Kosa la Samia ni kuleta Siasa za Zanzibar huku Tanganyika

Mwenye akili ndogo humjua mwenzie ndo maana anakua wa kwanza kutoa lawama akihisi kazidiwa kwa udogo wa akili.

Nimeshakupa somo hutaki kuelewa kazi kutyoe magazeti makuubwa point zero.

Unahamahama mara JPM mara samia mara nchimbi hueleweki

Nani kakwambia anamtaka nchimbi,ina maana nchi nzima nchimbi ndo kiboko yako bila yeye wewe huwezi kuishiiii
 
Uwezekano wa kumficha kutomwambia ukweli upo ila sababu ya kumficha ndiyo tunaweza tusiijue.

Je ilikuwa kwa ajili ya kujipendekeza au ilikuwa kwa ajili ya kumuharibia? Zote zinaweza kuwa sababu.
 
Nimefuatilia malumbano yenu. Sijaelewa kwa nini mnalumbana. Kimsingi wote mnapinga uovu unaoendelea, mnatofautiana padogo sana ila cha kushangaza mnalumbama kama vile mmoja ni chawa wa CCM na mwingine ni Gen-Z.

Hajakosea anaposema tatizo la msingi la TZ ni mfumo ndiyo maana anasema akiondoka Samia akapachikwa mwingine, shida itakuwa pale pale na inaweza hata kuwa zaidi.

Tuwe makini na hawa wanaotuaminisha shida ni Samia au dini au Uzanzibari. Shida ni mfumo na tunaposema hivyo siyo kwamba tunamtetea Samia. Mifumo kandamizi ina tabia ya kutumia tofauti za watu za kidini, kiitikadi, rangi, nk. kuendelea kuwatawala.
 
Uwezekano wa kumficha kutomwambia ukweli upo ila sababu ya kumficha ndiyo tunaweza tusiijue.

Je ilikuwa kwa ajili ya kujipendekeza au ilikuwa kwa ajili ya kumuharibia? Zote zinaweza kuwa sababu.

Kujipendekeza naona ndio sehemu kubwa! CCM inaendeshwa kwa uchawa! Ingawa hata ndani ya CCM, Samia hapendeki, hiyo iko wazi kabisa, ndio maana alipitishwa kimagumashi na kundi la Kikwete kwa kuuvunja kabisa taratibu za CCM, kama wengelifuata taratibu zao wenyewe, Samia asingefika popote. Hivyo hata kumpa taarifa za uongo kumuharibia inawezekana kabisa.
 
Katika mazingira yale, njia ipi bora ya kujenga ukaribu na Rais? Kwa kumdanganya kitu ambacho ndani ya muda mfupi atakuja kujua ukweli tofauti na uliomwambia au kwa kwenda kinyume na wengine na kumnong'oneza, "Mheshimiwa Rais, wanakudanganya. Ukweli ni huu hapa"?

Nauliza hivi siyo kwamba nakupinga unaposema uchawa unaweza kuwa sababu kubwa. Tunajua washauri wenyewe akili zao fupi wanaoendeshwa na maslahi ya pesa na vyeo. Sidhani kama utendaji na matendo yao wanayafikiria kwa upana na weledi wa kazi zao.
 
kwann umteke mtu kisa kutoa maoni yake juu ya mwenendo wako kama kiongoz wake
 
kwann umteke mtu kisa kutoa maoni yake juu ya mwenendo wako kama kiongoz wake
Hakuna sababu ya kumteka mtu yeyote, hata mmoja.

Ndiyo maana nawashangaa wanaotaka kuweka tofauti kuwa "yule aliteka watu wasio wa kawaida, huyu anateka mpaka watu wa kawaida" kuwa wanaandika ujinga tu.

Mtu wa kawaida ni nani? Nani anastahili kutekwa na kuuawa nchi hii?

Hivi hawa watu hawaoni kuwa ukizuia kuteka tangu mwanzo, kwa hao watu wanaoitwa sio wa kawaida, ndiyo utakuwa unawalinda hata hao unaowaita wa kawaida?

Hawaoni kuwa ukiachia wasio wa kawaida watekwe tabia ya kuteka itazoeleka na kuendelea mpaka kwa hao wanaojiona ni wa kawaida?
 
Ambacho hujaelewa ni EGO tena ile ya kitanzania kali kali ndio inasababisha malumbano makali mpaka kupimana uwezo wa akili ndogo kiasi au ndogo sana.

Ndo maana wadau wanataka reforms zitakazo ukandamiza mfumo uliopo.
 
Ambacho hujaelewa ni EGO tena ile ya kitanzania kali kali ndio inasababisha malumbano makali mpaka kupimana uwezo wa akili ndogo kiasi au ndogo sana.

Ndo maana wadau wanataka reforms zitakazo ukandamiza mfumo uliopo.
Nini mtazamo wako kuhusu Magufuli na utawala wake? Naomba unijibu kwa aya zisizozidi mbili. Kuna kitu nataka kufahamu. Inawezekana nina suluhisho la malumbano yenu.
 
Pemba yenyewe haina mahusiano mazuri na Unguja.

Bila Tanganyika hata hiyo Zanzibar haitakuwepo..


Watagawana mbao, au itakuwa ni vita.
 
Aaah mkuu haya masuala yalisabbisha nikose raha kwenye somo la kiswahili kuwekewa limits.

Mtazamo wangu ni kwamba JPM alifanya makosa mengi sana na hakufata katiba. Jembe katupa maendeleo ya vitu na kuvuruga maendeleo ya watu na siasa.

Sijui nimezingatia aya mbili ama


Nini mtazamo wako kuhusu Magufuli na utawala wake? Naomba unijibu kwa aya zisizozidi mbili. Kuna kitu nataka kufahamu. Inawezekana nina suluhisho la malumbano yenu.
 
CCM mtandao w CCM mtandao walikua began kwa began na Mbowe ndiyo maana Samia alipo apishwa kua Raisi Mbowe akapoa hakawa hakosoi tena Serikali akalambishwa Asali, mfano Mbowe angekua Kiongozi wa Chadema mpaka sasa Chadema wangeshiriki uchaguzi. Ndiyo Maana Lissu alipowaambia Viongozi wa Chadema Mwaka huu Chadema haitashiriki uchagu Viongozi matapeli na mawinga wakachanganyikiwa na kuanza kukikimbia chama.
 
Pemba yenyewe haina mahusiano mazuri na Unguja.

Bila Tanganyika hata hiyo Zanzibar haitakuwepo..


Watagawana mbao, au itakuwa ni vita.
Mkuu hiyo ilikua kipindi cha miaka ya Nyuma leo hii Mwinyi kaijenga Pemba na kunamaendeleo sana, CCM walikua hawapeleki Maendeleo pemba, Kingine viongozi wa Kizanzibar hawana Akili na mipango ya kimaendelo, Serikali ya Zanzibar haina dira ya Maendeleo yani wao ni kwenda kazini na kurudi nyumbani.
 
1.Ni nani aliagiza watu wapigwe risasi na kuuawa vile?
2.Wapigaji risasi wale ni wakina nani na wapo wapi?
3.Ni kwanini uchaguzi ufanyike kwa namna OVU kwa kiwango kile?
4.Watu waliokufa wapo wapi?
5.Wataongozaje taifa la watu wasiowataka?
6.Ni nani anayeteka na kuua watanzania?
Waliotekwa wapo wapi?

Haya maswali wayatafakari na wayazingatie
 
Huyu anateka hadi walimu ambao wapo vijijini kabisa
 
Kitendo cha kumuita "jembe", kwa jicho langu la kijasusi naona una mahaba ndi ndi ndi juu yake na ndiyo maana umekwazika kwa maneno ya Kiranga kiasi cha kushindwa kukubaliana naye kwa jambo ambalo kimsingi unalikubali mwenzio alichosema.

Tuishie hapo.
 
Kikwete hakuwahi kuteka na kuua, bali aliteka na kutesa then anakuachia ukiwa hai. Magufuli kateka na kuua na kaenda mbali hata maiti hupewi kwenda kuzika.
Si ndo ujinga tunaousemea we unaona ni sahihi mtu kutekwa na anarudi hana hata kucha
 
Wewe utakuwa ulikuwa una shida binafsi na Magufuli hapo ilitakiwa kama ni wizi useme ulianza tokea awamu ya kwanza lakini wewe unachokifanya eti ulianzia kwa Magufuli
 
Tatizo la Watanzania wengi kama huyo ni ushamba.

Huyo naye ni mshamba tu.

Hawa watu washamba washamba mara nyingine mini huwa nashindwa jufanya mazungumzo nao kwa sababu we have no common ground to start a conversation.

Sasa ntu anayemsifia JPM kama jembe na kumkataa Samia mimi namuona ni mshamba asiyejitambua tu.

Haelewi mambo mengi sana mpaka nashindwa nianzie wapi.

Mtu anashindwa vioi kuelewa kuwa Magufuki na Samia wote ni mazao ya uizi wa CCM na wote wana matatizo mengi tu?

Anashindeaje kuona kuna tatizo la kinfumo la CCM, la utamaduni wetu kama Watanzania, ambalo hakiwezi kumakizwa kwa sisi kumtoa Samia tu?

Mtu mshamba na mjinga kama huyu mnaelewana vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…