Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Hayo ya hospitali, maji, shule, yaliimbwa toka mwaka 1961 na CCM imeshindwa kuyatimiza chini ya katiba hii ya sasa, definitely haitoweza kuyaondoa kwa miaka 60 mingine mbele chini ya katiba hiihii
Ilishindwa sio kwa sababu ya kukosa Katiba mpya,South na Kenya kuna Katiba mpya kwani kuna jipya gani?
 
Wenzenu wanateuliwa ukuu wa wilaya , nyinyi mmo tu kwenye kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu toka enzi za mwendazake mnasugua makalio tu mpaka leo pole sana mataga kuja na nyuzi za ajabuajabu .
Umepotoka rafiki. Kama ingekuwa hivyo kusingekuwa na media duniani. Maoni yana-shape utawala.
 
Baada ya Rais Samia Suluhu kuwatumia vijana wasio na mwelekeo kumsifia ndani ya siku 100 hatimaye arudi nyumbani CCM Kulinda masilahi ya chama chake

Chadema wameshafutwa kwenye ramani ya siasa hata kama wangefanyeje
Uzi ujao utakuja kumponda Mama. Akili ya kuku hii
 
Baada ya Rais Samia Suluhu kuwatumia vijana wasio na mwelekeo kumsifia ndani ya siku 100 hatimaye arudi nyumbani CCM Kulinda masilahi ya chama chake

Chadema wameshafutwa kwenye ramani ya siasa hata kama wangefanyeje
Kwa kuwa sifa za ubabe mnazo basi ni kweli mtafanikiwa kuwafuta na ndio maana mnaona hakuna haja ya katiba mpya.
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...
Kumkumbusha Rais ni vyema, lakini bado lazima kuna priorities. Mathalani, Canada wamezuia ndege kusafiri hadi COVID iishe, sasa Mbunge Godbless Lema tutampataje? Tusubiri iishe. Pia kuna katazo la EU kuleta raia zao Tanzania kwa vile hatuna lockdown ya corona sasa tundulissu atakujaje? Ni bora tukasubiri wanyanyue katazo.

Halafu kuna WHO nao wanesema tuvae koboroa saa zote, tutaongeaje? Pia wameamuru tusikae pamoja, mikutano ya Mzee Warioba itafanyikaje?

Mie naona tuchague Kamati Huru kuwasiliana na wananchi maoni yao kwa jinsi ya kuanza. Kamati itoke pande 2 za Muungano watu wanne wanne:

MWENYEKITI - profesarwaitama
MAKAMO - fatmakarume
WAJUMBE VISIWANI - sheikhfarrid/makamo1warais/mwanakombo
WAJUMBE BARA - askofubagonza/mariamsarungi/yegomurume

Hawa ni watu huru hata wewe utakubaliana na mimi. Balanced by gender, balanced by belief, balanced by age, completely neutral and objective. Anza na hiyo. Waapishwe na Jaji Mkuu wa Kenya huyo kabila lake lazima Mluhya ili iendane na BBI. Tusitumie Jaji wa Tanzania, wenzetu Kenya wanatuzidi sana kwa demokrasia.
 
Kila Rais mnamponda tu
Umenifanya ni-smile! Samia nimeamua kumpa muda na anafanya vizuri kwa kweli. Shida ndogo ni kuwa anajaribu kuwafurahisha watu! Pia ana maoni yake yaliyo taofauti na wengine sio kosa! JPM nilim-support ila naye hakuwa malaika. Rais lazima arekebishwe!
 
Hakika viongozi wetu hebu toeni sababu za msingi kwenye mambo mazito.mikutano ya vyama vya siasa ipo kisheria kwa mujibu wa katiba iliyopo.mikutano imezuiliwa sio kisheria ni kwa ubabe wa mtu. ccm wamekuwa wanafanya mikutano watakavyo bila kuzuiliwa.

je kuzuia mikutano kwa hoja ya kujenga uchumi kuna athari gani? hoja dhaifu isiyo na nguvu.viacheni vyama vya siasa vifanye mikutano kwani huko huko kwenye mikutano vitawahamasisha wananchi wafanye kazi walipe na kodi mbali mbali za serikali
 
Hakika viongozi wetu hebu toeni sababu za msingi kwenye mambo mazito.mikutano ya vyama vya siasa ipo kisheria kwa mujibu wa katiba iliyopo.mikutano imezuiliwa sio kisheria ni kwa ubabe wa mtu.ccm wamekuwa wanafanya mikutano watakavyo bila kuzuiliwa...
Shida sio mikutano nadhani. Shida ni hulka za Chadema! Kutakuwa na vurugu mitaani! Tumpe muda Mama. Kaomba muda.
 
Kumkumbusha Rais ni vyema, lakini bado lazima kuna priorities. Mathalani, Canada wamezuia ndege kusafiri hadi COVID iishe, sasa Mbunge Godbless Lema t
Maoni yalishatoka. Na hao uliowasema baadhi ni radicals sana hawana sifa za kuwakilisha maoni ya wananchi bali ya kwao.
 
Shida sio mikutano nadhani. Shida ni hulka za Chadema! Kutakuwa na vurugu mitaani! Tumpe muda Mama. Kaomba muda.
Kwani Chadema imeanza Siasa Awamu ya 5? Shida ni Awamu ya 5 haitaki Wapinzani Wakutane na Wananchi kuwaeleza Ukweli wa Mambo
 
Katiba ya nini saivi hata mwaka hajamaliza, mama alisema tumpe mda
 
Back
Top Bottom