Mtambachuo
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 2,919
- 5,558
Hivi mmefanya utafiti ukajua waliobaki Tanzania wako kwenye hali gani? Mbona wana kiwango hicho hicho cha umaskini na wengine zaidi? Na umefanya utafiti ukajua ni wangapi waliweza kupata mafanikio kwa kwenda huko? Na umejuaje kama hao waliorudishwa kama wangekuwa wamebaki Bongo huenda wangekuwa wamashafariki kwa magonjwa au kuuawa? BTW Tanzania kuna ushamba wa kudhani ukihamia nchi nyingine basi ni lazima mafanikio yatakuwepo.
Mkuu hivi umeshawahi kuishi nje ya inchi?Mna overrate sana maisha ya Tz. Sio kila ambae yuko Ulaya na hataki kurudi Tz ni kwasababu hawezi au anaona aibu kwasababu ya hali yake kiuchumi. Wapo wengi tu hawataki kurudi kwasababu hii ni nchi ya hovyo. Huduma za afya mbovu,elimu mbovu,siasa za kijima kuuana tu kisa mtu umeongea ukweli. Low quality of life kila kona. Mnasema ooih tafuta hela hata ukiwa na hela nchi hii bado ya hovyo tu. Late Mufuruki aliwahi kusema unaweza kuwa na cash 100m kwenyw gari ukapata ajali hapo pwani tu ukafa kwa kukosa huduma ya kwanza.
Ha ha ha. Unauliza makofi polisi? Mentality kama yako ndio niliowajibu. Tamu kwako ila kwa wengine ni nchi ya kishenzi tu hata uwe na hela. Full uholela. Mimi nimeishi nje miaka mingi dunia ya kwanza na sijaishi kwa shida hata wiki moja. Naishi Tz sasa hivi sioni chochote cha ajabu just another third world country aka sithole ila ndio kwetu.Mkuu hivi umeshawahi kuishi nje ya inchi?
Hakuna raha kama ukirudi toka nje na una hela,,
Bongo ni taamu sn AISEE,,
Ukiona ndg au rafiki yako hataki kurudi Tanzania ujuwe bado mambo magumu upande wake ,asilete visijgiziio.
Walioenda South Africa kwa kuzamia wengi wao kuanzia Dar ni vibaka wenye elimu duni. Watanzania walioenda hata nchi jirani kama Malawi na Zambia sio vibaka kama walioenda SAWatu wote ninao wafahamu walio enda nje wamefanikiwa pakubwa tena wako mbali kimaisha na uchumi.
Uso generalize hapa.
Labda mimi ndio nikufundishe kwanini hukufanikiwa hapo Greece na ukaamua kurudi bongoNimeondoka Greece mwaka 2011.nipo Africa now..
Kama utahitaji kujifunza utajifunza ,ila kama unaleta ubishi basi endelea kubishana.
Nilikuwa Greece mwaka 2010 nikiwa na mtoto 1 nimeacha Tanzania,Kwani kuwa na mke na watoto ndio maisha?
Kwani ni lazima kila mtu awe na mke na watoto?
Mkuu rejea comment yang nilisema nilishauriwa na mzee wng niondoke Greece napoteza muda.,na unajuwa hao waliokimbia Greece kwenda huko German na kwengineko ulaya kulitokea nn hapo Greece hata wakapata nafasi ya kuondoka hapo?Labda mimi ndio nikufundishe kwanini hukufanikiwa hapo Greece na ukaamua kurudi bongo
Na hili ni tatizo la wabongo wengi hasa wale wa stori za kimaskanimaskani huwa wao wanaongeleaaga Italy na Greece tu, hizo ni choka mbovu halafu hazina fursa kwa wageni labda uwe muuza unga
Wewe ulikuwa Greece miaka yote unasota ulishondwa kujua kuwa Greece ni SHENGHEN, ungehitaji kukata tiketi tu na kwenda aidha Germany au Holland, mimi nimekutana na wabongo Hollanda wameekimbia Italy na Greece huko wamejilipua kama Warundi hii ilikuwa 2006, mimi sikusimama nilipitiliza mpaka UK.
Wewe ulikuwa unafanya ni Greece miaka yote hio na unasota mpaka kuamua kurudi bongo?
Una paspoti ya Greece ?
Wazazi wa nani mkuu Elon au maana kama Elon walitengana aliamua kuishi kwa baba yake kisa alikua na Computer na yeye alikua anapenda hizo mambo akiwa bado mtoto..Hivi unajua wazazi wake walikuwa na ukwasi aina gani?
Labda Marekani ya Vingunguti mkuu..Tanzania kuna fursa za watanzania kuishi maisha mazuri kuliko hata anayeishi Marekani.
Daah pole sana Mkuu miaka hiyo mlikua hamjui kabisa Nchi za kwenda ndio uende Ugiriki kweli...Mwaka 2010 niliwahi ishi Greece kwa miezi 6..
Kipindi hicho nipo under 30 ..
Athens nilikuta watanzania wengi sn,,wenye maisha mazuri na maisha ya kutubu.
Mimi nilikuwa miongoni mwa vijana ambao walikuwa na maisha magumu sn pale Athens.
Ndipo mzee wng mmoja mtanzania akaniweka chini akanishauri.
Mwandende"wewe bado mdogo sn,,
hapa Greece hapakufai,,utapoteza muda wako bure..
Mimi nina umri wa miaka 50 now,nipo hapa tangu 1998 , najuta kuwa hapa hadi sasa,,
Sina pesa na pia sina family zaidi ya ile niliyoacha Tanzania.
Tanzania nimeacha mke na mtoto mmoja tu,,,
sipendi na wewe yakukute.. natamani kurudi nyumbani Nashindwa.
Nakushauri tafuta maisha pia tafuta na family .
watu wengi wanaoishi ulaya hawana family .
Rudi nyumbani kajipange upya,
Tafuta maisha na tafuta family pia,
Ukikosa maisha unaweza ukapata maisha mazuri kupitia watoto wako hapo baadae...ukiwa hapa hutotengeneza family,.watu wengi hapa wanaishi kisela tu.
Nilimsikiliza yule mzee na kuamua kurudi Tanzania..
Nilichojifunza kwa watanzania wengi wanaoishi Africa kusini,na baadhi ya inchi za ulaya na America kusini zenye maisha magumu.
Wengi hawana maisha na family pia hawana..
Wamekosa vyote...
Mtu yupo south miaka 30 hana mke wala mtoto na ameshakuwa mtu mzima...
Mtu una over 55 umeishi nje zaidi ya miaka 30 hata ukirudshwa Tanzania now utafanya nn?...
Huna maisha na family pia huna.
Mkuu kwenye kutafuta maisha unaweza kwenda popote kama unadhani ulaya yote ni sawa..Daah pole sana Mkuu miaka hiyo mlikua hamjui kabisa Nchi za kwenda ndio uende Ugiriki kweli...
Pole sana mkuu ni kweli unachosema ila kwa wasafiri ni vizuri unapokua haujatoka kujua kabisa zipi Nchi zenye unafuu kidogo yote kwa yote ni maisha tu ok poa...Mkuu kwenye kutafuta maisha unaweza kwenda popote kama unadhani ulaya yote ni sawa..
Mwnzo nilikuwa Turkey nilikaa kwa miezi kadhaa baadae nikakimbilia Greece ,,
nilidhani nitapata nafuu ya maisha kumbe hamna kitu.
Unajuwa mkuu mara nyingi watu wa ulaya huwa hawasemi uhalisia wa maisha ya kule.Pole sana mkuu ni kweli unachosema ila kwa wasafiri ni vizuri unapokua haujatoka kujua kabisa zipi Nchi zenye unafuu kidogo yote kwa yote ni maisha tu ok poa...
Ok sawa mkuu ila Nchi za Uturuki,Portugal,Greece yako,Spain,Hungary na hizo zilizopo huko upande wa mashariki hazipo sawa kiuchumi wengi wanafanya ni daraja tu la kwenda Nchi ambazo sijazitaja hapo zenye viwanda vingi ingawaje kwa sasa vibali ndio imekua changamoto tofauti na miaka ya nyuma..Unajuwa mkuu mara nyingi watu wa ulaya huwa hawasemi uhalisia wa maisha ya kule.
Niliuliza kuhusu turkey nikaambiwa kuna fursa ya kufanya kazi viwandani lakini ikawa ndivyo sivyo..
Nikaona nielekee Greece tena kwa njia za panya ili niingie ulaya nzr zaidi,
Kufika Greece nikaona ni rahisi kurudi Tanzania kuliko kutoka Greece kwenda inchi ingine yeyote ya ulaya.
Ndy nilipofanya maamuzi ya kurudi Tanzania na kuanza upya..
Hilo nalijuwa mkuu,,ila baada ya hapo sikupenda tena kusihi ulaya.Ok sawa mkuu ila Nchi za Uturuki,Portugal,Greece yako,Spain,Hungary na hizo zilizopo huko upande wa mashariki hazipo sawa kiuchumi wengi wanafanya ni daraja tu la kwenda Nchi ambazo sijazitaja hapo zenye viwanda vingi ingawaje kwa sasa vibali ndio imekua changamoto tofauti na miaka ya nyuma..
Twende taratibu ndugu, Schenghen Viza haiingii UK, UK wanajitegemea na UK Viza na sarafu yao Sterling pound.Labda mimi ndio nikufundishe kwanini hukufanikiwa hapo Greece na ukaamua kurudi bongo
Na hili ni tatizo la wabongo wengi hasa wale wa stori za kimaskanimaskani huwa wao wanaongeleaaga Italy na Greece tu, hizo ni choka mbovu halafu hazina fursa kwa wageni labda uwe muuza unga
Wewe ulikuwa Greece miaka yote unasota ulishondwa kujua kuwa Greece ni SHENGHEN, ungehitaji kukata tiketi tu na kwenda aidha Germany au Holland, mimi nimekutana na wabongo Hollanda wameekimbia Italy na Greece huko wamejilipua kama Warundi hii ilikuwa 2006, mimi sikusimama nilipitiliza mpaka UK.
Wewe ulikuwa unafanya ni Greece miaka yote hio na unasota mpaka kuamua kurudi bongo?
Una paspoti ya Greece ?
Zamani mtu mwenye pesa alikuwa anaitwa Giriki kabla ya Greece kufirisika.Daah pole sana Mkuu miaka hiyo mlikua hamjui kabisa Nchi za kwenda ndio uende Ugiriki kweli...
Halafu anazumgumzia ugumu wa maisha Ulaya kwa reference ya Ugiriki. Kipindi hiko ndio Ugiriki ilifilisika hadi kuchangiwa hela na EU.Daah pole sana Mkuu miaka hiyo mlikua hamjui kabisa Nchi za kwenda ndio uende Ugiriki kweli...
Sijawahi kufikiri kama pana mzala ataenda Greece kutafuta maisha hao mabaharia tu wa kutoka Greece ni roho mbaya balaa kutokana na life ya kwao sema Watanzania tunateseka kwa kutokua na taarifa ila kaenda juzi tu hapa sio miaka yetu hata simu za touch hakuna..Halafu anazumgumzia ugumu wa maisha Ulaya kwa reference ya Ugiriki. Kipindi hiko ndio Ugiriki ilifilisika hadi kuchangiwa hela na EU.
Bongo waliwaita hivyo kwa sababu wengi walikua wanatoka kupanda meli za Greece na wakirudi kutoka huko na zile dollar tunawaona ni matajiri ila Nchi yao ilikua sio nzuri kivile toka kitambo mimi nimevuruga docks nyingi Duniani maana nilipokua na Globe marine SA tulikua tunaenda kutengeneza meli walizo na mkataba nazo popote inapoleta changamoto..Zamani mtu mwenye pesa alikuwa anaitwa Giriki kabla ya Greece kufirisika.
Ila kwa sisi watu Maritime route ya Greece ni sahihi kupanda meli, Greece ndio kituo kikubwa cha kukarabati meli dry dock port of Piraeus, Attica, Greece