PreGE2025 Kongamano la Kitaifa la TLS kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hivi ni kweli hujui, au swali lako ni ulalamishi tu kwa kuwa tayari unao upande unaoushabikia?

Ngoja hata hivyo nijaribu kusaidia kama ni kweli hujui:

Kwanza ni lazima ujue hizo "hoja" zinazozungumziwa ni zipi, na kwa nini TLS na CHADEMA (na wananchi wengi siyo CHADEMA pekee) wanakuwa upande huo mmoja, dhidi ya upande wa pili (unajuwa ni upande upi huo?) serikali, na baadhi ya wananchi, huenda nawe ukawa huko)
Kwa hiyo ziainishe hizo hoja kwanza, na kama ni kweli huelewi kwa nini makundi hayo yapo hivyo; basi unahitaji kuelimishwa kwa sehemu kubwa sana.
Itakuwa ni kwamba hata HAKI zako kama mwananchi huzijui! Wewe utakuwa ni mtu ambaye yupo yupo tu, akienda msalani na kurudi, kulala, kula na hakuna la zaidi kwenye maisha yake.
Kwaiyo hapo ndo tayari umenielimisha! kama hapo ndo umenipa elimu ya kujitambua acha tu bora nisijitambue.
 
Naamini kuwa mhimili wa Mahakama pekee yake katika mazingira ya Tanzania haiwezi kuhakikisha maamuzi ya Mahakama yanazingatiwa. Hivyo umma mpana wa waTanzania pia uweke mbinyo utekelezaji kwa No Reforms No Election.
Mahakama kwa sasa ni kitengo kile kile cha serikali. Jaji Mkuu yupo hapo kuhakikisha Samia anabaki madarakani. Mahakama inaamuriwa nini ifanye/iamue na serikali; hili lipo bayana.
 
Kwaiyo hapo ndo tayari umenielimisha! kama hapo ndo umenipa elimu ya kujitambua acha tu bora nisijitambue.
Hapana. Sidai kuwa nimekupa elimu ya kujitambua, ila ,labda kukustua tu uanze kujishughulisha ili ujitambue.
Nimekupa mwongozo wapi pa kuanzia. Ni juu yako kufuatilia.
 
Kongamano kubwa la Kitaifa la TLS kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2025.


Jaji Warioba

- 2015 Kuna sababu Nyingi zilizofanya wagombea wakaenguliwa lakini zile hazikuwa na Misingi iliyoko kwenye sheria za Uchaguzi wala Katiba ya Nchi na ilileta Matatizo mengi kwenye uchaguzi wetu

- Mimi na Mzee Butiku tumeona bado kuna muda wa kufanya mazungumzo na tukafanya Uchaguzi wa Amani, Matatizo tuliyoyaona kwenye Uchaguzi wa 2019,2020 na 2024 yanaweza kurekebika. Kanuni zinaweza kubadilishwa kwa sababu hakuhitajiki bunge kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi

- Wakati wetu ukiona una kesi yenye Public Interest unatafuta mahala pakubwa ili watu washiriki, Tarehe 24 walijua ile kesi ina Public Interest na wangeweza kutafuta mahala pa kuhakikisha watu wanashiriki, Kazi ya Polisi ilikuwa ni Kushirikianashirikiana na Wananchi waliokuja kusikiliza Mwenendo wa Kesi ili kuwapanga na wakiwa wengi watafute Namna ya kuwalinda

- Mahakama nayo Imeingiliwa, Nimemwona Mwanasheria Mkuu akiongea Bungeni Pia Waziri wa Mambo ya Ndani anatoa ufafanuzi wa Uendeshaji wa Kesi kwa Mtandao, Utaratibu ni kwamba kesi ikishafika Mahakamani ni Jukumu la Mahakama kuiendesha ukianza kuiongelea ile kesi inaweza toa Pressure kwa mahakama kufanya maamuzi

Tatizo lagu kwa wazungumzaji wote, they are beating around the bush! Wanaacha kumsema mtu mmoj ambaye anaruhusu haya yote... ambaye akisema haya yakome yatakoma instantly. RAIS!
 
Back
Top Bottom