Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Yanaluka Mataga ka akina Kingwangala yanajifanya yanaijua Serikali na CCM kuliko Jaji Werema, eti anapewa muda wa kutoa maoni Mangula mtu ambaye ameshakatwa moto hajia hata leo ni siku gani.
 
Ni ajabu kwa utawala wa awamu ya 5 kuja na hoja nyepesi kuwa kwa hivi sasa inajenga uchumi hivyo mchakato wa katiba mpya usubiri. Nimekuwa najiuliza kuna tatizo gani ujengaji wa uchumi ukienda sambamba na mchakato wa katiba mpya?

Je wakati katiba iliyopo inaandikwa ujengaji wa uchumi ulisimama? wakati rais mstaafu jakaya kikwete alipoanzisha mchakato wa katiba mpya mbona aliendelea na ujengaji uchumi?

Mwaka 2015 kwenye ilani ya ccm suala suala katiba mpya lilikuwepo lakini magufuli akaliambia taifa kuwa katiba mpya sio kipau mbele chake anajenga uchumi na juzi mama samia anarudia yale yale eti apewe muda wa kujenga uchumi.

Labda tuwakumbushe ili uchumi uweze kujengeka na kujilinda lazima kwanza katiba iwe imara.tanzania tuna katiba mbovu na ndio maana tunapiga hatua 2 mbele hatua 10 nyuma.

suala la kujenga uchumi sio suala la muda ni kazi endelevu ya kila siku hivyo hakuna siku tutasema tumekwisha jenga uchumi sasa tushughulikie katiba tusidanganyane.

Wakati ni huu tunataka katiba mpya
 
wananchi hatuhitaji katiba kwa sasa, tunahitaji maendeleo.
wanasiasa wanataka katiba kwa lengo la kugawana vyeo/madaraka.
hatutaki labda hadi mwaka 2040.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...
Namba 4 ndio ' executive summary' ya andiko lako. Katiba mbovu ilitumiwa na Magufuli kuvuruga uchumi.
 
Katiba ya nchi gani na muungano ni Batili? Hata yeye kuwepo hapo hastahiki kwani hakuna Muungano. Ni kiini macho cha Laanatullahi Nyerere.

La muhimu ni warudishe nchi ya Zanzibar kule UN baadaye ikatafutwe ile nchi iliyokuwa ikiitwa Tanganyika ndio baada ya kuulizwa wananchi kama wanataka kuungana au la ndio waje na mashauri ya kuandika hiyo katiba.

Vinginevyo ni kuzidi kunya juu ya vinyesi.
Duu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tofauti na mawazo ya wanasiasa wachache anavyosema, kwamba waachwe wasimamishe, uchumi, lakini ukweli ni kwamba Katiba Bora itasaidia au kupunnguza maamuzi, mabovu ya baadhi ya baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya wana taaluma wanao wateu kushika madaraka hayo bila kufuata ueledi, hivyo kuwa vibaraka wa walio wateu.

Baadhi ya miradi ya hivyo iliyopitishwa na katiba hii ni wa ukodishaji wa kiwanja cha kia, loliondo, iptl na mingeneyo, netgroup, alliance air, etc na sa, ukodishaji wa ndege, mikataba ya madini, epa , dcp, uuzwaji wa twiga, hivyo ucheleweshwaji wa Katiba Bora ni jiitihada wa baadhi ya wanasiasa kupitisha mambo yenye ubinafsi
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Sidhani kama ni yeye, wale wahafidhina wa ccm waliozuia mara ya kwanza ndio hao hao wana remote hata sasa
 
Ilishindwa sio kwa sababu ya kukosa Katiba mpya,South na Kenya kuna Katiba mpya kwani kuna jipya gani?
Kenya imepiga hatua kubwa kiuchumi.
fedha ya kenya iko juu kupita yetu.
Investors wanje wapo wengi kushinda kwetu.
haki ina patikanwa
wafanya biashara wan uhuru.
na mengineyo.
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi? Wananchi wengi, tunataka uchumi, tupate mkate wetu wa leo na kesho, mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa, sisi wananchi bora mkono uwende kinywani. Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi, hata kwa kupiga kura, kwenye maeneo yenu.
Kwani tume ya jaji Warioba ilipokusanya maoni wewe ulikuwa ughaibuni? Au umejikuta Jf kwa bahati mbaya!
 
Tunahitaji Katiba mpya pia ili cake ya Taifa kila mtu afaidi isiwe kama hiviView attachment 1844082
FB_IMG_16247422013045014.jpg
View attachment 1844083
 
Wanajidai kumuenzi hayati mwl. Nyerere lakini aliposema katiba hii in hatari halo hawapataki maana pataruhusu chaguzi huru!!
Lakini hata wakikubali katiba sasa kwabunge hili hatutokubali maana mapungufu yatarudishwa kama yalivyo ili kujihakikishia kubaki madarakani
 
Back
Top Bottom