Kukosa Upendo: Chanzo cha Tabia na Mahusiano Magumu

Nimependa hii sana
 
Nimependa pia uliposema ulianza safari ya kujitambua. Hapo ndipo mabadiliko ya kweli huanzia. Kujua chanzo cha maumivu hakufuti yaliyopita, lakini hukupa nafasi ya kuacha maumivu hayo yaendeshe maamuzi yako.
Yes, imenichukua miaka na miaka... Kurudia pattern na kufeli, nilianguka na jamii I kasema ni mimi mwenye shida...

Nili weka maneno yao kama uhalisia... Ila baada ya kujua ukweli, nako nilikuja kuwaona wabaya na wajinga...

Ilinifanya kuwa toxic, hakuna mtu niliye mwamini tena.. Hasa hasa nikiwa tukana kwa sababu sikuwa na upendo tena...

Ila baadae nikajua ninawachukia kwa sababu najichukia na hapo ndo nilipo anza kurudi katika true love. Both kwangu na kwao
Can't agree more mkuu umesema kila kitu
 
Hicho ndicho wengi huwa hawakioni. Kuna tofauti kubwa kati ya kujua nani alikukosea na kuendelea kubeba maumivu hayo maisha yote. Umefika hatua ya kutambua kwamba maumivu yasipotibiwa hubadilika kuwa hasira, kutokuamini watu na wakati mwingine kuwadhuru hata wasiohusika.

Nimependa ulivyosema ulipogundua kuwa ulivyokuwa unawachukia wengine, kwa kiasi fulani ulikuwa pia unapambana na nafsi yako. Si rahisi kufika kwenye utambuzi huo. Kuanzia hapo ndipo mtu huanza kujikubali, kusamehe taratibu na kuishi bila kutawaliwa na yaliyopita.

Safari ya kujitambua si ya siku moja, lakini kila hatua unayopiga inakufanya uwe huru zaidi kuliko jana.
 
Bandiko lako linatufundisha na kutukumbusha kwamba sometimes tuwe tunavumiliana humu jukwaani ,sio kila jambo la kubishana ,na sio kila anayebishana na wewe anapenda bali ni trauma ambayo inamsumbua,ndio maana mimi huwa sipendi kubishana sana humu

Nikiona mtu hatuelewani nina jambo moja huwa nafanya nakuacha na kusema Asante ,nikishasema hivyo ujue naacha kubishana
 
Mimi siku hizi nikiona mtu ana tukana hovyo sioni matusi bali naona trauma iliyo jificha ndani yake... Na hapo ndo ni apo pata nguvu ya kumsaidia.. Ila Kuna wengine nawaacha au nawapa benefit of the doubt maana bado hawana mental capacity au uelewa wa kubadilika
Mkuu Ninaposema imenichukua miaka. Ya kuanguka na kuinuka, kufa na kufufuka sitanii. Na watu wengi hawapendi kuingia katika maumivu yao maana ni machungu zaidi
 
Neno asante ni zuri sana, inabidi nianze kuitumia na mimi japo.... Ego yangu inapenda kunikatalia.
 
Neno asante ni zuri sana, inabidi nianze kuitumia na mimi japo.... Ego yangu inapenda kunikatalia.
Anza kidogo kidogo baada ya muda itakuwa sehemu ya maisha yako,to be honest mwanadamu akifanikiwa kuishinda ego yake anakuwa amefikia daraja ya juu sana ya kujitambua

Kwasababu ego hutufanya kujilinda na kujiona sisi bora kuliko wengine,hutufanya tutake kuonekana tupo juu kuliko wengine

Lakini ukimasta ego yako unakuwa huru na hauhitaji validation kutoka kwa watu wengine
 

Uko sahihi kabisa.
 
Actually mimi naona ego sio kitu kibaya, ni ile relationship yetu na ego ndo huleta shida.

Bila ego huwezi kisruvive tena hasa katika dunia hii yenye mashindano kwenye kila kitu... Ego ndo inakufanya umkimbie simba, ila sasa tu nacho kosa ni wisdom ya kujua namna ya kuweza kuishi na ego kiafya zaidi.

Tunaitumia kujiuliza na kuumiza watu wengine disguised as protection mechanism na hapo ndo chanzo cha maumivuu
 
Upo sahihi kila kitu huwa na positive side na negative side,hata hasira sio kwamba haina faida au kuchukia kote huko kuna faida,lakini je kwa namna gani unatumia nyenzo hizo ndio kipengele

Kwahiyo kwa bahati mbaya sana tunatumia ego vibaya,nadhani ni wakati muafaka sasa kujifunza kuitumia vizuri
 
Hakika mkuu

Kuna mwana saikolojia anaitwa Jordan Peterson anasema ga kuwa lazima kwanza uwe beast then uintergrate huo u beast na wisdom...

Kuna shadow ambayo ndo mzizi wa maumivu mengi kujua hiyo shadow lazima ukubali kuwa vulnerable
 
Haya mambo ni kujifunza tu,binafsi baada ya kujua kwamba hakuna maneno ambayo yanaweza kuniumiza au kunikera mpaka nitake mwenyewe,hakuna neno utasema utanikera

Kinachoumiza ni tafsiri ambayo unaipa Hayo maneno,mathalani ukiniambia mimi ni mngese,hauniumizi kwasababu najijua sipo hivyo,so kwanini niumie kwa maoni yako juu yangu

To be honest ndio maana huwa sigombani huwa nawapuuza tu
 
Hakika

Our minds cannot differentiate between imagination and reality ndo maana unaweza kuangalia movie na ukalia... Hata kama una fahamu fika ni maigizoo

Inakutaka uwe soo detached kufikia huko, mimi bado najitahidi sana kufikia huko

Na imenichukua kupitia maumivu makali sana kufikia leo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…