Inategemea umejipanga vipi! Tatizo si mtoto mdogo ukiwa 60+ tatizo kubwa ni Bibi mdogo akiwa ni under 30, hakuna Rangi utakayokosa kuiona. Mtoto unamfurahia akiwa 5 years hadi 15 years. Hapo uwe ni 75 akiwa binti ni Raha mstarehe.Hapo ndo wanaume wanapozidi kufa kwa kiharusi....
Umestaafu umri miaka 60+, kwa jeuri ya kiume wanajitutumua ng'ombe hazeeki maini anaendelea kutotoa watoto.....
Halafu wanalalamika wanawake wanabebwa wakati mwanamke akifosi sana mwisho kutotoa miaka 50.
Mwanamke akistaafu anakula pensheni yake maana watoto wake wakubwa wanajitegemea sana sana atakuwa anajichangamsha na wajukuu.
Wanaume sasa, kama mzee Mchanga....
Na miaka 70+ unamtoto anatoka shule anaita baba, kesho tunatakiwa kwenda trip ya kishule mchango laki moja....!!
Kama chanzo cha mapato ni pension tuu amekwisha.
NB: Too much of anything is harmful.