Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.
Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo...
Kumkumbusha Rais ni vyema, lakini bado lazima kuna priorities. Mathalani, Canada wamezuia ndege kusafiri hadi COVID iishe, sasa Mbunge Godbless Lema tutampataje? Tusubiri iishe. Pia kuna katazo la EU kuleta raia zao Tanzania kwa vile hatuna lockdown ya corona sasa tundulissu atakujaje? Ni bora tukasubiri wanyanyue katazo.
Halafu kuna WHO nao wanesema tuvae koboroa saa zote, tutaongeaje? Pia wameamuru tusikae pamoja, mikutano ya Mzee Warioba itafanyikaje?
Mie naona tuchague Kamati Huru kuwasiliana na wananchi maoni yao kwa jinsi ya kuanza. Kamati itoke pande 2 za Muungano watu wanne wanne:
MWENYEKITI - profesarwaitama
MAKAMO - fatmakarume
WAJUMBE VISIWANI - sheikhfarrid/makamo1warais/mwanakombo
WAJUMBE BARA - askofubagonza/mariamsarungi/yegomurume
Hawa ni watu huru hata wewe utakubaliana na mimi. Balanced by gender, balanced by belief, balanced by age, completely neutral and objective. Anza na hiyo. Waapishwe na Jaji Mkuu wa Kenya huyo kabila lake lazima Mluhya ili iendane na BBI. Tusitumie Jaji wa Tanzania, wenzetu Kenya wanatuzidi sana kwa demokrasia.