Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbio za sakafuni uwa zinaishia ukingoni.Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.
Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.
Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.
Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?
Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege
Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?
Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?
Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?
Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?
Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.
Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
Muda utaongea .
Kwa kweli Mungu fundi jamani daaaukichunguza vizuri hii thread, wanaopondea wana mihemko kuliko facts! huenda muandishi umepiga kwenye mshono!.
Mkuu, kuna mchezo mpya unachezwa. Mimi nimeuona kama ambavyo niliuona wa JPM kabla haujatokea. Huu wa sasa unaweza kuwa mbaya zaidi.Kila mtu ajishindie mechi zake.
Tuheshimu maoni ya kila mtu na mitazamo, maoni na uhuru wa watu kutoa walichokishudia.
Kila mtu ajishindie mechi zake.
Tuheshimu maoni ya kila mtu na mitazamo, maoni na uhuru wa watu kutoa walichokishudia.
Kila jambo na wakati wake na huu ni wakati wa mama hivyo tunaombeni utulivu
Sitaki..
Ninasikia Sauti ya Magufuli akilia na kulaani kwamba hata kabla hajaoza tayari ameanza kusulubiwa na kulaaniwa hata katika maeneo ambayo alijitahidi kuyaweka sawa.Swali langu ni
Tunajadili ripoti ya CAGNinasikia Sauti ya Magufuli akilia na kulaani kwamba hata kabla hajaoza tayari ameanza kusulubiwa na kulaaniwa hata katika maeneo ambayo alijitahidi kuyaweka sawa
Kwasababu kuna watu WAPUMBAVU wanataka kuwapumbaza watu ya kwamba JPM hajafanya kitu. Tunataka kuwaambia yeyote anayefikiri hivyo, aitishe Uchaguzi Mkuu haraka halafu apande jukwaani aseme JPM hakufanya kitu, awe CCM au Upinzani aone kama atatoka jukwaani salama!!!Hivi mbona legacy ya Nyerer hakuna anayeahangaika hivi kuitetea iendelee kuwepo? WHY huyu?
Mkuu, Mimi narudia tena!! Kuna mchezo mpya unapikwa. Tusikubali iwe ni RAHISI kwa nchi yetu kuyumbishwa na watu kwa matakwa yao. Natamani Mgome ili tuwekewe mifumo imara. Hii michezo hii tunachezewa sio kabisa.Tumtetee jpm Alie tutukana mbili Mara tatu kutwa?
Tumtetee jpm Alie ua ndugu zetu bila huruma kwa kiwatupa kwenye viroba na kuwatumia watu wasio julikana?
Tumtetee mtu ambae baada ya kutuma washenzi wakamuue lisu walimimina risasi 38, akamnyima fedha za matibabu stahili ya mbunge, akakataza watu wasiemde kumwona hospitali na hata tulipo taka kukusanyika kumwombea Lissu akakataza na hata tulipo vaa tshert za pray for Lissu akatukamata???
Tumwombee mtu Alie nyima maslahi ya wafanyakazi?
Tumwombee Alie bomoa nyumba dar na za Mwanza zilizo kua katika mpango huo akasema waziache kwa kuwa ni wapiga kura wake??
Magufuli alikua ni shetani anae tembea,
Mwizi Alie jifucha katika kichaka Cha uzalendo.
Tunamshukuru Mungu kutuondolea kansa hii Kama taifa.
KWENDA ZAKO MAGUFULI, HATUKUPENDI.
Mimi Leo Nasimama Kuhesabiwa,Nasimama Kuonekana ili wakati ukifika basi Iwe kwamba nilisimama.
Natambua kabisa kwamba Hayati Magufuli hakuwa Mbegu Bora kabisa ya kiongozi katika nchi ila kinachoendelea sasa hivi sio dhuluma dhidi ya Magufuli bali ni dhuluma dhidi ya Watanzania ambao ni wazalendo wa nchi hii.Nasema tena hii ni dhuluma dhidi ya Watanzania.
Sijajua Dhuluma hii ni kwa sababu ya Uoga au ni unafiki wa Watanzania.Naona kabisa inatumika nguvu kubwa sana kutaka kuuaminisha umma kwamba miradi yote ya Magufuli ni shody na kwamba sasa ni wakati wa kuiacha.Niseme tu ukweli kwamba kuna weza kuwa kuna matatizo katika miradi hii ila kwa kweli sidhani kama ni sawa kinachoendelea sasa hivi.
Ninasikia Sauti ya Magufuli akilia na kulaani kwamba hata kabla hajaoza tayari ameanza kusulubiwa na kulaaniwa hata katika maeneo ambayo alijitahidi kuyaweka sawa.Swali langu ni
Je ni kweli kwamba hawa wanaotuaminisha leo kwamba kila kitu hakifai kweli wana nia njema na taifa letu?Au nia yao ni kujijengea mazingira ya kuweka mambo yao sawa?