Kigogo, ni nani huyu aliyeuandama utawala wa awamu ya tano na sasa yuko kimya...

Pia kuna mjukuu wa baharia wa Kinyasa aliyehamia upande wa pili zama za jiwe alikuwa kila siku kelele, siku hizi kawa kimya kwa kuwa sasa ni zamu ya mtu wa kwao, hata baba yake alikuwa amepotea enzi za jiwe, siku hizi kila siku yupo kwenye kila shughuli na mwanya wake.
 
Siasa za bongo zimejaa hila na kuharibiana.
 
Noma sana...

Jamaa alipambana kweli kweli na Chadema masikini, Kumbe kikulacho kipo nguoni mwake ..
 
Ngoja nikupe tips kadhaa na wewe utaweza kuendelea na mjadala.

Kwanza Kigogo ukitaka kujua ni nani [uhalisia wake baada ya cover yake kutoka]

Angalia machapisho kadhaa ya ID ya fisadi Ridhiwani ya humu utaona yanawiana na yale kwenye ile account ya Kigogo kwa sasa hiyo ID kama wewe ni mkongwe na mdadisi utakua ushaijua maana utakuta post kadhaa zimefuatana kutoka account ile na huku zipo vile vile.

Kigogo hakuwa mkosoaji wa Kikwete& Rostam maana yake alikua team Msoga , Kigogo alikia anawakosoa Bashe & Mwigulu, Bashe ambao kwa nyakati fulani walikua kinyume na mzee wa Msoga tena Bashe hata aliwahi reply tweet ya Kikwete kumkaribisha Lowassa tena CCM kwa jazba maana alikua team Lowassa hii inakupa picha kambi aliyokuwepo kigogo ilikua team Msoga.

Account ile ilichagua mtandao wenye securiry kubwa ambao hautoi taarifa za mtumiaji kirahisi kwa serikali [Twitter] wakati ule , waliweza kugundua hili kwani wakati wa Magufuli mwanzoni ilikuwepo account Facebook inajiita Tanzagiza waliizima mapema sababu Meta sera zao sio nzuri sana kulinda faragha za wateja hali iliyotoa ugumu.

Kigogo aliendesha shughuli zake kutokea UK huko ila taarifa walikua wanampa waliopo karibu hasa ikisemekana taarifa nyingi zilikua zikitoka jiwe akiwa Magogoni kuliko sehemu nyingine je pale Magogoni walifunga nini mimi na wewe hatujui, hiyo ilichangia jiwe kuharakisha safari ya kuhamia Dodoma .

Baada ya jiwe kufa kigogo alimkosoa Samuya kidogo baadae akabadili gia baada ya kusemekana mwanzo Samuya alitaka kwenda kinyume na kambi yao ila alivyorudi akawa ni mwendo wa mapambio.

Baada ya jiwe kukodi waisrael na waromania kujaribu kudeal na account hiyo walijua ilikua inatokea nchi gani kilichobaki kikawa kigumu kwao ni kupata sura yake na mtandao mzima wa taarifa hapo ugumu ukaja sura ni lazima wawasiliane na mamlaka huko alipo na Twitter haikua tayari kutoa taarifa za mteja ikabaki njia ya kuiripoti account ile hadi.ikapotea kama wiki 2 kabla ya uchaguzi ila wakatuma appeal ikatoka.

Account ya Kigogo ilikua verified /blue tick siku moja kabla ya uchaguzi baada ya appeal kukubaliwa na akaambiwa sasa ili asisumbuliwe atume picha/video/selfie na document kadhaa apewe uthibitisho hapa naongelea ile Twitter ya zamani kupata blue tick ni hadi wao wakufanyie verification ya document na uhalisia wako sio kama hii ya Elon unalipia dola kadhaa unapata blue tick.

Hivyo mtu anayebaki kumfahamu Kigogo kwa uhalisia zaidi ni wafanyakazi wa Twitter ya enzi zile na pengine wachache sana katika mtandao wao aliyekua anampasia taarifa nyeti.

Nimejaribu kuchambua kwa kiasi kidogo nilichodadisi kuhusu ile account tangu na baada ya kufa kwa Magufuli


NB:Account ile kwa sasa inaonyesha location yake sio UK tena bali Tanzania ni uhakika kazi ilishaisha na pengine walishamrudisha bongo baada ya kazi yake kuisha au account kapewa fisadi mtoto aindeshe kwa maslahi ya mtandao wao.
 

Kile kijukuu cha baharia wa Kinyasa kilimchukia jiwe kwa udini nadhani maana yaliyofanywa na jiwe na haya ya sasa ya sasa yanatisha ila yuko kimya sababu ya uzanzibari, jinsia na udini wa mtu wao.

Imagine kuna siku aliwahi kutweet eti Samia yuko "misguided" watu walipompiga spana kwamba kwanini kwa jiwe hakusema hivzo bali aliamini ni utashi akazira na kupotea mitandaoni hata ya October 29 hakuwahi kuyashikia bango kama alivyofanya enzi za jiwe, yule na Zitto nawaweka kwenye kapu moja wameelimika ila ulevi wa dini umewapitia .
 
Umeiweka vizuri...
 
Jamaa alikua anapata taarifa za mbele ya mda na ni nyeti hasaa...
alikua anapewa na mtandao wa alyeko sasa madarakani. Baadae alipoingia madarakani akawa anapata taarifa za uongo na kwasababu ana followers wengi alipoaanza kumuita Jamog wakaweka uhusiano mzuri akakatia mpunga sasa hivi ni chawa. Niliwahi kumuuliza dm kwanini sasa hivi kabadilika akanijibu kwasasa hafanyi bure analamba asali na baadae akani block
 
Dokezo kubwa linalotumiwa na wengi sasa hivi ni namna akaunti hiyo ilivyotuliza kasi au kubadili mwelekeo tangu kuingia kwa utawala wa Awamu ya Sita—jambo linalowafanya wengi waamini kuwa "dhamira kuu" ya waliokuwa nyuma ya akaunti hiyo ilikuwa ni kubadilisha upepo wa kisiasa wa kipindi kile.​
 
Na watajuta sana !
 
Kigogo alipost hilo gari la kubebea maiti na aliandika.

"Gari linakatiza mitaa ya mjini daresalam kuelekea hospitali" ni siku kadhaa hata kabl ya kifo cha magufuli kutangazwa. Zile siku mbazo watu walikuwa wakiuliza yuko wapi magufuli?


Alitumia maneno ambayo si vizuri kuyaandika hapa ila yalikuwa ya kejeli kebehi moja ya hayo maneno ni "asije kufufuka nikaabika" (sio exact words ila maneno kama hayo)

Hapo akimaanisha kuna wakat magufui alipotea ila baadae akaibuka na isije tena amesema amekufa na baadae akaonekana yuko hai.
 
Kuna wakati Kigogo alikuwa anampelekea moto mpaka mzee wa msoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…