Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu amefanya majumuisho ya mwisho Mahakamani 23/9/2026

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu amefanya majumuisho ya mwisho Mahakamani 23/9/2026

Nje ya mada: Hivi huyu Katibu utumia mbinu gani kutotiwa nguvuni kama wenzake? Lengo, tukijua mbinu anazotumia, basi zitumike kuwalinda wenzake wasiwe wanakamatwa mara kwa mara.
Mkuu lakini records zinaonyesha Katibu Mkuu pia ameshahudhuria majumba ya dola mara kadhaa.
 
SEHEMU YA 4.

Hili ambalo nimezungumza sasa hivi halikuzungumzwa kabisa katika kesi ya Grey Kungu Matata wala Khatibu Gandi.

Katika kesi hii, Mahakama lazima ilitolee uamuzi.

Ndiyo maana nilisema, njia yoyote mtakayoichagua itaandika historia na kuweka sheria.

Utaratibu upoje watu wengine wanapokuwa wanachochewa kufanya makosa?

Ni lazima Mahakama Kuu ijadili na kutoa mwongozo.

Kwa vyovyote vile, Mahakama yenu itakuwa imetengeneza sheria.

Uzito wake si kuwa na hatia au kutokuwa na hatia kwa mtu mmoja. Hapana. Uzito wake ni kutunga sheria na kutoa mwongozo.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kuweka hizo parameters, naomba sasa nipendekeze kwenu masuala ambayo mnatakiwa myatolee uamuzi, na yote yanatokana na maelezo ya ziada na sheria.

La kwanza ni kama Mshtakiwa aliitisha mkutano wa tarehe 03 Aprili, kama inavyodaiwa.

La pili ni kama Mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari katika mkutano wa tarehe 03 Aprili 2025, kama inavyodaiwa.

La tatu: Kama Mshtakiwa alitengeneza nia kwa mtu au kikundi kuhamasisha/kuchochea mtu au kikundi kuzuia Uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kutishia Serikali.

La nne: Ni kama maneno ambayo anadaiwa/kutuhumiwa kuyaongea Mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria za Tanzania.

Na kama jibu ni ndiyo, ni kosa la uhaini?

La tano: Kama maneno yanayodaiwa kuzungumzwa na Mshtakiwa yanatengeneza matendo chini ya sheria ya uhaini.

Namba 6: Ni kama Mshtakiwa alichapisha hayo maneno katika mtandao wa Jambo TV, kama inavyodaiwa.

Namba 7: Ni kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika na maneno yanayodaiwa ya kihaini.

Namba 8: Ni kama upande wa mashtaka umedhibitisha mashtaka yao kwa mujibu wa viwango vinavyotakiwa na sheria.

Namba 9: Ni hukumu gani Mahakama ifanye baada ya kupata majibu ya masuala hayo namba 1 hadi 8 niliyoyasema hapo juu.

Waheshimiwa Majaji, katika tafakari yenu kuhusu ushahidi ambao upo katika rekodi, nawaalikeni muongozwe na kanuni kuu zifuatazo za sheria.

Ni hizi zifuatazo:

Kanuni ya kwanza: Sheria zinazotoa adhabu zinatakiwa kutafsiriwa kwa umakini mkubwa.

Kanuni za kutafsiri jinai haziwezi kufanana na kanuni za kutafsiri madai, na zinatafsiriwa kwa upendeleo wa Mshtakiwa.

Hii inapatikana katika kesi maarufu ya Regs Vs Mwanangomeni, ukurasa wa 134 na 135.

Pili, Amin S/o Mrisho Vs Republic, 1971.

Tatu, Issa Hassan Uki Vs Republic, Criminal Appeal Number 129 of 2017, Mtwara, ukurasa wa 23.

Hizo zote, Waheshimiwa Majaji, zina-support kwamba sheria za jinai zinatakiwa kutafsiriwa kwa faida ya Mshtakiwa.

Kanuni ya pili: Haya yanayoitwa makosa, ukiambiwa umefanya makosa, umefanya matendo yanayokatazwa na sheria, na kama hayajakatazwa na sheria siyo kosa.

Msingi wa kanuni hii upo kwenye Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mtu hawezi kuadhibiwa kwa kitendo ambacho siyo kosa wakati anafanya.

Pia ipo katika Section 5 of the Penal Code.

Order 1 of Paragraph 5 ya General Police Orders za mwaka 2021 inasema kwamba makosa ni yale yanayokatazwa na sheria tu.

Pia ipo katika kesi ya Bahame Sitta na Wenzake Vs Jamhuri, Criminal Appeal No. 166 of 2019, Court of Appeal at Shinyanga, tarehe 11 Novemba 2022, ukurasa wa 13 na 14.

Hizo ndiyo Principle of Legality.

Kama hakijakatazwa na sheria, siyo kosa.

Kanuni kuu ya tatu: He who alleges must prove.

Anayetoa tuhuma lazima azithibitishe.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
👍
 
Mimi sio mshirikina na Wala siamini kwenye ushirikina ila ninachokuambia usimfanyie dhihaka mtu anayeonewa itakuridia pia. Ni ushauri tu. Wenzako mpaka wanaomba msamaha na kuondoka JF Ina maana wamejutia makosa yao. Wewe una ona Raha kumdhihaki Lissu kwa kupost hiyo picha, ukiulizwa Lissu alikukosena nini huna cha kujibu.

Mtu anayetupambania tupate Sheria Bora za uchaguzi wewe unamdhihaki Tena kwa personality yake sio hata kwa hoja. Usimcheke anayedhulimiwa nakusihi sana.
Mara nyingi yanawakuta mabaya, Kama Samwel Doe wa Liberia!
 
Jam
SEHEMU YA 2

Waheshimiwa Majaji, upande wa Mashitaka ulidai kwamba mimi ndiye niliyeitisha mkutano wa watia nia wa chama changu mnamo tarehe 3 Aprili 2025, ambapo nilisema hayo maneno.

Kwa madai ya upande wa Mashitaka, mkutano huo uliitishwa na mimi.

Waheshimiwa Majaji, maelezo hayo yapo katika ukurasa wa 131 wa rekodi ya Mahakama.

Waheshimiwa Majaji, upande wa Mashitaka vilevile ulidai kwamba mimi ndiye niliyewaalika waangalizi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo.

Na waandishi wa habari ninaodaiwa kuwaalika walidaiwa kutoka katika vyombo vya habari vifuatavyo: Mwananchi Communications Ltd., Jambo TV na Clouds Media.

Hayo vilevile yapo katika ukurasa wa 131 wa rekodi ya Mahakama, Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, inadaiwa vilevile kwenye hayo maelezo ya ziada kwamba kauli hiyo niliyoitoa katika mkutano huo iliwachochea baadhi ya wananchi wa umma.

Ambao walianza kuhamasishana katika maeneo mbalimbali yaliyotajwa kama Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Dar es Salaam na Mbeya.

Na walianza kuhamasishana ili kuzuia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa kutumia nguvu (through violence).

Na baadhi yao, inadaiwa, walikamatwa na askari Polisi wakati wakitekeleza maelekezo yangu.

Waheshimiwa Majaji, hayo yapo katika ukurasa wa 132 wa rekodi ya Mahakama.

Waheshimiwa Majaji, maelezo ya ziada ya mwisho yanasema kwamba kauli hiyo niliyoitoa katika mkutano wa tarehe 3 Aprili ilikuwa ni kitendo cha uhalifu (amounted to a criminal offense).

Na matendo hayo yaliripotiwa kwa Afisa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Zonal Crime Officer).

Waheshimiwa Majaji, kuna kitu nimekisahau kwenye hayo maelezo ya ziada.

Inadaiwa kwamba hayo maneno niliyoyasema kwenye mkutano niliyachapisha mwenyewe kwenye chombo cha habari kinachoitwa Jambo TV, na yalirushwa moja kwa moja kwa umma na chombo hicho.

Waheshimiwa Majaji, taarifa iliyowasilishwa Mahakamani pamoja na maelezo ya ziada ya Mashitaka niliyoyasema ndiyo kiini cha kesi hii.

They are the centre of this case.

Na Waheshimiwa Majaji, kwa vile yapo katikati ya huu mgogoro, hoja zangu za leo na pengine kesho zinahusu taarifa hii ya ziada na ushahidi ulioletwa.

Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na tuhuma hizi na kwenye maelezo ya ziada:

“With regards to the Information, the allegations and additional particulars given at the preliminary, I have the initial comment.”

Kauli yangu ya kwanza, Waheshimiwa Majaji, sijawahi kuficha wala kukana kusema maneno niliyowahi kuyasema.

Waheshimiwa Majaji, ukiangalia ukurasa wa 97 wa rekodi ya Mahakama ya Ukabidhi Kisutu, tarehe 18 Agosti mwaka jana, niliiambia Mahakama maneno yafuatayo:

“It’s true I stated those words in an open meeting. The issue is whether those words amount to treason.”

Swala siyo nilisema au sikusema.

Swala ni je, hayo maneno yanatengeneza uhaini?

“I did not say those words just once, but I repeated them at Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Lindi and Mtwara, according to the committal records.”

Nikaendelea kusema:

Hayo maneno ya kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 hayajawahi kuwa siri.

Nikasema:

“The question is: do these words constitute treason or any other offence?”

Je, maneno haya yanatengeneza kosa la uhaini au kosa lingine la jinai?

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wangu wote, pamoja na mimi hapo kizimbani, chini ya kiapo wamesema kwamba maneno hayo yametolewa sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Haijawahi kuwa siri.

Waheshimiwa Majaji, kauli yangu ya pili ya awali ni kwamba utetezi wangu (my defence has never been that I am ashamed of what I have said).

Haijawahi kuwa utetezi wangu kwamba naona haya au aibu kusema haya maneno.

Utetezi wangu siku zote ni kwamba nilichokisema siyo uhaini.

Na siyo kosa lolote la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Jamii forum
Wametuharibia sana katika
Sitowasamehe
 
images1.jpg
 
Mkuu lakini records zinaonyesha Katibu Mkuu pia ameshahudhuria majumba ya dola mara kadhaa.
Kwa maslahi ya wengi, ukiturushia hapa nyuzi hata tatu za huyu ndugu yetu kuwekwa lupango na kukaa siku kadhaa na kisha kutoka, utasaidia sana kuondoa hii sintofahamu.
 
Ila huyu Tundu Lissu ni hazina kwa Taifa Sio tu anajitetea kwenye kesi Bali anatoa na darasa la Sheria hadi kwa majaji
Mwanzo tu jaji kauliza nani ataanza kuwasilisha,Lissu katoa muongozo kupitia kifungu😂.
Ina maana refa hakujua hichi kifungu na kuelekeza fulani aanze kwa kuzingatia utaratibu /kifungu hicho?
 
Kwa maslahi ya wengi, ukiturushia hapa nyuzi hata tatu za huyu ndugu yetu kuwekwa lupango na kukaa siku kadhaa na kisha kutoka, utasaidia sana kuondoa hii sintofahamu.
Bila ya kujali hayo unayoyajuwa wewe, kazi anayofanya inazungumza yenyewe. Kama kuna tatizo na hilo, elekeza nguvu zako huko kwanza,
Haya mengine tutakusikiliza baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom