Sasa swali langu linakuja. Wewe income yako ni kama GSM? Mimi nimetoka kwetu napata kila kitu, nikaanza kazi nijihudumie,
Umekuja kunioa ukasema niache kazi nilee watoto , nyumbani unaniachia elfu moja ya dagaa wanangu wale, wewe unaenda kukesha bar, kwakuwa mama yako hakusoma, baba yako alikupeleka shule ya kata unataka na wanangu wasome kata kwakuwa wewe huna uwezo, nakaa nyumbani nafubaa kama mzee wa miaka 60 kisa mume wangu hataki nifanye kazi nibaki nilee watoto,
Ukirudi nyumbani unanikuta nimefubaa huvutiwi tena na mimi ulienioa miaka 7 nyuma nilipokua najinunulia lotion ya 35,000. Saizi unanipakisha minara coconut oil. Unaenda kazini kwako unakutana na secretary anapaka lotion ya 20,000 anapendeza anawaka unamtamani unakaa ukimwambia mke wangu hana mvuto tena. Wanaume mna utindio si eti?
Nani aliwadanganya kuwa kupinga 50/50 ni lazima mwanamke abaki nyumbani? Personally huo ujinga wa 50/50 siutaki kwangu hata sukari ikiisha sinunui bila mahesabu. Nilishamtengenezea Mr kwamba mimi ni support yako. Pale unapotoa mimi ndo ntaongeza kama kuna ulazima. Gharama zangu za maisha ni kubwa, hujanioa ili u shrink my standards otherwise ungeenda kuoa kijijini kwenu sitimbi huko. Na kazi nafanya na wanangu nalea. Hivi mfano kazini umefukuzwa ghafla na akiba huna tunaishije nyumbani? Mwanaume huna uwezo wa kunitunza huna unakomalia nikae nyumbani nivae madera. Are you serious? Kazi nafanya kama kawa na familia yako utaihudumia maana wewe ndo baba.
Wanaume wengi mnataka mwanamke ambae anakaa nyumbani ili umnyanyase. Au sio.
Muwe na uwezo wa kuwahudumia basi sio mke anamiaka 30 anafanana na kabibi ka miaka 65.
50/50 ni kwenye fursa kwa sababu hawa waliosoma waende wapi? Kama wanaume mngekua that smart si mngekua mnaongoza peke yenu madarasani. Ndo maana kuna vilaza na kuna wanawake wanaongoza. Acheni ubinafsi.
Most of us submissive women tuko makazini na ndoa zetu wanaume tunawaheshimu vizuri tu.
Tena wanawake acheni leo niwape siri, ukitaka kumcontrol mwanaume kuwa submissive. Yani shingo ndo inazungusha kichwa. Sitawafundisha kila kitu. Mwanaume akirudi nyumbani muoneshe heshima zote, mkiwa public mtreat kama mfalme uone kama hato fall for your desires.
Hawa wa jamii forum wengi wanachuki za bure na wanawake na kuna mahali wanashindwa kuelezea wanachotaka. Chanzo cha wanawake kutokua na heshima sio kazi walizo nazo bali ni jinsi wanaume mlivyoshindwa ku play part zenu,yani mwanaume anashinda bar, ana shinda anabet, kila akirudi hana hela, watoto wanarudishwa ada. Na mke alisoma ana kadregree akae nyumbani kisa mume atajiskia vibaya? Stupid