Kanisa Katoliki Ujerumani kuanza kubariki ndoa za jinsia moja kuanzia 2026

Hizi imani inabidi turudi kwenye imani za mababu zetu za kuabudu milima,miti mikubwa na mizimu,huku tuelekeapo si kuzuri kwa kweli.
Usisingizie imani. Usi-generalize. Sema huu UKRISTO.

Tatizo ni kuwa UKRISTO unaongozwa na mawazo ya watu tu. Ndio maana unakuta wachungaji:-

wanawalisha waumini wao majani, wanaambiwa wanywe jiki nao wanakunywa, wanawake wa kikristo wanawaheshimu na kuwanyenyekea wachungaji kuliko wanavyowaheshimu waume zao, waumini wanachapwa viboko eti ni njia ya kumtoa shetani, Waumini wapo tayari kulala njaa na kutosomesha watoto ili tu pesa wampe mchungaji.

Angalia wafuasi wa Mwamposa, Zumaridi, Geodevi, Kakobe, Mzee wa Upako etc. Ni kama misukule vile

Msisingizie imani, sema UKRISTO
 
Nasisitiza, hujawahi kuwaza kuhusu source ya taarifa kuwa ni ya kuaminika au la?
Okay, Kwani hata Kenge mpaka atoke damu ndo anajua kuwa sasa ameumia.

Hali hiyo ikifikia ndo utajua yanayoendelea huko Ulaya kuhusu Ushoga na baadhi ya Makanisa.
 
Ukristo unaongozwa na mawazo ya watu HOW?

Mimi ninavyojua imani ya kikristo inaongozwa na biblia, kama umetaka kuongozwa na mtu ni uvivu wako mwenyewe wa kutosoma biblia na kuielewa ila ukiielewa huwezi kuendeshwa na mtu yoyote.
 
Mleta mada inabidi upimwe akili.The Church will NEVER EVER do such a thing.Haipo na haitokaa kutokea, nyie endeleeni na conspiracy theories zenu zilizoanza tangu karne ya kwanza lakini mpaka sasa Kanisa limebaki vilevile.
 
Kanisa Katoliki ni moja, Maaskofu hao wamefanya vitu ambavyo hawana mamlaka navyo. Automatically walipaswa kusimamishwa huduma na kuteuliwa wengine.

Kanisa la Ujerumani baada ya ule uasi waliouchochea wa Martin Luther naona wanakuja na mpango mwingine wa kujitoa kuwa sehemu ya Kanisa Katoliki.

Dhehebu jipya litazaliwa soon alafu karne nyingi zijazo wafuasi wake watalishwa uongo juu ya Kanisa Katoliki na kulichukia bila kujua chanzo cha kuanzishwa dhehebu lao.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Ukristo unaongozwa na mawazo ya watu HOW?

Mimi ninavyojua imani ya kikristo inaongozwa na biblia, kama umetaka kuongozwa na mtu ni uvivu wako mwenyewe wa kutosoma biblia na kuielewa ila ukiielewa huwezi kuendeshwa na mtu yoyote.
Mifano ya namna ambavyo UKRISTO unaongozwa na mawazo ya watu nimekupa hapo. Ndio maana unakuta mtu anakwambia nafunga siku Saba kavu au siku 3 kavu, ulimuuliza hiyo ibada umeitoa wapi..anakosa jibu. Sasa hivi tupo Kwaresma, watu wamefunga ila haijulikani wamefunga nini. Mwingine anakwambia kafunga soda. Mwingine anakwambia anafunga kama waislamu. Mwingine anakwambia anafunga hadi saa sita mchana. Mwingine anakwambia anafunga siku 3 hali kabisa then anafungua siku 3 na kisha anafunga siku 3 na kuendelea Kwa system hiyo. Ni vurugu mechi tu
 
Sijajua iman yako? (Natamani ni ijue na sito reply comments yako nyingine bila kuijua imani inawezekana hata ninacho kiandika hukijui)

Maana inawezekana biblia unasoma kama hadithi za Juma na Uledi,Biblia haija andikwa straight kama vitabu vingine may be vya imani yako unayo iamini.

Hatuwezi kufunga kama alivyo funga Yesu siku 40 bila kula,hamna huyo binadamu mwenye uwezo huo. Kikristo Kwaresma maana naye kimatendo ni kipindi cha kukumbushana kwamba binadamu hapa unapita njia so tubu jiweke karibu na Mungu, mbili ni kipindi cha kujinyima kama ulikuwa unatumia elfu 10 kwa mwezi na ukajinyima ukawa unatumia elfu 5 na 5 ukatoa kwa wasio jiweza,hapo tunahesabu ni kama umefunga,ila hii ni kwa wasio na uwezo wa kufunga na kipindi cha kusali sana ili toba yako ikubalike mbele za Mungu.

Ila kwa kuwa hatuna uwezo kama wa Yesu,Kwaresma tunafunga ila tunatakiwa kula mara moja tu ndani ya masaa 24,ile fedha ya milo mingine tunatakiwa tusaidie wasio jiweza.

Ila wapo wenaofunga hata siku tatu bila kula cha msingi kile ulicho jinyima usaidie wasiojiweza.

Kwa kifupi Kwaresma ni kipindi cha kutubu, kusali sana,kufanya matendo ya huruma kwa wanao hitaji kwa kile unacho jinyima ni sawa na mwana mpotevu anaye tafuta mwanzo mpya au kuzaliwa upya ktk ulimwengu wa kiroho.

Na kufunga sio lazima iwe kipindi cha Kwaresma, hata kama ukiwa na maombi yako binafsi au changamoto zako binafsi unaweza ukafunga,ukasali na kutenda matendo ya huruma kwa kile unacho jinyima.

NB:NATAMANI NIJUE IMANI YAKO.
 
Mifano ya namna ambavyo UKRISTO unaongozwa na mawazo ya watu nimekupa hapo. Ndio maana unakuta mtu anakwambia nafunga siku Saba kavu au siku 3 kavu, ulimuuliza hiyo ibada umeitoa wapi..anakosa jibu.
Daniel 10:3 Sikula chakula cha fahari, sikugusa nyama wala divai, na sikujipaka mafuta kwa muda wa majuma hayo yote matatu.

Esta 4:16 “Nenda ukawakusanye pamoja Wayahudi wote waliopo mjini Susa. Fungeni, msile wala msinywe kwa siku tatu, usiku na mchana, ...
 
Ukristo sio dini ya Mungu ila ni dini ya wazungu waliinzisha na kuisambaza Kwa maslahi wenyewe na ndio maana hakuna muisrael mkristo
Umenena vyema,

Waisraeli wengi ni Judaism Wakristo ni Wachache.

Ukristo ni IMANI ktk YESU, Si dini kama wengi wanavyodhani, unaweza kuwa ndani ya uislamu na ikawa unamwamini Yesu.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Mmm!
 
Romee ndo mwanzilishi wa ukatoliki na uislamu, soon mtawekwa kibano msipate pa Kutokea.

Jitengeni na DINI zilizoanzishwa na WANADAMU.

Yesu haishi Kanisani au HEKALUNI, anabisha HODI ndani ya moyo wa mtu, ukifungua anaingia na kukaa.

ANGALIZO;

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen.
 
Moderator uzi kam huu ambao hauna credible source ni wakufuta
 
Yesu alipokuwa anasulubiwa pazia la hekalu lilipasuka unajua maana yake hatufungwi tena na mapokeo ya dini
Kanisa ni mtu na sio majengo na siku ya mwisho atakaye hukumiwa ni individual na sio jengo la kanisa
 
Yesu alipokuwa anasulubiwa pazia la hekalu lilipasuka unajua maana yake hatufungwi tena na mapokeo ya dini
Kanisa ni mtu na sio majengo na siku ya mwisho atakaye hukumiwa ni individual na sio jengo la kanisa
Amen.

Hata Walio ktk uislamu Wanamhitaji YESU Kwa IMANI, Si ktk DINI.

Maana YESU ndiye Mungu anayekuja kuwahukumu WANADAMU wote wenye mwili.
 
Anatakiwa atoke hadharani AKEMEE,

La Sivyo..........
 
Hamna jeuri hiyo, mnazipenda dini zenu kuliko chochote kile, mtakuwa tayari kuwa mashoga kuliko kuziacha dini zenu.
Hizi imani inabidi turudi kwenye imani za mababu zetu za kuabudu milima,miti mikubwa na mizimu,huku tuelekeapo si kuzuri kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…