholic Bishops Back Blessing of Gay Relationships, Defying Pope Francis

Germany’s Catholic bishops voted to adopt formal ceremonies for the blessing of same-sex relationships, defying the Vatican and testing church unity on what has become one of the most contentious issues in contemporary Christianity: moral teaching on homosexuality..

The resolution is a bold rejection of the Vatican’s position, expressed in a 2021 decree approved by Pope Francis, which prohibited the blessing of gay couples on the grounds that God “cannot bless sin.”

Pope Francis and other church leaders have warned the German synod not to stray too far from the rest of the church.
 
Ushoga mnaeneza bila kujua Kwa njia kama hizi.
Tunavyozidi kujadili ndipo upepo wake unavyozidi kusambaa, Kwa mtazamo wangu sioni sababu ya kupost mada kama hizi maana hapa mnazidi kupromoti Tu
Ni kweli unachosema,
Mfano Kule kenya Mmoja alimuua Mwenzake kwa Wivu wa kijinga sasa vyombo vingi vya habari hapa kwetu vilikimbilia kutangaza kwa nguvu kubwa sana wengine mara tatu kwa siku na picha zao wanaweka kabisa..na kutoa update kila kinachoendelea kumtafuta mhusika, bila kujua kwamba ndio wanawapa umaarufu kwa kujua au kitokujua...
 
Kusema kwamba turudi kwenye imani za mababu zetu siyo sahihi..

Hebu nikuulize swali...
Mmiliki wa Kampuni ya Google anaunga mkono mapenzi ya Jinsia moja,

Pia mmiliki wa Facebook naye kadhalika.... Je umeacha kutumia hiyo mitandao kwa maana wamiliki wake wanaunga mkono Ushoga?
Kutumia Google au Facebook haimanishi kwamba naunga hayo mambo,sababu ni bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine kwani kutumia Google au Fb hakudhalilisho utu au heshima ya mtu mwengine. Ila hili wanalo introduce kwenye maswala la kiroho ambalo kwenye biblia tunayo isimamia washasema wanaoshiriki vitendo hivyo hawato uona ufalme wa mbingu, haikusema watakaotumia Fb au Google.

Sasa ikiwa tunaenda kinyume na Bible imani yetu itakuwa haina maana ,sababu muongozo wa imani ya Kikristo unatoka kwenye biblia.
 
DINI UJERUMANI

Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujerumani warudisha baraka kwa wapenzi wa jinsia moja

03/10/2023 Machi 10, 2023

Wajumbe wa mkutano wa sinodi kuhusu mageuzi ya Kanisa Katoliki walipitisha karatasi ya kuruhusu sherehe za baraka kwa wapenzi wa jinsia moja kuanzia 2026.



Bunge la Sinodi — ambalo linalenga kuleta mageuzi katika Kanisa— lilipitisha karatasi mjini Frankfurt mnamo Ijumaa ili kuruhusu watu wa jinsia moja mahusiano yao yabarikiwe na Kanisa Katoliki la Ujerumani kuanzia 2026.

Kati ya wajumbe 202 wa Bunge la Sinodi, 176 walipiga kura ya kuunga mkono karatasi hiyo, huku 14 wakipinga na 12 hawakupiga kura.

Mchakato wa mageuzi ya Njia ya Sinodi

Kuruhusu sherehe za baraka kwa wapenzi wa jinsia moja imekuwa miongoni mwa mahitaji muhimu katika mchakato wa mageuzi ya Njia ya Sinodi, ambayo imekuwa ikiendelea tangu 2019.

Harakati inayoendelea pia inalenga kukomesha useja kwa makasisi na kuona wanawake wakiwekwa wakfu kama mashemasi.

Kulingana na shirika la habari la Katholiki la Ujerumani KNA, baraka pia zingeruhusiwa kwa waliooa au kuolewa tena kwa njia ya kiserikali na waliotaliki.

KNA iliripoti kwamba kulikuwa na pendekezo kwamba Baraza la Maaskofu wa Ujerumani na Halmashauri Kuu ya Wakatoliki wa Ujerumani "kuunda na kuanzisha sherehe zinazofaa za kiliturujia kwa wakati ufaao."

Miaka mitatu ya mabadiliko hayo itatumika kuendeleza muundo wa kiliturujia wa sherehe kwa kushirikisha
maaskofu.

Kanisa Katoliki na mageuzi


Vuguvugu la mageuzi la Vatican na Ujerumani

Kanisa nchini Ujerumani limezindua vuguvugu la kuleta mabadiliko huku kukiwa na rekodi ya Wajerumani wanaoacha makutaniko na kashfa za unyanyasaji wa kingono zinazohusisha kanisa. Uanachama wa kanisa ulipungua chini 50% kwa mara ya kwanza mnamo 2021.

Vatikani hapo awali iliweka wazi kwamba inaona miito ya Njia ya Sinodi ya kushughulikia ushoga, useja na wanawake Kanisani kama yenye kuleta migawanyiko, na kuonya simu hizo zinaweza kusababisha kuvunjika.

Mnamo Julai mwaka jana, Kanisa takatifu lilionya wanamageuzi wa Ujerumani kwamba hawana mamlaka ya kuwafundisha maaskofu juu ya mambo ya maadili au mafundisho.

Askofu wa Eichstätt, Gregor Maria Hanke, alionya juu ya hatari ya mpasuko kutokea ndani ya Kanisa kuhusu suala hilo, kama inavyoonekana ndani ya Kanisa la Anglikana
 
Back
Top Bottom