6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
- Thread starter
- #181
Unajua zamani wazungu walikuwa wanatulisha matango pori kutokana na watu wengi duniani (haswa Afrika) kutokuwa na uwezo wa kufuatilia au kujua kinachoendelea duniani.Yani hizi vita zimefumbua macho wengi
Miaka ya 90 kushuka chini, watu wengi walikuwa hawana TV kwa ajili ya kufuatilia taarifa za habari, sim zilikuwa chache, mitandao ilikuwa haijasambaa sehemu nyingi, vyombo vya habari vilikuwa vichache na 95% vilidhibitiwa na wazungu.
Sasa leo hii TV kibao, kila mtu mwenye tv ndani na anafuatilia taarifa za habari na anaona kinachoendelea duniani, simu kibao mpaka vijijini, mitandao ndo usiseme yani kama yote na inaonesha kila unachotaka kukiona, vyombo vya habari ni vingi mno, na robo ya vyombo hivyo ni private havidhibitiwi na mzungu. Yani wanaonesha vitu live bila chenga wala kuchakachua taarifa.
Ndomaana sasa tunaanza kuona chenga ziko wapi, mchele uko wapi, na mawe yapo wapi.