KISUTU: Jamhuri kuleta mashahidi 24, vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

KISUTU: Jamhuri kuleta mashahidi 24, vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

S
Mwenyekiti wa chama taifa Mhe. Freeman Mbowe amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo leo Agosti 23, 2021 kesi Na.63/2020 ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya Ugaidi ndani yake itaanza kusomwa kwa hati ya mashtaka na ushahidi kwa hatua ya awali...
Subiri sasa muone namna Lengai Ole Sabaya atakavyo achiwa kwenye kesi yake na kuwa shahidi mkuu wa Serikali kwenye kesi hii inayomkabili Mtuhumiwa wa UGAIDI, Mwenyekiti Mbowe na wenzake na hapo ndipo watu watashangaa na kumkubali Ole Sabaya kuwa utetezi wake ni wa ukweli kwenye kesi yake huko Arusha.
 
Hapo hakuna kesi .
Kula njama na kumsababishia Ole Sabaya majeruhi.
Sabaya huyu huyu aliyevamia kwa Mbowe usku usku .
Sabaya huyu huyu aliyewaumiza walinzi wa Mbowe .
RPC Kingai eti ndo shahidi aliyemwambia Mbowe mwaka huu hutoki tutakupa kesi ya ugaidi au kuna mwingine?
Ugaidi kwa kumiliki risasi 3 .
 
Hakuna eaia aliye mahakamani akaweka hata mtiririko wa mwenendo wa maswali na majibu, au leo ni kusomewa mashitaka tu na kusepa?
 
Hahaha boss anayelipwa mshahara na Mabeberu hahahah, sasa hapo sijui Mulamula ni boss au Mabeberu
Mulamula analipwa Mshahara wake na Mama Samia,na ndiyo alimpaa kazi hiyo! Sasa Mabeberu wanaingiaje hapo!?
 
Ndiyo maana TWAWEZA katika utafiti wao walisema CCM inaungwa mkono zaidi na watu wasio na akili. Huyu ni typical good example.
hahahaahahaa mtanyoooka tu mwaka huu wala hatuna haraka na nyie umizeni mioyo yenu tuuuuu
 
Mwenyekiti wa chama taifa Mhe. Freeman Mbowe amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo leo Agosti 23, 2021 kesi Na.63/2020 ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya Ugaidi ndani yake itaanza kusomwa kwa hati ya mashtaka na ushahidi kwa hatua ya awali.

UPDATE
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamesomewa maelezo ya mashtaka mbalimbali yanayowakabili ikiwemo la kutaka kudhuru viongozi wa Serikali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Upande wa mashitaka unasoma mashitaka kwa kusema kuwa; Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa, Mohamed Abdallah Ling'wenya na Mhe. Freeman Mbowe wanatuhumiwa;

1. Kula njama za kutenda ugaidi (kulipua vituo vya mafuta)

2. Kula njama na kusabisha majeraha kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya

3. Mhe. Mbowe alitoa laki 6 kwa ajili ya kufadhili matendo ya Kigaidi.

4. Watuhumiwa wote kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi.

5. Mshtakiwa wa pili anashitakiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi.

6. Mshtakiwa wa tatu anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT.)
Tafadhali rekebisha kwenye hati ya mashtaka ni Mbowe siyo Mheshimiwa Mbowe kama ulivyoripoti. Gaidi hawezi kuitwa na mahakama Mheshimiwa
 
Tafadhali rekebisha kwenye hati ya mashtaka ni Mbowe siyo Mheshimiwa Mbowe kama ulivyoripoti. Gaidi hawezi kuitwa na mahakama Mheshimiwa
Akili zako zimenenepa kama jina lako, hazina uwezo wa kufikiri
 
kwani walikuwa hawajui kuwa leo gaidi anakuja mahakamani? wameshaipuuza wameona gaidi hana cha kujitetea hapo
Hivi Mama alisema wenzake wameshahukumiwa na wanatumikia kifungo, ni nani na nani kati ya hao watatu?
 
Hivi Mama alisema wenzake wameshahukumiwa na wanatumikia kifungo, ni nani na nani kati ya hao watatu?
waliohukumiwa ni wale watatu ambao jumla walikuwa saba watatu wakahukumiwa kwa kuachiwa huru najuwa utasema hiyo siyo hukumu
 
Mbowe akishinda hii kesi itakuwa ni aibu kubwa sana na anguko kubwa la kisiasa kwa Madam SSH.

Binafsi sina chama na sipendi vurugu za kisiasa lakini naomba sana Mbowe ashinde.

Msiniulize sababu.
 
MaCCM jinsi yalivyo vyamia humu , unaona kabisa jinsi gani wanavyomuogopa Muheshimiwa Mbowe.
 
Back
Top Bottom